Nahitaji mashine ya kuchonga tooth pick

Nahitaji mashine ya kuchonga tooth pick

Nyakarungu

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2011
Posts
472
Reaction score
377
Wakuu,

Naweza kufahamu hiyo mashine ya kuchonga tooth pick naipataje ikiwa ipo nipeni njia wakuu.
 
Mashine zipo Turnkey Project.study.machine installation and training ni dola 120.000 interested PM for more information.
Wewe unalipa na kutupa eneo la ufungaji machine.raw material ni mabanzi ya mbao toka Iringa
Wakuu naweza kufahamu hiyo mashine ya kuchonga tooth pick naipataje ikiwa ipo nipeni njia wakuu
 
Hii kitu nimefanyia research ya kutosha kiasi, mashine zipo za aina tofauti kuanzia dollar elf tatu mia tano kutokana na uhitaji wako.
Kuna ndugu kasema mabanzi kutoka iringa ni raw materials sawa ila mtu wa kutumia mabanzi ni yule aliye ktk level za juu sana, fanya tafiti.
But ipo mashine inatumia bamboo stick (mianzi) ambayo ni rahisi zaidi na inamfaa muwekezaji mdogo... Good take
 
I

Iko wapi hiyo ya mianzi kaka ua dola 3elfu kwa hapa tz
 
Ukiagika kutoka china, pia afrika hapa hiyo technology wanayo waghana
 
Sasa mkuu, unataka kiwanda kidogo uwekeze kiasi gani... Maana hapo kama milion 15iv mzigo umeupata
 
But fanya kwanza research binafsi then uje na kitu halisi na unachokitaka kweli. Eneo la biashara, workers, management, market strategy and so on
 
Mashine zipo Turnkey Project.study.machine installation and training ni dola 120.000 interested PM for more information.
Wewe unalipa na kutupa eneo la ufungaji machine.raw material ni mabanzi ya mbao toka Iringa
Hzo mashine zinaitwaje ili hata kutafuta taarifa isaidie na iwe nyepesi.
 
Hii kitu nimefanyia research ya kutosha kiasi, mashine zipo za aina tofauti kuanzia dollar elf tatu mia tano kutokana na uhitaji wako.
Kuna ndugu kasema mabanzi kutoka iringa ni raw materials sawa ila mtu wa kutumia mabanzi ni yule aliye ktk level za juu sana, fanya tafiti.
But ipo mashine inatumia bamboo stick (mianzi) ambayo ni rahisi zaidi na inamfaa muwekezaji mdogo... Good take

Mkuu research yako ipo sahihi Ila hizo bamboo ulizo sema kuwa zipo Iringa hazipatikani kirahisi hivyo.

Naomba niongeze details kwenye hiyo research
1. Sio kila mti bamboo/muanzi unafaa kwa toothpick. Inategemea na specie, mti ukiwa mwembamba sana ina affect idadi ya uzalishaji. Pia lazima ujiridhishe kuwa aina hiyo ya bamboo au muanzi haina madhara kwa afya ya binadamu

2. Mianzi unayo iona Iringa wenyeji wanatumia kwa ajili ya kugema pombe ya ulanzi kwahiyo hawato kuuzia kirahisi, kwasababu hii utajikuta unakosa supply ya raw material Kama hauto jipanga. Wapo watu ambao walijaribu wakaleta mashine wakakwama kwenye kupata hiyo mianzi

3. Ili uweze kutengeza toothpick unahitaji mashine zaidi ya moja, kuna ya kukata, kuna ya kuzifanya ziwe smooth na kuna ya kufanyia package. Kwa utafiti wangu mdogo kwenye alibaba unahitaji si chini ya dola 25,000 (bila kodi) kuweza kupata mashine zote hizo. Ila unaweza kuanza na mashine moja ya kukata then packing unafanya manually

Ni hayo tu kwa leo
 
Back
Top Bottom