Nahitaji kumuoa, ila hii ndoa sijui itakuwaje

Nahitaji kumuoa, ila hii ndoa sijui itakuwaje

mahirtwahir

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2013
Posts
614
Reaction score
322
Habari wanajanvi,

Naomba munishauri kwa hekima mimi ni muislamu naruhusika kuoa hadi wake 4 kwasasa niko na 1 nataka kuongeza wa 2.

Mimi kazi yangu ni kutoa huduma kwa jamii, katika kazi yangu hio nimekutana na msichana akanivutia nikaamua kutangaza ndoa na nikasema kabisa kua atakua mke wa 2 hakua na shida akakubali kwa kua dini yangu hairuhusu uchumba wa kuishi ama kua karibu na msichana.

Baada ya kukubali nikaaamua kutoa posa kwao ili nisijekuvunja amri ya 6 na yeye basi wazee wake wakakubali wakanidai mahari fanicha ya ndani nikasema sio shida nikanunua nikaiweka ndani nishawaita wazazi wake wameshakagua wanaulizia harusi nataka ifanyike lini majibu sijatoa kwasababu hizi:-

1. Huyu mwanamke ukimuangalia kashakununia.

2. Kama hupokea simu yake utajuta kwa kulalamika unamzarau.

3. Ukimuelewesha anaona unapiga fix tuuu na hakawii kukuambia yeye basi.

4. Ndani ya miezi 2 kashavunja uhusiano ma 4.

5. Mwepesi yeye kuomba samahani ila ukimuomba yeye utakesa.

Hizo ni miungoni mwa sababu zinazonifanya kama sikua sahihi kumchagua akiingia na tabia hii katika ndoa kila ziku talaka na itakua shida kama mahari yake ni zaidi ya 2.5 milioni.

Waungwana nishaurini
 
Fanicha nimewaonesha tuuu wanakuwa hawaichukui wanaikuta siku akija mwanawao iko ndani
 
Atakusumbua tuu huyo baki na mkeo mmoja usijiongezee stresz
 
So tatizo ni pale mlipoanza kungonoka? Haya kazi kwako mwowaji.
 
Atakusumbua tuu huyo baki na mkeo mmoja usijiongezee stresz
Kweli inaweza kua ni kujiengezea ila jicho langu halijatulia linagharuza sana nje hasa ukizingatia ndoa yangu ina miaka 9 sasa
 
4b91960ca79abdc0b599cba1fa13dc5d.jpg
 
Asinune mchezo wakati anajua kabisa dushe umepeleka kwa mwenzie
Na pesa anahisi nyingi unapeleka kwa mke mkubwa
Wewe acha hizo mkuu nyama ni ileile bako n huyo huyo mmoja huwezi kuwatumikia mabibi wawili kwa wakati mmoja wote wakaridhika
Lazima mmoja apungukiwe upendo na huduma
 
Hujaeleza ile sector nyeti huyo mtoto ni vipiii

Kama kule mashaaalah hayo yote potezea
 
Kuna jamaa aliwahi kusema....
Hakuna upuuzi ulio upuuzi mtupu.
 
Uzinzi utakutafuna tu eenh maana hakuna namna nyingine
 
Habari wana janvi.
Naomba munishauri kwa hekima mimi ni muislamu naruhusika kuowa hadi wake 4 kwa sasa niko na 1 nataka kuengeza wa 2.
Mimi kazi yangu ni kutoa huduma kwa jamii katika kazi yangu hio nimekutana na msichana akanivutia nikaamua kutangaza ndoa na nikasema kabisa kua atakua mke wa 2 hakua na shida akakubali kwa kua dini yangh hairuhusu uchumba wa kuishi ama kua karibu na msichana baada ya kukubali nikaaamua kutoa posa kwao ili nisijekuvunja amri ya 6 na yeye basi wazee wake wakakubali wakanidai mahari fanicha ya ndani nikasema sio shida nikanunua nikaiweka ndani nishawaita wazazi wake wameshakagua wanaulizia harusi nataka ifanyike lini majibu sijatoa kwa sababu hizi:-
1 Huyu mwanamke ukimuangalia kashakununia.
2 Kama hupokea simu yake utajuta kwa kulalamika unamzarau.
3 ukimuelewesha anaona unapiga fix tuuu na hakawii kukuambia yeye basi
4 Ndani ya miezi 2 kashavunja uhusiano ma 4
5 mwepesi yeye kuomba samahani ila ukimuomba yeye utakesa.
Hizo ni miungoni mwa sababu zinazonifanya kama sikua sahihi kumchagua akiingia na tabia hii katika ndoa kila ziku talaka na itakua shida kama mahari yake ni zaidi ya 2.5 milioni .
Waungwana nishaurini


Mkuu unataka kwenda kuoa mombasa au zanzibar maana hizo ndio mahali zao
 
Back
Top Bottom