Nahitaji kujifunza lugha ya kikorea.

Freelancer Wakala

JF-Expert Member
Feb 6, 2016
1,193
828
Habari WanaJF.
Nahitaji kujifunza lugha ya kikorea kwa njia ya mtandao au mwenye kuweza basi msaada tafazali!!

Napenda sana kujua kikorea.
 
Habari WanaJF.
Nahitaji kujifunza lugha ya kikorea kwa njia ya mtandao au mwenye kuweza basi msaada tafazali!!

Napenda sana kujua kikorea.
Unachotaka kujifunza kikorea kwa mtandao kwa maana tukupe site za kujifunza au unataka mwalimu kabisa wa kukufundisha?
 
Comasmita-thank u

Comasmita komaoh au komaoh -thanx very much

Chu ah eeh -i like u

Kamsamnidah-nmesahau kidogo

Abujee-dad

Omunyee-mom

Horabunyee-brother

Hyung nim-respected man as brother

Muyoo? - what?

Unajitahidi lakini umeenda chaka, pronunciation zake hazipo hivyo.

Mfano Hyung~nim ~ kaka. Hiyo ukifanya direct translation utatamka kama "hyu" wakati inatakiwa itamkwe "hyo".

Ni sawa na kampuni ya "hyundai" watu mnasema hyu~nda~i. Ila inavyoandikwa kwa kikorea 현대 inatakiwa itamkwe "hyo~nde".

Nilikaa korea miaka saba kwa hiyo kinapanda sana tu.

Mleta mada sehemu ya kuanzia ni youtube
1. Anza na hangeul (한글) (maandish ya kikorea) jua jinsi ya kuyatamka na kuyaandika, kama una moyo hapa ni siku tatu tu. Ingia Youtube andika "Learn hangeul" kuna video nyingi, pitiapitia.

2. Njoo kwenye maneno common, unaweza anza na salamu za kikorea, hizi nazo pia Youtube utazipata sana.

3. Anza grammar, hapo ndo itakuchukua muda sana kupamaster, kwa grammar nakushauri site hii talktomeinkorean.com ukifika mbali tafuta vitabu vya watoto, utashangaa unaanza kuelewa, baada ya miaka michache utakua unakiongea.
 
Hongera kwa uamuzi wako wa kutaka kujifunza kikorea, ni rahisi sana kujifunza lugha endapo urajidhatiti na kujikita vilivyo katika kutafuta mafunzo ya hiyo lugha. Lugha kama Kikorea ni lugha isiyotumia ROMANIZATION(yaani haiandikwi kwa herufi za kiroma kama A,B,C) hivyo kwenye kuanza kujifunza nakushauri uanze kujifunza kupitia mfumo maalum uliowekwa kwa ajili ya tuliozoea ROMANIZATION, mfumo huo wanauita Hangul, kwa njia ya mtandao waweza angalia videos mbalimbali zenye mafunzo ya namna ya kuiongea hiyo lugha, wakati huohuo ukijibiidisha mtandaoni ni vyema ukawa na apps mbalimbali za kukusaidia wewe kufanya mazoezi ya sarufi. Mojawapo ya app nzuri ya kujifunzia lugha takriban 15 ikiwemo kikorea ni *Rosetta Stone.
Ukiweza kufuata mlolongo huu wa mafunzo yaani kuangalia vipindi vya lugha ya kikorea kupitia Youtube, kufanya mazoezi ya kuiongea kupitia app ya Rosetta Stone na kuangalia tamthilia zao mara kwa mara huku ukiwa makini katika kusikia matamshi na namna wanavyoiongea lugha yao utakuwa njiani kuijua kwa ufasaha kabisa.
Waweza angalia video hii yenye mbinu ya jinsi ya kujifunza lugha yoyote ile yenye kutamkika
 
Nimekaa korea miaka 2 ila sijui chochote lugha nyingine ngumu kumeza....... Inatakiwa ule barger sousage mayai pizza nk ili uweze kuzungumza japo cha kuombea maji.
 
we angalia tu zile tamthilia zao, mi nimeokota si hapa, arattaa = sawasawa. . . . mianee = samahani. . . . . chonaa = mfalme
 
ahjussi..huwa ni kwa mwanaume wa makamo ambae humjui yaan umekutana nae tu hivi ndo unamuita hivyo

ahjumma...huwa ni kwa mwanamke wa makamo pia( kama ndugu au rafiki)
 
Back
Top Bottom