Nahitaji kufunga Drip Irrigation system

Chenery

New Member
Sep 27, 2020
4
6
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, nahitaji kufunga drip irrigation system kwenye shamba langu. Ijapokuwa shamba lenyewe ni kubwa, nafikiria kuanza na eneo nililolichagua, lenye ukubwa wa mita za mraba 4,000 (4000sqm).

Hali ya shamba:
1. Liko tambarare kwa asilimia 90
2. Tayari nina maji ya uhakika ya kisima nilichotoboa kwa mashine/drilling, ambayo yanapanda kwenda kwenye tenki kwa kutumia pampu ya umeme (auto-connected).
3. Nahitaji kulima nyanya

Hoja ya msingi na lengo la kuandika uzi huu: Itanigharimu Tsh ngapi kwa wastani kufanikisha kuunganishiwa drip system? Je, nifanyeje ili kupunguza gharama? Naomba wazoefu wa hii kitu mnipe ushauri. Niko Nyanda za juu kusini.
 
Gharama zote + ufundi gharama itakua milioni 1.8 mpaka 2.2 kutegemea ubora wa vifaa utakavyotumia.
 
Back
Top Bottom