Nahitaji kuanza kutumia pombe

Nahitaji kuanza kutumia pombe

name 97

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2023
Posts
200
Reaction score
553
Nimepitia changamoto nyingi za kimaisha na sasa naona nina stress sana.

Nafikiria kuanza kutumia pombe ili niweze ku-cope na hali hii inayonipelekea kuwa na mawazo sana

Nimekuja kwenu, mnisaidie mambo yafuatayo:

01: Ni aina gani ya pombe inafaa, hasa kwa mtu anaenza.

02: Kutokana na nature ya familia yangu na kazi yangu, ikiwa itajulikana kuwa natumia pombe itawadissapont sana familia yangu na pia itaathiri kazi yangu.

Hivyo basi nataka kutumia kwa siri nikiwa nimetulia 'gheto'..hivyo pombe hiyo ni lazima iwe take-away.

Lakini pia uchumi wangu sio mzuri, naomba pombe hiyo iwe 'cheap in terms of cost' let say iwe less than 5000 per bottle.

Naomba jina la pombe ambayo ina-meet above conditions

Nawasilisha, umri middle 20's
 
Kijana
Sikushauri kunywa pombe na zaidi tafuta starehe nyingine pombe kama huna hela nzuri utaishia kwenye madeni .

Pombe usipoweza kujidhibiti utakuwa na magonjwa ya zinaa kila uchwao .

Pombe ukiendekeza utafeli mipango ya maisha

Mwisho pombe ni uraibu mbaya kuacha sio rahisi .

Siongei nikiwa nyumbani naongea nikiwa bar nakunywa pombe kwa hela yangu ila sitamani uje huku .

Nilianza kunywa pombe nikiwa na miaka 14 , sasa mimi kwa maelezo yako ni baba yako , nilitamani kuacha nikiwa na miaka 29 sijafanikiwa mpaka sasa na uzee huu .

Pombe imenipunguzia heshima kwa jamii kubwa iliyodhani mimi ni mtu wa heshima kwa elimu yangu na kazi yangu .

Pombe imenipunguzia ufanisi kazini , pombe imepelekea sasa nina gonjwa lisilotibika japo lipo katika early stage hivyo naweza kupambana kupona nikiamua .

Pombe imenifanya vitu vingi kuamuliwa na ndugu na mke hata kama kitu naona naweza kuamua mwenyewe lakini bado naamuliwa kwa nguvu .

Ndugu sikushauri kunywa pombe , watakuja vijana sio muda watasema nakunywa matuputapu wambie sijaanza kunywa pombe Tanzania hivyo wakumbushe nje hakuna mataputapu .

Usinywe pombe .
Kwasasa Mbeya pazuri .
 
nimepitia changamoto nyingi za kimaisha na sasa naona nina stress sana,

Nafikiria kuanza kutumia pombe ili niweze ku-cope na hali hii inayonipelekea kuwa na mawazo sana

nimekuja kwenu,mnisaidie mambo yafuatayo:

01:ni aina gani ya pombe inafaa,hasa kwa mtu anaenza

02:Kutokana na nature ya familia yangu na kazi yangu,ikiwa itajulikana kuwa natumia pombe itawadissapont sana familia yangu na pia itaathiri kazi yangu

Hivo basi nataka kutumia kwa siri nikiwa nimetulia 'gheto'..hivo pombe hiyo ni lazima iwe take-away

Lakini pia uchumi wangu sio mzuri,naomba pombe hiyo iwe 'cheap in terms of cost' let say iwe less than 5000 per bottle

Naomba jina la pombe ambayo ina-meet above conditions

Nawasilisha,umri middle 20's
Nakukuhakikishia ukianza kunywa pombe,unaongeza changamoto nyingine mpyaaaaa maishani mwako. Usijaribu huko
 
5f752389564f8.image.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom