Nahitaji gari ya kubebea taka haraka (kununua ama kukodi)

Nahitaji gari ya kubebea taka haraka (kununua ama kukodi)

Abramovic

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2013
Posts
324
Reaction score
610
Habari ya majukumu wakuu? Bila kupoteza muda niende kwenye mada, Mimi ni mfanyabiashara wa biashara mbalimbali ikiwemo mafuta, gesi n.k. Lakini pia mbali na hayo mimi nina kampuni ya ukandarasi wa taka, hua nachukua tenda za kuzoa taka katika mitaa na halmashauri mbalimbali hapa nchini hususani hapa Dar. Kwa sasa nina kazi ya kuzoa taka ktk Jumla ya mitaa 15 hivyo unaweza kuona ukubwa wa kazi iliyopo.

Sasa changamoto ninayokumbana nayo ni ukosefu wa gari ya uhakika ya kupiga kazi suala linalopelekea ufanisi wa kazi kupungua na kutokamilisha kazi kwa wakati. Hivyo basi kwa sababu humu kuna watu wa kila aina, naomba nitangaze kua nahitaji gari kwa ajili ya huduma hiyo. Iwe ni ama ya kununua kabisa au kukodi.

Gari ninayotaka hapa ni yoyote yenye uwezo wa kubeba taka ila yenye kubinua (tipper) itapewa kipaumbele zaidi.

NB : Kama mnavyojua gari ya taka haina complications sana Kikubwa tu iwe inatembea so sihitaji gari mpya, nataka iliyotumika kweli kweli ila iwe na hali nzuri na inayotengenezeka.

Kwa yeyote anayehusika na ujumbe huu Tafadhari tuwasiliane PM au whatsapp 0715 143 900 au barua pepe hgecompany@gmail.com

Natanguliza shukurani zangu za dhati!
 
Hivi hawakukagua uwezo wa mkandarasi kabla ya kukupa Tenda?Kwa nini usifanye sub contract?
 
Hivi hawakukagua uwezo wa mkandarasi kabla ya kukupa Tenda?Kwa nini usifanye sub contract?
Mkuu gari ninayo sema haikidhi mahitaji kama navyotaka mimi, kwa mtu mwingine akiwa na hii gari kama yangu inamtosha lakini mimi nna mtazamo tofauti. Napenda kukamilisha kazi yangu kabla ya muda wa deadline. So lazima niongeze idadi ya gari. Kwa mfano kazi ya siku 5 mi napenda niikamilishe within 3 days.
 
Back
Top Bottom