Nahitaji bodaboda

Bandabichi

JF-Expert Member
Jun 3, 2012
230
42
habari wanajamvi. Nahitaji pikipiki aina ya SUN LG CC 150 kwa hapo Dar duka gani napata kwa bei nafuu. Coz huku mikoani bei kinyama.
 
Kwahuku dar zinapatikana duka moja kariakoo, lakini sikumbuki jina lake, mara ya mwisho ilikuwa 1.9 milion.

Lakini kwanini unahitaji hiyo ya cc 150? Niliwahi kuona jamaa mmoja wa bodaboda anauza yakwake nilipomuuliza akaniambia inakula sana mafuta, nilipomuuliza kwanini alinunua hiyo, akasema alikuwa hafahamu kuwa 150cc zinakula mafuta sana kwa kuwa injini ni kubwa sifa yake nikwamba zinanguvu sana lakini kwabiashara ya bodaboda hazifai.

Angalizo jingine nikwamba ukitafuta pikipiki aina hiyo lazima uwe muangalifi kwasababu zipo feki zake muda sio mrefu utaanza kusikia kama manyanga.
 
Nakushauri uende dukani, hivi vitu vya mkononi wakati mwingine vinaweza kukuletea shida. Kuna jamaa alinunua simu kumbe aliyeporwa ni marehemu tayari halafu akakutwa nayo, sijui atasemaje?
 
ningekua mie ningeahirisha kununua yani kuuliza tu bei unapewa angalizo la kununua sanda dah:confused2::whistle:
 
Angalia sana mkuu ukishanunua usijifundishe kuendesha asubuhi halafu jioni ukabeba abiria.
 
Hii haikufai?
 

Attachments

  • http___a3.img.mobypicture.com_13f27fd64ad720747e58afb38fd8f5ed_view.jpg
    http___a3.img.mobypicture.com_13f27fd64ad720747e58afb38fd8f5ed_view.jpg
    30.8 KB · Views: 93
Back
Top Bottom