Nahisi wana JamiiForums wakitumika katika kuwafanyia 'interview' Wagombea Urais tutampata aliye bora kabisa!

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,548
108,882
Habari zenu!

Nisiwaficheni kama kuna kitu ambacho kila uchao / siku ' nakiombea ' siku moja kiweze kutokea hapa nchini Tanzania ni kufanyika kwa utaratibu ' maalum ' kabisa ambapo Wagombea Urais wote nchini Tanzania kutoka Vyama Vyote wawe wanafanyiwa Usaili wao ( Interview ) moja kwa moja na Members kutoka Mtandao wangu huu pendwa kabisa wa JamiiForums.

Yaani kule Ukumbini awepo tu ' Moderator ' mmoja pamoja na Wagombea wote ambapo Maswali yote atakuwa anayotoa Kwetu Sisi huku Members kisha na Wao ( Wagombea ) wanajibu na kila Mgombea atakuwa anapewa Swali lake tofauti na mtindo wa sasa ambao Swali moja linaulizwa kwa Wagombea wote.

Nina uhakika Mtandao wa JamiiForums ukitumika kufanya hili ambalo naliombea kila siku liweze kutokea na kufanikiwa Tanzania inaweza ikapata Kiongozi ( Rais ) ambaye atakuwa ' Kipanga / Mwerevu ' hasa kwa masuala mbalimbali na tutakuwa tuna uhakika nae kwani tayari atakuwa ameshachujwa vilivyo na Jamvi hili la Great Thinkers.

Mungu lifanikishe hili.

Nawasilisha.
 
Hapana yaani unaamanisha hawa mamluki wa vyama vya siasa waliojaa mahaba ndiyo watuletee mgombea bora hapana nakataa kabisa
 
Naunga mkono hoja, japo siku hizi JF imevamiwa na wajinga kibao. Twitter nayo ingefaa zaidi.
 
Kuhusu Raisi ni jambo la siri sana sio rahisi kama utoavyo maoni yako. Fanya rejea uongozi wa kimila wa eneo lako na hii yote inafanyika kwasababu ya usalama wa nchi, taifa ambao ni watu pamoja na fikra za huyo atakaye chaguliwa au kupendekezwa.
Hii dunia haipo sawa na huru kama uifikiriavyo kuna mambo mengi hayaonekani ila yanamadhara makubwa endapo ukikosea kuweka mtu ambaye si sahihi.
Ni kweli nchi na taifa kwa ujumla tunapitia mambo mengi ambayo huenda ni magumu ila tuwe wavumilivu, tuweke imani kwa wale wachache wenye kuijua nchi na michezo michafu ya dunia inavyoenda watuwekee mtu sahihi japo kila mwanadamu anamapungufu yake.
 
Members wa JF kasoro wanaCCM hapo tutakuwa pamoja, ili tukiyahusisha na haya maCCM yaliyopo humu katika hiyo interview lazima tutapata kichaa kama huyu tuliyenae sasa
 
hapa sasa hivi kuna uchadema na uccm wengi wanasapoti vyama badala ya kusapoti au kukosoa hoja mfano mada ya Paskal juu ya dereva wa Tundu Lissu kufichwa badala ya kujadili hoja wanamjadili mtoa hoja.labda hilo lingefanyika miaka mitano iliyopita ambako watu walikuwa wanajadili hoja makini
 
"Mheshimiwa Rais, niache niseme na unisikilize, ukinipeleka hivyo sitoweza kujibu..." — John Heche
(mb) Tarime vijijini Mara paaap akanyang'anywa kipaza sauti.

Magufuli uvumilivu sifuriiiiiiiiii
 
Habari zenu!

Nisiwaficheni kama kuna kitu ambacho kila uchao / siku ' nakiombea ' siku moja kiweze kutokea hapa nchini Tanzania ni kufanyika kwa utaratibu ' maalum ' kabisa ambapo Wagombea Urais wote nchini Tanzania kutoka Vyama Vyote wawe wanafanyiwa Usaili wao ( Interview ) moja kwa moja na Members kutoka Mtandao wangu huu pendwa kabisa wa JamiiForums.

Yaani kule Ukumbini awepo tu ' Moderator ' mmoja pamoja na Wagombea wote ambapo Maswali yote atakuwa anayotoa Kwetu Sisi huku Members kisha na Wao ( Wagombea ) wanajibu na kila Mgombea atakuwa anapewa Swali lake tofauti na mtindo wa sasa ambao Swali moja linaulizwa kwa Wagombea wote.

Nina uhakika Mtandao wa JamiiForums ukitumika kufanya hili ambalo naliombea kila siku liweze kutokea na kufanikiwa Tanzania inaweza ikapata Kiongozi ( Rais ) ambaye atakuwa ' Kipanga / Mwerevu ' hasa kwa masuala mbalimbali na tutakuwa tuna uhakika nae kwani tayari atakuwa ameshachujwa vilivyo na Jamvi hili la Great Thinkers.

Mungu lifanikishe hili.

Nawasilisha.
Naona kichaa chako kinahitaji dawa sasa..wahi ukatibiwe kijana.
 
Back
Top Bottom