Nahisi nimekumbwa na jini mahaba

Nahisi nimekumbwa na jini mahaba

ENDELEA KUTUMIA DAWA MKUU. AU RUDI TENA UKASOMEWE JINI MAHABA ANAKUWA MBISHI SANA KUTOKA MWILINI.
 
hatari sana sheikh, huyo mtaalam wako wa mwanzo alikua ni sheikh au mshana jr!?
 
Habarini JF members, kifupi nikwamba nilivurugwa nikaamua kumfata mtaalam anisaidie. Mpenzi wangu alirudisha mapenz kwa kasi ya ajabu ila kumbe nilikua nimekosea njia kwasababu mwisho wa SIKU mwili wangu ulibadirika nikajawa HOFU YA AJABU, nguvu za kiume kupungua kwa kasi, ugomvi kila siku na mpenzi wangu, hamu ya kufanya mapenzi ikapungua kwa kasi kwa wanawake na kujawa sana na hamu ya kuwaingilia wanaume wenzangu au kama ni mwanamke basi nimuingilie kinyume na maumbile, kichwa kikavurugika akili ikawa kama imefungwa.

Nilihangaika huku na kule nikabaini kua nimesaidiwa na mtaalam katika namna ya kurogwa (kutupiwa jini) sasa nikakutana na sheikh mmoja siwez kumtaja akanisomea na kunipa dawa ya kupaka kiukweli nilipata nafuu sana ila nahisi bado maana kunawakati zile hali zinanijia japo so kwkasi kama mwnzo, hofu imepungua japo bado ipo kiasi.

Nachoshangaa bado ni kutokwa na jasho ambalo linatoa harufu kama ile ya mpenzi wangu ila nkiligusa nilinuse vizuri ile harufu siisikii lakini nikitulia upepo ukipita makwapani inatoka harufu ya mpenzi wangu.

Kingine ni kwamba bega langu la kushoto linakua linatembelewa na vitu ndani ya mwili sehem hiyo ya bega na nakua na hasira na butwaa visivo kawaida.
NISAIDIENI NATESEKA MIE


SAFARI YANGU YA MIAKA 3 YA MATESO YA JINI MAHABA MPAKA KUPONA KWANGU

Ndugu zangu nawasalimu habari zenu!

Niende moja kwa moja kwenye dhumuni ya kuandika huu uzi. hii ni true story.

Mwaka 2019 nilipatwa na tatizo la kutupiwa jini mahaba na mtaalam wa mchongo ambaye alitake advantage kwangu baada ya kumkimbilia anisaidie, nadhani kama ulisoma maelezo yangu ya hapo juu utanipata na tutaenda sambamba.

Nilipopatwa na tatizo hilo kiukweli nilipoteza vitu vingi including muda, pesa, marafiki, kuaminiwa na watu, utu na madili mengi ya pesa.

Nilitembea kwa wataalam wa jadi, watumishi wa Mungu na wengine wengi wa kila aina ili tu kupata suluhu. Kifupi zilinitoka pesa mingi sana siwez hesabu nitaishia kutoa machoz. twende moja kwa moja kwenye jinsi vile nilivopona mpka naandika uzi huu am fine very fine.

Huo mwaka 2019 kipindi napatwa na hili tatizo sikua home wala karibu na home. Na sikua nimewaambia home maana nilihisi ningepata aibu na ningewafamya wajskie very disappointed on me. Lakini baada ya kurud home sikuweza kuendelea kuficha maana kwa yeyote ambaye aliishi namm kwa muda kidogo kabla ya tatizo angeniona baada ya kupata matatizo bas angegundua kabisa kwamba nina matatizo. Nyumbani nilikuwa naishi na mama na dadaangu, mama ni mtu wa dini na maombi sana, nilipofika nyumbani walinipokea na zikapita siku mbili siku ya tatu mama aliniita nakumbuka ilikuwa ni asubuhi, alivoniita akanikarisha chini na akaanza kunihoji. Nakumbuka aliniuliza kama niko sawa siumwi chochote namm nilikaza nikaficha kwamba nipo sawa kumbe nilikuwa najidanganya mwenyewe na mama alikuwa keshagundua tayar kwamba mwilin mwangu kuna shida. Alinisisitiza nimwambie ukweli, niliendelea kukaza kiaina lakini mwishoni nilikubali nikaeleza kila kitu. Mama alinambia ya kwamba kwa zile siku mbili nilizokuepo pale nyumbani mama aliona mambo mengi ya ajabu juu yangu. aliniambia ya kwamba anaona kuna mwanamke anakuja usiku na anaingia chumbani kwangu katika namna isiyo yakawaida na baada ya muda kidogo anaskia vurugu kama mtu anahangaika hapo kitandani kumbe ni lile jini mahaba lilikua linakuja linanikojolesha hafu linasepa na kweli kwa zile siku zote mbili nilikua napata ndoto za ngono yani nlikuwa naota nazagamua warembo wa aina tofaut tofaut.

MAOMBI YAKAANZA
Nilisomeshwa sala ya toba na baadae maombi yalianza, kifupi baada tu ya maombi kuanza nilijikuta naanza kukakamaa na kuingiwa na nguvu za ajabu na baada ya hapo sikuweza kunotice vzr kilichoendelea lakini mama alinihadithia ya kwamba nilianza kutamka maneno kwa ukali kwamba "sitokiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii" lakini baada ya moto kuzidi nikaanza kusema "natoookaaaaaaaaaaaaaa" na mwishoni nikaregea sana na kuishiwa nguvu kwa hali isiyo ya kawaida na baada ya kusalia chini kwa muda kidogo baada ya kazi kuisha basi nilipata nafuu na nguvu za kuinuka na tukaanza kuongea na mama. Tulizungumza mambo mengi na yalijikita katika kunihasa kumtegemea mungu na niliahidi kutorudia kwenda kwa waganga na nikamgeukia Mungu. yani kilichonifanya niamini kwamba kweli jini katoka ni kurelax kwa mwili, kurudi kwa faham akilini na macho nilikuwa nakodoa sana lakini yalirud kuwa kawaida na nilikuwa napigwa sana na butwaa lakini haya yote yalipotea mara moja.

BAADA YA JINI KUTOKA
Safari haikuishia hapo, nakumbuka baada ya kufanyiwa maombi zilipita kama wiki mbili huku mwili ukiwa unapitia mabadiriko mbalimbali kujirud katka hali yake ya kawaida. Mabadrko makubwa yalikuwa ni relaxation ya mwili mzima ikiwemo misuli hali ambayo ilinipelekea kulazwa hosptal na haya yote mama alikuwa ananiambia kwamba nisijali ni mabadrko ya mwili tu na niyakawaida kwahiyo hosptal nilipewa madawa mengi na kifupi nilipatwa na kama stroke maana upande wa kushoto wote ulikuwa haupo sawa. Nilikuwa natembea kwa kuchechemea na nilipoteza uwezo wa kuongea kwa takriban siku 4 lakini haya yote mama alikuwa ananambia nisihofu ni hali ya kawaida na kweli baada ya kupatiwa matibabu hosii nilipona na mpka saii nipo sawa na nipo kazini na namshukuru sana Mungu kwa kuniokoa na kunitakasa. Nimeamua kurudisha mrejesho kwenu kwasabb nilipokuwa na matatzo niliandika uzi kuomba ushauri na nilipewa ushauri japo wengine walinitolea maneno mabaya ya kunikatisha tamaa Mungu awasamehe na walionipa ushauri mzuri nawashukuru sana kwasababu ushaur wenu ulinisidia kwa namna moja ama nyingine. Nachotaka kuwaomba tusikimbilie kwa waganga chonde chonde.

I REST MY CASE! MAY GOD BE WITH YOU! AMEN
 
Mkuu ukiachwa, achika mambo yakulazimisha mapenzi ni hatari mno.

Hasahasa hiyo njia uliyotumia ili upendwe wakati mwenzako hakupendi ulikosea sana, bado uko na nafasi fanya toba na uungame mwenyezi Mungu atakusamehe na kukuokoa katika hilo janga.

Pole sana.
 
Ukienda tu kwa mganga once
Tayar umejenga mnara wenye network yenye nguvu mnooooo
Endelea kuhudumia wateja tu.

Ulipoenda kwa mlozi haukuomba ushauri leo ndio umekuja sasa

Usisumbukie ya dunia itakumeza

Kachukue uchawi kabisa uweze kukontrol jini mahaba
Nakuona litakavyokutajirisha


Tunapambana na wasiojulikana nyie mnawatafuta?

Nawaza lingekuwekea hali ya wewe kutaman kuingiliwa sijui ungefanyaje?

Mkuu pambana na hali yako usitikise za wenzako
 
Habarini JF members, kifupi nikwamba nilivurugwa nikaamua kumfata mtaalam anisaidie. Mpenzi wangu alirudisha mapenz kwa kasi ya ajabu ila kumbe nilikua nimekosea njia kwasababu mwisho wa SIKU mwili wangu ulibadirika nikajawa HOFU YA AJABU, nguvu za kiume kupungua kwa kasi, ugomvi kila siku na mpenzi wangu, hamu ya kufanya mapenzi ikapungua kwa kasi kwa wanawake na kujawa sana na hamu ya kuwaingilia wanaume wenzangu au kama ni mwanamke basi nimuingilie kinyume na maumbile, kichwa kikavurugika akili ikawa kama imefungwa. Nilihangaika huku na kule nikabaini kua nimesaidiwa na mtaalam katika namna ya kurogwa (kutupiwa jini) sasa nikakutana na sheikh mmoja siwez kumtaja akanisomea na kunipa dawa ya kupaka kiukweli nilipata nafuu sana ila nahisi bado maana kunawakati zile hali zinanijia japo so kwkasi kama mwnzo, hofu imepungua japo bado ipo kiasi. Nachoshangaa bado ni kutokwa na jasho ambalo linatoa harufu kama ile ya mpenzi wangu ila nkiligusa nilinuse vizuri ile harufu siisikii lakini nikitulia upepo ukipita makwapani inatoka harufu ya mpenzi wangu. Kingine ni kwamba bega langu la kushoto linakua linatembelewa na vitu ndani ya mwili sehem hiyo ya bega na nakua na hasira na butwaa visivo kawaida.
NISAIDIENI NATESEKA MIE

hukupata hamu ya wewe kuingiliwa kinyume maana ndio jini mahaba wanataka nahisi umeingiliwa kinyume ila unaona aibu kusema
 
Vipi huyo mpenzi wako bado mko naye ama mapenzi yameota mbawa tayari?
 
hukupata hamu ya wewe kuingiliwa kinyume maana ndio jini mahaba wanataka nahisi umeingiliwa kinyume ila unaona aibu kusema
Ningesema coz nitatizo but sijawahi kuingiliwa wala kuingilia mtu kinyume kwani tiba niliokwisha ianza ilinisaidia kwakiasi kizuri
 
Ukienda tu kwa mganga once
Tayar umejenga mnara wenye network yenye nguvu mnooooo
Endelea kuhudumia wateja tu.

Ulipoenda kwa mlozi haukuomba ushauri leo ndio umekuja sasa

Usisumbukie ya dunia itakumeza

Kachukue uchawi kabisa uweze kukontrol jini mahaba
Nakuona litakavyokutajirisha


Tunapambana na wasiojulikana nyie mnawatafuta?

Nawaza lingekuwekea hali ya wewe kutaman kuingiliwa sijui ungefanyaje?

Mkuu pambana na hali yako usitikise za wenzako
Asante sana na unadhani kua hilo ndo tatizo kubwa kuliko mengine yote duniani nadhani lakini yamkini tatizo ulonalo wewe likawa ni kubwa kuliko langu ila hujui tu pengine
 
Hivi hawa wanawake walivojaa hivi kuna watu wanaenda hadi kwa waganga kurudisha wapenzi wao? Haya ndio madhara ya kumoenda mtu moja kupita kiasi na ndio maana mimi nishasema sitopenda sana na sitopenda mwanamke moja ila ninachokifanya ni kupiga show ya maana yaan hata mwanamke akinigundua kuwa nina mwanamke mwingne hawezi niacha kwa urahisi maana shuguli angu ndani ya 6*6 akikumbuka anatokwa na machozi
 
Cheki marinda vzr. Jini mahaba lazima kwanza akuingilie uani ndio akutawale vzr
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom