Aisee chief ogopa sana stress za kudhani umeambukizwa, dah nilipata maralia hapo hapo, kwenda kupima nikakutwa na typod, sijakaa sawa uzito ukaanza kushuka, hilo halijaisha nikawa nahisi homa nikajua chalii yenu hapa nimeumaliza mwendo, nikaandika uzi humu wakanishauri vema wengine wakaniongezea vitisho kupima nako naogopa.
Kubwa zaidi nikabackup mihondomolo yangu nikagundua kuna ngono zembe nishafanya kama mara tatu daaaaah weweeeeeeeeeeee.
Ila nikaja kujipa ujasiri wa kupima dah sikuamini kama kipimo kimeonyesha negative, nilifurahi na hofu kimtindo nikarudia tena kama mara tano sehemu tofauti majibu ni yale yale negative nikasema asante muumba.
Hofu ni mbaya sana.
Nilichofanya ni kukata mawasiliano yote na wanawake ambao niliona hawa sio sawa kuendelea nao.