Nahisi mbwembwe za Oktoba Tunatiki kama zimefifia

Manyanza

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
19,147
Reaction score
43,079
Maneno ya Humphrey Polepole yameweka hadharani kile ambacho tulikuwa tukisema kwa miaka mingi – CCM si chama tena cha siasa, bali ni kampuni ya mafisadi wenye maslahi binafsi.

Amedai wazi kuwa mchakato wa kumpata mgombea wa urais ndani ya CCM umekiuka kanuni, taratibu na miongozo ya chama chao. Hii inamaanisha kwamba hata kabla ya uchaguzi kufika, figisu na njama za kifisadi zilishapangwa mezani.

Amefichua pia jinsi CCM wanavyoiba kura hadharani, jambo ambalo wananchi wamelalamikia mara nyingi lakini wakazimwa kwa risasi, mabomu ya machozi na vitisho vya dola.

Aliwataja Rostam Aziz na Jakaya Kikwete kama vinara wa mtandao wa kihuni ndani ya CCM, mtandao ambao umegeuza siasa kuwa mradi wa kifamilia na kibiashara huku Watanzania wakiachwa na umaskini, deni la taifa na ukandamizaji wa demokrasia.

Na sasa ameweka bayana kuwa vyama vya ACT Wazalendo na Chaumma si wapinzani wa kweli – bali ni projekti za CCM zilizoundwa kudhoofisha upinzani wa kweli. Wapinzani halisi ni CHADEMA, chama pekee kilichosalia kupigania maslahi ya wananchi bila hongo wala hila.
 
wanajipanga, kufurukuta. Lucas yupo kwa liheso. atatuma 'mada ya kumjibu polepole'
 
Vita ni vikali mno
 
Back
Top Bottom