Nahisi mbinu chafu Bodi ya mikopo ie HESLB

Nahisi mbinu chafu Bodi ya mikopo ie HESLB

Edobeny

Senior Member
Joined
Nov 26, 2014
Posts
143
Reaction score
29
Wiki mbili zilizopita nilimtumia mdogo wangu hela ili ajaze form ya kuomba mkopo HESLB. Baada yakulipia 30000/= kwa Mpesa akapewa ID ambayo ndio password yake ya kuingia na kujaza form.

Lakini kila anapoingiza inamwambia the identity does not much wakati mwingine inamwambia the system does not recorgnize the number akajua labda ni mtandao tu sasa ni wiki ya pili bado haikubali . Deadline ya kuomba ni 30/6/2015.

Itafunguka lini? Atajaza lini? Adownload na kuprint hardcopy na kuituma HESLB lini ? Tatizo limewakuta vijana wengi tena wako mikoani huko hawana uwezo wa kuja Dar kufuatilia physically.

Wameweka namba ya simu lakini ukipiga inaita tu haipokelewi. Je hizi ni njama za makusudi za kupunguza idadi ya waombaji wa mikopo au ni nini hasa kinaendelea?

Mwenye uelewa wa jambo hili karibu tushirikishane.
 
Nahisi wengi sana wanaweza kukosa mikopo mwaka huu kwa kigezo cha mtandao unasumbua.
 
hiyo ni network tuu MKUU Mimi pia imesumbua sana mwambie kufanya usiku ndo poa watumiaji wanakuwa wachache Mimi nilifanikiwa juzi
 
hiyo ni network tuu MKUU Mimi pia imesumbua sana mwambie kufanya usiku ndo poa watumiaji wanakuwa wachache Mimi nilifanikiwa juzi
Ulijaribu kwa muda gani au siku ngapi?
 
Kama hali itaendelea hivi mpaka Deadline, ntaomba msaada wa kisheria ili niishitaki HESLB na warudishe 30000/= aliyolipia mdogo wangu
 
Mimi nimejaza almost 90% but kuna kipengele cha kuselect district, sasa pale sioni wilaya hata moja hata ukuselect ile sehemu ya kuonesha list
 
kumbuka ni Mpesa tu..km umetumia mitandao mingine iyo ni sadaka tu ukatafute nyingine
 
huu ni ukiritimba kama sio urasimu.

Lleo niliwafuata HESLB, mlinzi anasema kuhusu matatizo ya form hawana huduma za ana kwa ana bali wameweka namba ya simu pale nje na ndo hiyo ambayo haipokelewi. Kibaya zaidi mlinzi anasema muda wa kazi ni saa mbili hadi saa saba tu.
 
Back
Top Bottom