Nahisi maumivu

Nahisi maumivu

wida

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2014
Posts
247
Reaction score
40
Samahani wana jamvi,

Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 21, nipo na mpenzi wangu kwa mda wa miaka mitatu sasa tulianza mahusiano tangu tupo o-level, kiukwel nampenda, mnamo mwezi ulopita alinibadilikia ghafla.

Nilijitahidi kumuuliza kwa kutumia simu ya rafiki yangu kwani laini zangu kazifungia binafsi niliumia kwa hali hiyo ila nilipo muuliza sababu akajibu nilimwambia kila mtu awe kivyake.

Niliwaza ni mda gani nilitamka kauli hiyo, hadi sasa bado kafungia laini zangu kiukweli bado nampenda ila sifahamu nini nifanye awe kama zamani kwani bado nampenda.

Kutokana na vishawish nikapiga simu kwa mganga flani huko mkoani na akanijibu;

MGANGA: Kiukweli bado huyo mwanamke anakupenda na unauwezo wa kumrudisha

Binafsi naogopa kwani mapenzi ya dawa haya dumu, naombeni ushauri ndugu zangu kwani bado nampenda, nilijaribu kumsau ila nimeshindwa kwa mazoea.

Naombeni ushauri msinitukane wala kejeli
 
Ushauri atakupa huyo hyo mganga.!we ni mchawi,tena mchawi haswa na nyie ndo mnaoua maalbino kwa imani zenu za kishenzi..!
 
Aiseee humu kuna grit thinkers...semi grit thinkers..na vilaza typical
 
Inawezekana ulimwambia. muombe msamaha. Alafu usitumie simu. kama unapafahamu anapoishi nenda ukaongee nae ana kwa ana.
 
Ushauri atakupa huyo hyo mganga.!we ni mchawi,tena mchawi haswa na nyie ndo mnaoua maalbino kwa imani zenu za kishenzi..!

Sio km nimeenda ndugu yangu ila nilipiga tu cm, na wala sina mpango wa kwenda ila nakirikukosea kwa step hiyo, naomba ushauri nifanyeje ili mpenzi wangu arejee
 
Inawezekana ulimwambia. muombe msamaha. Alafu usitumie simu. kama unapafahamu anapoishi nenda ukaongee nae ana kwa ana.

Ahsante ndugu yangu ntajaribu
 
Mh! Jipende kwanza kisha nafsi yako itakuelekeza kifuatacho. Au umefilisika
 
Sio km nimeenda ndugu yangu ila nilipiga tu cm, na wala sina mpango wa kwenda ila nakirikukosea kwa step hiyo, naomba ushauri nifanyeje ili mpenzi wangu arejee

Kimsingi hakupendi kama wewe unavyompenda ndio maana kakuacha njia panda! Kama unajua anapo ishi nenda umfate usipige simu!

Achana na tabia za kukimbilia kwa waganga kwani huo ni uchawi kabisa! Huyo mwanamke akikataa sio mwisho wa maisha yako tulia piga kitabu wanawake wamejaa utapata mwingine..mwanamke asikufanye uwe mchawi kataa hilo kabisa kwa vitendo!
 
Ushauri atakupa huyo hyo mganga.!we ni mchawi,tena mchawi haswa na nyie ndo mnaoua maalbino kwa imani zenu za kishenzi..!

teh teh teh teh nimecheka sana najiulza unaweza ukawa unaonekanaje?
 
Unajua ifike mahali usilazimishe mtu ambaye hujapangiwa na mungu, subiri wa kwako atakuja tu, isitoshe we bado kijana mdogo sana. Jenga maisha yako kwanza mengine yatajileta yenyewe, muombe sana mungu.
 
kila kitu utokea kwasabab zake...move on kijana
 
Sio km nimeenda ndugu yangu ila nilipiga tu cm, na wala sina mpango wa kwenda ila nakirikukosea kwa step hiyo, naomba ushauri nifanyeje ili mpenzi wangu arejee

Raha sana.... unapiga sim kwa nganga.... then mganga anakupa mchongo mzima??,
vip mganga ulimlipa kwa M-pesa?
 
Mkuu, achana na mambo ya waganga, mganga kaongea ili apate hela ila jua hata demu asiekupenda anaweza kurogwa akanasa kwako.

Wew piga chini, sahau. Halishindikani hilo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom