puker
JF-Expert Member
- Nov 22, 2018
- 940
- 1,847
Habari za muda huu wanajamvi.
Niingie moja kwa moja kwenye lengo mahususi la uzi huu. Kama kichwa cha habari kinavyoeleza.
Leo ni siku ya tatu kuna maumivu yamezuka ghafla mithili ya mtu aliyeungua na mafuta ya moto au mvuke katika sehemu ya tumbo langu upande wa kushoto.
Maumivu hayo yalianzia mgongoni kwa mbali nikahisi ni kawaida labda ni uchovu na pilika za mjini. Nikapuuza.
Lakini kadri masaa yanavyozidi kusogea yanaongezea mpaka kufika maeneo ya tumboni upande huo huo wa kushoto.
Cha ajabu hakuna vipele, wekundu wala dalili yoyote inayoonesha kama ngozi au mwili una hitilafu. Nina mpango wa kwenda kucheki hospital kesho Mungu akinijalia uhai. Lakini pia nimeeleza hata labda kuna hatua za kuchukua ili tatizo lisiendelee kuwa kubwa.
Pia nikitathmini siku za karibuni hakuna Jambo au tukio lolote linaloweza kusababisha maumivu haya.
Naombeni msaada tafadhali. Yani hata nguo naona inaniumiza.