Nahisi kudata

Nahisi kudata

sabuni jr.

Member
Joined
Oct 14, 2014
Posts
19
Reaction score
4
Kuna binti nilitokea kumpenda sana wakati nasoma o level sikubahatika kudoo nae ila nilimpenda sana na yeye alinipenda sana, baada ya olevel nilikwenda
A level boarding mikoani mbal na nyumbani, toka a level mpaka chuo na sasa nimemaliza chuo nimeanza kazi sijawahi kumuona tena nilimpenda sana na sijawahi kupenda msichana mwingine tena zaidi yake hiyo hali imepelekea mpaka sitamani wasichana kabisa nimekuwa mpenzi wa pombe tu.

Nahisi kuchanganyikiwa maana now sijielewi bila pombe silali usiku.

Sijui nifanyeje?
 
Acha ubwege ww! Ww sema ukweli tu kuwa unaipenda pombe na imekukolea ila usisingizie mapenzi.

Unadata na mtu ambaye hujamfunua utupu?

Mbaya zaidi unajihakikishia kabisa kuwa et nayeye alikupenda sasa kwann hajakutafuta kama alikupenda?

Acha utoto bwana mdogo piga kazi ule maisha sasa ww endelea kuwaza na utakuja kuwaza sana sku unastaafu huna hata banda la kuku wala taili la baiskeli
 
Bora uchanganyikiwe kabisa ili uende milembe tujue moja
 
Inaonekana wewe ni katoto sana na hata huu mwandiko wako unaonesha hivyo .....

Ukikua utaacha tu ...!!
 
Wacha pombe kwanza kisha anza kujihusisha na michezo, burudani nyinginezo tofauti na ulevi, jichanganye na watu pia kama itawezekana lakini kujichanganya kuwe kwa yaliyo mema
 
Back
Top Bottom