Nahisi kichwa kupasuka kwa mawazo

Nahisi kichwa kupasuka kwa mawazo

chafu pozi

Member
Joined
Oct 9, 2017
Posts
66
Reaction score
58
Habari zenu wakuu,nimekuwa na mahusiano na binti mmoja huu ni mwaka wa nne na niwe mkweli tunapendana sana na uyu binti maana mapenzi ameyajulia kwangu kwani mimi ndiye niliye mtoa bikra,tangu mwezi wa nne mwaka huu huyu binti anataka mimi nipereke barua kwao kwa ajili ya uchumba rasmi,lakini kwa kipindi hiko chote anachotaka nipeleke barua kwao mimi nilokuwa bado sijamaliza chuo kikuu ila ndo nikiwa katika mwaka wangu wa tatu wa masomo yangu.

Baada ya kumaliza mwezi wa saba mama yake alinita na kuniambia nimuoe binti yake kwani nitakaa kwao maana wana nyumba kubwa tu,mimi nikapinga kwa hilo na kuwaambia wanisubiri kidogo nitafute kazi maana mimi siwezi kukaa ukweni lakini hali bado inazidi mpenzi wangu anazidi kudai tu na anasema nipeleke japo barua.kiukweli nampenda sana huyu manzi maana ana sifa zote nazotaka kuanzia uzuri mpaka tabia,ila tatizo bado sijapata kazi na vyuma vimenikazia kwelikweli.

Jamani waungwana naombeni ushauri wenu nifanye nini kwenye situation kama hiyo?
 
Upo tayari kuoa? jibu hapana, sasa kipi kinachokupa shida? Umelazimishwa? Dogo, uoe kwa mapenzi yako na sio ushawishiwe utakuja kulia tena hapa. Mwanaume wa wapi wewe

Joverest amesdisco udsm
Hapana kwa kushawishiwa nilikataa mkuu maana nilihaidiwa mpaka makazi nikagoma
 
Oa ukaishi ukweni kama umesoma la kwanza hadi chuo kikuu hata nyumba ya vyumba vitano huna unategemea nini kama si mama mkwe kwenda kukufuga kwenye hekalu lake ili akikutaka pia usifurukute maana atakuwa anakulisha
 
Mkuu mambo bado ndo kwanza nimemaliza mwaka huu
 
Upo tayari kuoa? jibu hapana, sasa kipi kinachokupa shida? Umelazimishwa? Dogo, uoe kwa mapenzi yako na sio ushawishiwe utakuja kulia tena hapa. Mwanaume wa wapi wewe

Joverest amesdisco udsm
hahahah jose ni Tiss yulee boss huwa anaingia humu kwa kazi maalumu ..
Atarudi baada ya mwezi mmoja
 
vyuma vimekukazia ee? chelewa chelewa mwisho utakaziwa
 
Habari zenu wakuu,nimekuwa na mahusiano na binti mmoja huu ni mwaka wa nne na niwe mkweli tunapendana sana na uyu binti maana mapenzi ameyajulia kwangu kwani mimi ndiye niliye mtoa bikra,tangu mwezi wa nne mwaka huu huyu binti anataka mimi nipereke barua kwao kwa ajili ya uchumba rasmi,lakini kwa kipindi hiko chote anachotaka nipeleke barua kwao mimi nilokuwa bado sijamaliza chuo kikuu ila ndo nikiwa katika mwaka wangu wa tatu wa masomo yangu.

Baada ya kumaliza mwezi wa saba mama yake alinita na kuniambia nimuoe binti yake kwani nitakaa kwao maana wana nyumba kubwa tu,mimi nikapinga kwa hilo na kuwaambia wanisubiri kidogo nitafute kazi maana mimi siwezi kukaa ukweni lakini hali bado inazidi mpenzi wangu anazidi kudai tu na anasema nipeleke japo barua.kiukweli nampenda sana huyu manzi maana ana sifa zote nazotaka kuanzia uzuri mpaka tabia,ila tatizo bado sijapata kazi na vyuma vimenikazia kwelikweli.

Jamani waungwana naombeni ushauri wenu nifanye nini kwenye situation kama hiyo?
Kama kwel unampenda na anakupenda bac mtasikilizan na kuaminiana..pata kazi,shusha mjengo, weka mke...Ukweni sio mahala sanifu pa kuanzia maisha ya hustling..
 
Back
Top Bottom