Tatemahunda
JF-Expert Member
- Sep 14, 2013
- 232
- 91
Wakuu salaam!
Siku chache zilizopita nilikuja humu kuomba ushauri kuhusu mguu kuvimba, ulianza kuvimba tu bila maumivu na ulianzia chini kwenye vidole hadi kwenye goti, sijawahi kuumiza, nilishauriwa humu ndani Mara moja kuwahi hospital, nikafanya hivyo.
Cha kwanza dokta aliniandikia nikapimwe matende, nikalazimika kulala hospitali. Usiku wakaja wahusika na kuchukua damu, ila ilionekana sina vimelea vya matende. Nikarudi tena kwa Mara nyingine nikaandikiwa kupima figo, ini pamoja na X-ray kwenye maeneo yaliyovimba, ila pia ilionekana niko salama.
Hofu inakuja kwamba isije ikawa ni matende, maana unafanana kabisa na muathirika wa matende, naogopa isije ikaja kugundulika muda ambapo ishakua sugu tayari, kuna wakati nawaza labda ningejua dawa za matende ningenunua nijinywee tu sasa.
Naombeni ushauri wenu tena kwa mara nyingine., natanguliza shukurani