Karibu ughaibuni. Elimu ni ile inayokuwezesha kutawala mazingira yako. Ikuwezeshe kuishi popote katika sayari hii na kustawi. Sasa naweza kusema shuleni ulielimika. Wengi wenu mkifika Dar mnajiona mko "on top of the world". Mnajiona mmepata "trophy" maishani. Wewe ni mfano wa kuigwa kwa wadogo zetu. Hapo Botswana leseni ya udereva inaisha muda wake baada ya miaka 5, siyo mitatu kama Bongo. Gaborone kuna parking lots za kutosha. Hautolipia tena ku-park kwenye ardhi ya Mungu. Gaborone ina wakaazi kama lakh 3 hivi na magari machache lakini barabara zao ni pana ajabu. Hakuna foleni. Unaweza kukaa sehemu yoyote ya mji na kuamka saa 12:30 asubuhi, ukaoga, ukala kifungua kinywa na bado ukawahi kazini. Malls kubwa ziko kila mahali. Siyo Dar yenye wakaazi mil 5 lakini ina ka-Mlimani City tu. Cost of living iko chini ukilinganisha na Afrika Kusini.