Nafikaje Mbulu Manyara

Nafikaje Mbulu Manyara

SON OF THE LAND

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2015
Posts
204
Reaction score
210
Wakuu naomba msaada jinsi ya kufika mbulu Manyara kwa barabara, na mabasi gani mazuri luxury tafadhari na makadirio ya nauli sh ngapi
 
unatokea sehemu gani?
kama unatokea dar kwa ndege ukishuka KIA Panda shuttle mpaka arusha mjini(45 km) tsh 10000,then unaenda stendi kuu ya arusha unapanda shuttle noah za karatu(147 km) tsh 7000
then karatu - mbulu kuna land cruiser tsh 5000.

bus panda dar express ya karatu 35,000 ukishuka panda land cruiser za mbulu tsh 5000.
 
Thanx Obama natokea Dar na ni kwa basi
 
Ukifika Arusha, uliza Majengo Bar kuna Landcruiser nauli haizidi 20,000. Safari zinaanza saa moja asubuhi saa saba uko Mbulu
 
Thanx nimepata direction pia nami naenda mbulu.
 
Mkuu ongera kwa kwenda huko ila usisahau kondom

Kuna watoto wazuri kama wazungu au brazili ahahahah
 
Wakuu naomba msaada jinsi ya kufika mbulu Manyara kwa barabara, na mabasi gani mazuri luxury tafadhari na makadirio ya nauli sh ngapi

Karibu sana Mbulu,fika majengo bar asubuhi sa 1 upande kruza ni masaa matatu tu,nauli 12,000
 
unatokea sehemu gani?
kama unatokea dar kwa ndege ukishuka KIA Panda shuttle mpaka arusha mjini(45 km) tsh 10000,then unaenda stendi kuu ya arusha unapanda shuttle noah za karatu(147 km) tsh 7000
then karatu - mbulu kuna land cruiser tsh 5000.

bus panda dar express ya karatu 35,000 ukishuka panda land cruiser za mbulu tsh 5000.

Anaweza pitia Magara pia
 
Nakushauri panda mtei express ya Babati lala hapo then siku ya pili panda cruiser kuelekea mbulu, hizo cruiser za kutoka Arusha yanachosa sana maana mnabanana sana alafu kuna kaumbali lakini za Babati mtabanana ila si mbali sana
 
Mimi pia kuna siku nitaenda.... Haydom inacost how much
 
Duh nimefuta bahati mbaya ila
Minjingu-Mbuyu wa Mjerumani-Magara-Mbulu
Karatu-Daudi-Mbulu
Dareda-Dongobesh-Mbulu

Zote hizo ni njia kuu za kukufikisha Mbulu.

Gharama ni 20000 from Arusha
Au nenda kalale Karatu au Babati.

Ukifika Mbulu Lala Paris Lodge na chakula kapate Aljazeera restaurant.

Ukikwama nipm
 
Nilishawahi fika Lake Manyara Hostel na kuna sehemu inaitwa Mto wa Mbu i hope ni maeneo ya huko huko... palikuwa pamechangamka kiaina maana tulikuwa kwenye safari ya utalii wa Ndani so eneo kama hilo ni motomoto ila tuliambiwa sifa zake hapo magari na matruck huegeshwa pembezoni na mengi hufanya kama sehemu ya kupumzikia wakiwa safarini
 
Siku ikifika nitakuwa nishajipanga so nitaeleza fresh nitakapokuwepo...

Kifupi
Nikapanda ya Hydom inapatkana ktk njia kuu ya Singida Arusha
Kama unatoka Arusha Basi Ukifika Dareda kunja left then utafika Katesh na nusu saa ivi utafika hiyo junction kula kulia nako utaenda kama 1hr hadi Hydom.

Au route Nyingine ni from Singida ambapo utafika hiyo junction kabla ya Katesh
 
Nilishawahi fika Lake Manyara Hostel na kuna sehemu inaitwa Mto wa Mbu i hope ni maeneo ya huko huko... palikuwa pamechangamka kiaina maana tulikuwa kwenye safari ya utalii wa Ndani so eneo kama hilo ni motomoto ila tuliambiwa sifa zake hapo magari na matruck huegeshwa pembezoni na mengi hufanya kama sehemu ya kupumzikia wakiwa safarini
Mto wa mbu ni njia ya kwenda Karatu zikitokea Makuyuni Junction.
Karatu Unaweza kwenda Mbulu au kuingia Ngorongoro kiongozi.

Kama JPM vile, karibu na Mwanza
 
Poa Mkuu lakini nahisi nitakuwa nikitokea Dar na lazima nitue Arusha Kwanza
 
usisahau kupitia mamaisara,gehandu na tlawi..
 
Back
Top Bottom