Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,558
- 41,078
Kabla ya shambulio la kigaidi la Hamas, kulikuwa na wafanyakazi 21,000 toka Gaza waliokuwa wakifanya kazi Israel.
Baada ya shambulio hilo la Oktoba, na vita vinavyoendelea, Waziri wa usalama wa Israel bwana Itamar Ben-Gvir, amesema kuwa kutokana na uhasama wa Waarabu wa Gaza unaozidi kuongezeka dhidi ya Israel, hakuna mfanyakazi atakayeruhusiwa kutoka Gaza kuingia Israel kufanya kazi. Hivyo kutakuwa na upungufu wa wafanyakazi 21,000 kwenye sejta mbalimbali.
Wakati huo huo, waziri wa fedha wa Israel, bwana Smotrich, amesema kwamba hakuna hata shekel moja itakayopelekwa kwa utawala wa Gaza kwa sababu hayupo tayari kutoa pesa kwa mamlaka ya Gaza ili ikalipe mishahara itakayoenda kutunza familia za magaidi.
Wanaohangaikia ajira, mnaweza kuitumia hii nafasi, kama walivyofanya wenzetu wa Kenya na Malawi.
HABARI ZAIDI
Mpaka sasa vifo vya wapalestina ni zaidi ya 17,700. Kati ya hao, 7,000 ni wapiganaji wa Hamas na makundi yenye mafungamano nayo. Israel, toka October 7 mpaka sasa imepoteza askari wapatao 400. Mapigano yote yapo ndani ya Gaza na Westbank. Ndani ya Israel, tangu vita ianze, hakuna shambulizi lililosababisha kifo chochote, kutokana na ubora wa mifumo ya ulinzi wa anga.
Habari ndani ya Israel ni kwamba vita itaendelea kwa miezi 2 zaidi. Mwezi miwili imewakuta Wapalestina zaidi ya 17,700 wakipoteza maisha. Miezi 2 ijayo huenda itafikisha vifo vya Wapalestina zaidi ya 20,000.
Wakati magaidi wa Hamas na wanaowaunga mkono wanastahili wanachokipata, tuzidi kuwakumbuka wanadamu wale wasio na hatia, mkono wa Bwana ukawalinde ili wakivuke kipindi hiki kilicho kigumu sana kwako.
Hekima ikawapate watawala wa Dunia, ili ikiwezekana, watoto na wale wanaojulikana si sehemu ya haya makundi ya kigaidi (yaani wao si sehemu ya wapiganaji wala si miongoni mwa wanaounga mkono mbinu za magaidi), wawatafutie mahali salama, hata nje ya Gaza.
Maisha ya mwanadamu Duniani ni mafupi sana, hayastahili kufupishwa kwa mtutu wa bunduki, isipokuwa kwenye mazingira yasiyozuilika, kama vile uwepo wa huyo mtu kunaondoa maisha ya watu wengine. Hamas ni haki yao kupukutishwa, lakini wale wasiohusishwa nao, wana haki ya kuishi.