Jamii Opportunities
JF-Expert Member
- Feb 10, 2014
- 5,158
- 1,688
WAKALA WA MABASI YAENDAYO HARAKA
Kumb Na: AB.23/134/01-I/46 06 Machi, 2020
TANGAZO LA AJIRA YA MUDA MFUPI
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka, anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi wazi tatu (03) kama ilivyobainishwa katika tangazo hili.
1. MHUDUMU WA MAKUNDI MAALUM – NAFASI 3
SIFA ZA MWOMBAJI
Awe na Elimu ya kidato cha nne na amehitimu elimu ya cheti cha mafunzo (NTA Level 4) katika fani ya maendeleo ya jamii/Ustawi wa jamii kutoka vyuo vya maendeleo ya jamii vinavyotambuliwa na Serikali.
MAJUKUMU YA KAZI
- Kutambua na kuhudumia watu walio katika makundi maalum,
- Kukusanya takwimu zinazohusu watu walio katika Makundi maalum wanaopita katika vituo,
- Kutoa taarifa ya utekezaji wa kazi zake kila wiki,
- Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na Elimu, uzoefu na ujuzi wake.
MASHARTI YA JUMLA
- Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania,
- Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa,
- Waombaji wote wawe na umri usiozidi miaka 45,
- Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees)watatu wa kuaminika.
- Maombi yote yaambatane na vyeti vya kidato cha nne, taaluma, kwa wale waliohitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika waambatanishe vyeti vya mafunzo husika.
- Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA
- Picha moja “Passport size” ya hivi karibuni.
- Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na Baraza la Mitihani Tanzania –(NECTA).
- Uwasilishaji wa taarifa, nyaraka na sifa za kugushi, wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
- Mwisho wa kupokea maombi ya kazi ni tarehe 19 Machi, 2020.
MTENDAJI MKUU,
WAKALA WA MABASI YAENDAYO HARAKA,
UBUNGO MAJI,
BARABARA YA MOROGORO,
S.L.P 724,
DAR ES SALAAM.
LIMETOLEWA NA;
MTENDAJI MKUU
WAKALA WA MABASI YAENDAYO HARAKA
2
WAKALA WA MABASI YAENDAYO HARAKA
2