AKO Group Ltd inayofanya kazi zake Barrick Gold Mine (Bulyanhulu) inakaribisha maombi ya watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi 5 za kazi katika idara ya Usafi (Housekeepers) kutoka katika vijiji/maeneo yanayouzunguka mgodi
MAJUKUMU MUHIMU USAFI(HOUSEKEEPER)
Kusafisha vyumba vya wateja na mazingira yake kwa kiwango kinachohitajika na kampuni
Utunzaji wa vifaa vyote vya usafi na vya wateja kwa ujumla
Utekelezaji wa kiwango cha juu cha huduma kwa wateja ukiwa mgodini
Kuhudhuria vikao vya utendaji kazi kila siku na muda uliopangwa
Kutunza siri za kampuni
Kufuata utaratibu na maelekezo mengine yote atakayopangiwa na kiongozi wake
VIGEZO
Elimu kidato cha nne na kuendela
Cheti katika fani ya Hotelia
UZOEFU UNAOHITAJIKA
Uzoefu usiopungua mwaka mmoja ikiwa ni pamoja na kufahamu mambo yote mhimu katika fani husika
Uzoefu wa kupokea malalamiko na kuyatatua kwa wakati
Awe anafahamu kusoma na kuandika (kiingereza ni muhimu zaidi)
Awe na uzoefu wa kufanya kzi katika hoteli yenye hadhi ya nyota tano atapewa kipaumbele
Maombi yanaweza kuandikwa kwa lugha ya Kiswahili au iingereza pamoja na wasifu CVs yapelekwe katika ofisi za AKO mapokezi au tuma kwa barua pepe eemmanuel@akogrouo.co.tz
Kama haujapigiwa simu na AKO ndani ya siku 5 baada ya siku ya mwisho ya kupokea maombi, basi ujue ombi lako halijafanikiwa utajaribu tena wakati mwingine
Tuma maombi kablaya tarehe 14/05/2020 saa 11:00 jioni