Nafasi za kazi 200 NARCO | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nafasi za kazi 200 NARCO

Discussion in 'Nafasi za Kazi na Tenda' started by Sojochris, Feb 27, 2012.

 1. S

  Sojochris Member

  #1
  Feb 27, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  NAFASI ZA KAZI ZA WAKALA MAUZO “SALES AGENTS”

  “Kongwa Beef” ni Nyama yenye Ubora wa Kimataifa inayozalishwa na NARCO, Kampuni ya Ranchi za Taifa Limited ambayo hivi sasa inafanya maboresho ya namna ya kuwafikia wateja wake wa nyama ya “Kongwa Beef”. Ili kuhakikisha tunawapatia wateja wetu huduma zinazozidi matarajio yao, tumeamua kutoa nafasi 200 za Wakala Mauzo “Sales Agents” kwa vijana wa kike na wa kiume wa miaka 18-30. Hii ni fursa muhimu sana kwa vijana wote wenye uzoefu au wanaopenda kujenga uzoefu na kufanya kazi katika upande wa Masoko na Ujasiriamali.

  Kama unashauku ya kupata nafasi ya kutafuta oda za “Kongwa Beef” kutoka kwa wateja, basi hii ni nafasi yako.


  MAJUKUMU YA WAKALA MAUZO WA “KONGWA BEEF”
  • Kutangaza Ubora wa Kongwa Beef na kutafuta oda kutoka kwa wateja kwenye maofisi, mahoteli, na taasisi mbalimbali.
  • Kugawa vipeperushi na kushawishi wateja kununua “Kongwa Beef”.
  • Kukusanya na kutunza kumbukumbu za wateja na mauzo
  • Kuelimisha wateja wajue Ubora wa Kongwa Beef

  MALIPO NA FAIDA UTAKAZOPATA
  • Utalipwa kwa kila kilo moja ya nyama utayoleta oda na kuhakikisha imemfikia mteja kupitia wasambazaji wetu.
  • Kadiri utakavyoleta oda nyingi zaidi na kuhudumia wateja vizuri zaidi ndivyo utakavyopata kipato ki-kubwa zaidi.
  • Utakutana na mazingira mazuri ya kufanyia kazi na kupata changamoto za kujiendeleza kitaaluma na kimapato.
  • Utapata mafunzo ya masoko, biashara na ujasiriamali ili kukuwezesha kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.
  • Vyeti vya heshima na vya mafunzo vitatolewa
  • Utapata fursa ya kuendeleza ujuzi na taaluma yako katika fani za biashara,ujasiriamali na masoko.

  TAALUMA NA UZOEFU UNAOHITAJIKA
  Mwombaji:-
  • Awe na uwezo mkubwa wa kutoa huduma inayozidi matarajio ya wateja.
  • Awe na uwezo wa kujieleza vizuri kwa Kiswahili.
  • Uwezo wa kuongeza Kiingereza kwa ufasaha itakua ni sifa ya nyongeza
  • Awe mwenye shauku ya kuuza sana.
  • Uwe na uwezo wa kuandaa na kutunza kumbukumbu za wateja na taarifa za Mauzo na Masoko.
  • Awe Mbunifu na Anayependa Kujiendeleza

  NAMNA YA KUTUMA MAOMBI
  • Andika barua kwa mkono bila kuchapisha na uambatanishe “CV” yako pamoja na barua kutoka kwa wadhamini watatu (3) mmoja kati yao awe mzazi au mlezi wako. Barua ziwe na namba za simu za wadhamini
  • Ambatanisha namba za simu na anuani ya barua pepe kama unayo.
  • Ambatanisha barua kutoka kwa Serikali za Mitaa iliyogongwa Muhuri na yenye picha yako.
  Maombi yote yatumwe kwa:

  Meneja Mkuu,
  Kampuni ya Ranchi za Taifa Ltd (NARCO),
  Mavuno House, Azikiwe Street,
  S.L.P 9113,
  Dar es Salaam.

  Simu : +255 22 211 0393/211 1956
  Barua Pepe: info@narco.co.tz
  Tovuti: www.narco.co.tz

  Tuma maombi yako kwa kuleta mwenyewe ofisini au kwa Posta. Kila tutakapopokea maombi tutayafanyia kazi mara moja.

  *********Wahi Wateja Wanatusubiri Tuwahudumie**********
   
 2. libent

  libent JF-Expert Member

  #2
  Feb 27, 2012
  Joined: Oct 29, 2011
  Messages: 385
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Ahsante mkuu ila mwisho wa kuapply ni lini?
   
 3. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #3
  Feb 27, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,005
  Likes Received: 739
  Trophy Points: 280
  Poa mkuu
   
 4. S

  Sojochris Member

  #4
  Feb 27, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  First to come first to be saved but wawe na vigezo hadi post zitakapojaa.
   
 5. Tanganyika1

  Tanganyika1 JF-Expert Member

  #5
  Feb 27, 2012
  Joined: May 10, 2011
  Messages: 396
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  umesomeka mkuu....
   
 6. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #6
  Feb 28, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,653
  Trophy Points: 280

  Dah, Mkuu hii ni best Business Opportunity...mtu unakula jasho lako!! am very impressed kuona kitu kama hii ambayo ina-motivate uwajibikaji kwa sasa inatumika na govt agency! Palipo na 200 Sales Agents, lazima pawepo pia na Team Leader. Mie nasubiria hizo posts za Team Leader.
   
Loading...