nimeona nitoe ufafanuzi kidogo, kwanza hili ni kanisa na linafanya kazi na shirika la kikristo hivyo kila shirika lina mission na dira. sasa hivi tukiajiri mtu asie mkristo atawezaje kusimamia maono na utume wa huduma. kama tungekua na ubaguzi basi tungeishia kutangaza kanisani tu lakini tangazo limetangazwa kuanzia kanisani na pia tumeona tuwatangazie na watanzania popote wenye vigezo wajaribu bahati yao. kama una vigezo bila shaka hauwezi kulalamika. kumbuka hii ni kazi ambayo ndani yake ni huduma ya kumtumikia Mungu kwa njia ya watoto maskini na kwa muktadha wa kazi na majukumu inakubidi uwe ni mtu wa kudumu wa mahali hapo . sasa nakushauri kuliko kuwapotosha watu kama haujakidhi vigezo ni heri kuwaachia wenzako watafakari na kuomba kazi. kila kazi ina sifa na vigezo vinavyohitajika . kwahiyo hakuna kosa lolote lililofanyika kwa kutangaza nafasi hii humu. na si lazima kila jambo likufurahishe ndio lionekane jema kwa kila mtu. nawatakia kazi njema
usitake kupotosha watu hapa lengo ni kuwabadilisha dini vijana wote mtakaowachukua kuwalea ambao si dini yenu sasa mkimuweka mtu ambaye si wa dini yenu atafichua mnayoyafanya