Nafasi ya wazee katika jamii | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nafasi ya wazee katika jamii

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Juniour K, Mar 9, 2012.

 1. Juniour K

  Juniour K Member

  #1
  Mar 9, 2012
  Joined: Mar 8, 2012
  Messages: 54
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wazee wana nafasi muhimu sana kwa jjamii yeyote,ni kiungo na hamasa kwa maisha ya wanajamii katika jamii yeyote,wazee ni alama ya utimilifu wa maisha ya mtu hata jamii,wazee ni walezi kwa watoto na vijana.

  Nilipata kumsikia siku moja Baba mtakatifu akisifu heshima inayotolewa na jamii kiafrika kwa wazee wao,kwamba wazee barani Afrika ni utajiri,hawatengwi hawdharauliwi bali wanabaki kuwa miamba na walezi wakuu wa mila na desturi katika jamii tofauti na nchi za magharibi(tusipokuwa makini Watanzania tunaelekea huko).

  Katika jamii zetu za kiafrika wazee wamechukua nafasi kubwa katika kutatua migogoro na kuharakisha misamaha na Amani katika jamii,Amani na utulivu vilivyopo Tanzania vimejengwa katika mabaraza ya usuluhishi ambamo wazee ndio waamuzi.

  Wana JamiiForums kwa machache hayo tumwache Rais wetu aongee na wazee huenda tukapata uvumbuzi wa tatizo hili, watu wanakufa, ndugu, rafiki, dada, wazazi hata watoto wetu.

  Asanteni.
   
 2. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #2
  Mar 9, 2012
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 160
  Mkuu wangu,

  Umesikika vema kabisa na umeeleweka.

  Jiulize: Ataongea na wazee au atawahutubia wazee lakini akimaanisha kuhutubia taifa?
   
Loading...