Nafasi ya vyombo vya habari katika kuchochea mgogoro wa Tanzania na Rwanda

Rose Mayemba

JF-Expert Member
May 7, 2012
721
1,017
Taarifa iliyopo ni kwamba mnamo tarehe 21 Mei 2013 wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Umoja wa Afrika (AU) Addis Ababa nchini Ethiopia, ulipofika wasaa wa Mh. Rais Jakaya M. Kikwete kusema aliyokuwa nayo, alitumia fursa hiyo kuishauri serikali ya Rwanda ikiongozwa na Raisi Paul Kagame juu ya hali ya amani nchini Congo. Alimsihi ya kwamba ili hali ya amani irejee, hana budi kufanya mazungumzo na kundi la FDLR, waasi wa Kinyarwanda walioko Congo.

Ushauri huu ulikuwa kama cheche kwenye kichaka maana kilichofuata hapo ni kama ambavyo tumeshuhudia serikali ya Rwanda ikionyesha kugadhabishwa kwa hali ya juu kutokana na ushauri huo.

Kabla sijarejea kwenye mada kuu iliyonifanya niandike, ningependa kuchambua ushauri huu kimtizamo binafsi na kwa kutuma utashi (common sense) ambao kila mwanadamu amejaliwa. Mtu anapokushauri jambo, na zaidi zaidi awe ni mshirika wako (katika hali hii wahusika ni maraisi wa nchi jirani), unaweza kuuchukua ushauri huo na kumshukuru, pengine hata kumdadisi juu ya namna ya kuufanyia kazi kwa maono na maoni yake. Pili, kama ni ushauri usioshabihiana na mtizamo wako au utashi wako juu ya mambo, utaukataa. Ni jambo la nadra sana kukuta mtu anakataa ushauri kwa ukali na lugha ngumu kama aliyotumia Mh. Kagame labda awe na ukosefu wa staha (kitu ambacho siamini raisi wa Rwanda kapungukiwa kwacho). Hivyo basi inanifanya niamini kukaripiana huku ni hatua ya mwisho kabisa ya tatizo ikiashiria kuwa kumekuwa na misuguano ya chini kwa chini ambayo kwa namna moja au nyingine haikufika kwenye vyombo vya habari. Hata hivyo, naepuka kujihusisha na utabiri (speculations).

Nini basi alichokisema Raisi Paul Kagame? Alipokuwa akihutubia wahitimu wa mafunzo ya kijeshi katika chuo kilichopo Musanze, mnamo tarehe 10, Juni 2013, (nitanukuu na kutafsiri yale muhimu kwa mujibu wa video ipatikanayo mtandaoni (youtube) iitwayo (President Kagame on Kikwete’s statement) alisema

“…nilisikia kuna baadhi ya watu walikuwa na mambo ya kusema kuhusu Rwanda kufanya mazungumzo, kujadiliana na wauaji wa watu wetu…watu wanaizungumzia FDLR kirahisi rahisi hivyo…na wanajua wanazungumzia makaburi haya ya watu wetu, na kwamba wale waliofanya hivi (waliofanya kitendo cha mauaji)…tuna deni kwao. Hata hivyo, awali sikusema kitu juu ya hili, kutokana na mosi, kuchukizwa nalo, pili nilifikiri ni upuuzi mtupu, tatu, labda ilitokana na umbumbumbu, nne…kama ni tatizo la kimlengo, (na nadhani ndio tatizo kuu) basi tatizo hilo ni bora likabaki na wenye nalo…lakini tutapata siku nyingine ya kulikabili hilo (tatizo)…”

Ikafuata hotuba ya Mh. Raisi Kikwete mwishoni mwa mwezi Julai ambayo ilisheheni mambo kadha wa kadha likiwemo la uhusiano baina ya Rwanda na Tanzania. Nitanukuu yale machache nyenye manufaa katika andiko langu hili;

“…napenda kuwahakikishia watanzania wenzangu na ndugu zangu wa Rwanda kuwa mimi na serikali ninayoiongoza tunapenda kuwa na ushirikiano mzuri…mimi na serikali ninayoiongoza tutakuwa wa mwisho kufanya vitendo vibaya dhidi ya serikali ya Rwanda au nchi yoyote jirani au nchi yoyote duniani…napenda kuwahakikishia ndugu zetu wa Rwanda kuwa kwa upande wetu hakuna kilicho badilika wala kilicho pungua katika uhusiano na ushirikiano..

…kwa upande wangu binafsi, sijasema lolote kuhusu Rwanda, pamoja na maneno mengi kutoka Rwanda na viongozi wake, pamoja na maneno mengi ya matusi na kejeli kutoka kwenye vinywa vya viongozi wa Rwanda dhidi yangu…sio kwamba sisikii, wala si kwamba siambiwi yanayosemwa au sijui kusema, au sina la kusema, la hasha! Sijafanya hivyo kwasababu sioni faida yake…”

Kwa mtizamo wa karibu wa hotuba hizi mbili; yaani ile ya Mh. Kagame na ile ya Mh. Kikwete zina ujumbe (tone) tofauti. Wakati ile ya awali ikionekana kutoka kwa mtu mwenye gadhabu, ya mwisho inaonekana ikitaka kusawazisha hali (atmosphere) ilo tengenezwa na ile hotuba ya mwanzo.

Shida inakuja pale vyombo vya habari vinapozinasa hotuba hizi mbili na kuamua kuleta muktadha viutakavyo vyenyewe sijui kwa manufaa ya nani.

Gazeti la Mwananchi, Agosti 3 lilibeba kichwa cha habari kisemacho “Kikwete amvaa Kagame, amshangaa kwa lugha za matusi na kejeli.” Jambo la kujiuliza hapa ni je? kulikuwa na “kuvaana” kupi katika hotuba ya Mh. Raisi, kama sio kutia chumvi kwenye kidonda? Muandishi wa makala husika alimnukuu raisi Kagame kwa kusema,

“…nilinyamaza kimya kwasababu sikupenda kusikiliza ushauri kuhusu FDLR, kwa sababu nafikiri ni upuuzi ulioambatana na ujinga. Hatuwezi kuacha maisha yetu kama Wanyarwanda tunavyoishi sasa. Ushauri wa kikwete ni sawa na kucheza na makaburi ya watu wengi ambao ni ndugu zetu”

Kwa mtu makini ni rahisi kugundua kuwa nukuu hii imeongezwa chumvi hasa ikizingatiwa kwamba Rais Kagame hakumtaja Raisi Kikwete katika hotuba ile.

Hata yale magazeti ambayo huitwa ya “udaku” (sijui kwanini) kama vile Uwazi yakajitosa. Katika toleo lake la tarehe 6 agosti, lilibeba kichwa cha habari “choko choko za Rwanda, Kagame kukiona”. Pia liliambatana na picha za vifaa mbali mbali vya kijeshi (bila shaka kuashiria nguvu ya kivita ya Tanzania). Je? Katika hotuba ya Mh. Raisi, alilenga ujumbe ufikishwe kwa mantiki hii? Ni kweli kwamba raisi alilenga kutoa onyo kwamba tuko tayari kwa vita na jirani zetu?

Makala nyingine iliyoandikwa katika gazeti la Mwananchi la tarehe 21 Agosti ilibeba kichwa kisemacho “Kagame kujenga nchi miaka, kuibomoa dakika”. Kwa juu juu, kichwa hiki cha habari hakina madhara yoyote, ila mpaka pale utapo ingia na kusoma undani wake. Moja ya aya ilisema;

“Chuki za Kagame dhidi ya kikwete zimeibuka pale Tanzania ilipoamua kupeleka majeshi yake DRC kwa mapendekezo ya UN kwa ajili ya kulinda amani katika kifungu cha saba, kinacho ruhusu kujibu mashambulizi pale askari wa kulinda amani wanapo shambuliwa.”

Sijui na sidhani kama muandishi wa makala husika hapo anao ushahidi wa kutosha juu ya hilo alilopenda kutuaminisha ya kwamba kisa cha uhusiano wa nchi hizi mbili kuharibika ni kutokana na sababu hiyo ya askari wa Tanzania kuingia nchini Congo .

Mwandishi wa makala hiyo pia anajitahidi kuihusisha serikali ya Rwanda na uwepo wa kikundi cha M23 kule Congo pale anaposema;

“…lakini uhusiano huu umeanza kuingia dosari pale Tanzania ilipoamua kuingilia mgogoro wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) pale ilipokitaka kikundi cha M23 kiondoke katika nchi hiyo ya Afrika ya kati.”

Huu ni uandishi unaotia doa taaluma ya uandishi wa habari maana hakuna vyanzo vyovyote vya habari vinavyo nukuliwa ili kuthibitisha madai haya. Na hata kama vyanzo vingenukuliwa, hadithi ilipaswa kufunika pande zote mbili (yaani ile ya wanaodai Rwanda inahusika na M23, na ile inayopinga).

Kwa upande mwingine, vyombo vya habari vya nchini Rwanda navyo havikuwa nyuma.

Mara baada ya kutoka kwa makala tajwa hapo juu ya gazeti la Mwananchi, gazeti la The New times la Rwanda la Tarehe 27 Agosti, liliandika hivi; “war mongers in Tanzania media: Rwanda supports peace, not war” na kwa tafsiri isiyo rasmi ni “wachochezi wa vita katika vyombo vya habari Tanzania: Rwanda inapenda amani na sio vita.” Andiko hili lilikuwa jibu la andiko la gazeti la Mwananchi nililojadili awali. Tofauti ni kwamba wakati mwandishi wetu akichochea mtafaruku, mwandishi wa Kinyarwanda ambaye ni Stephen Ruhanamilindi alitofautiana na hali hiyo.

Hata hivyo, gazeti hilo hilo la Tarehe 9 Agosti lilichapisha toleo lenye kichwa cha habari kisemacho “Govt reassures Tanzanians as Kikwete kicks out Rwandans”, likiwa na maana “serikali yawapa uhakika watanzania (waishio Rwanda) huku Kikwete akiwafukuza Wanyarwanda.” Tatizo la kichwa hiki cha habari, kinamfanya mtu aamini kwamba Raisi Kikwete kawafukuza Wanyarwanda kibaguzi ilhali si kweli. Katika hotuba yake niliyonukuu hapo awali, alipata kutoa agizo kwamba wale wote waliohamia nchini Tanzania isivyo halali, basi wahalalishe ukaazi wao au la warudi makwao. Kama wanyarwanda ambao tumewasikia wakilalamika baadae kuwa wamefukuzwa baada ya kuishi nchini miaka yote walikuwa na uhalali wa kuendelea kuishi, hapakuwa na ugumu wowote wa kuhalalisha ukaazi huo.

Gazeti la The News of Rwanda la tarehe 19 Agosti, nalo lilibebelea kichwa cha habari kilichosema Tanzania president Kikwete “married to Habyarimana Cousin”, kikimaanisha Raisi wa Tanzania Kikwete kamuoa binamu yake Habyarimana. Ndani yake kuna aya isemayo;

“New details obtained by News of Rwanda may give insight into why Tanzania’s president Jakaya Kikwete came out as the sole global leader symphatheic to Rwandan FDLR rebels based in DR Congo jungles since 1994.

According to secret US State Departement cables published by whistle blowing site Wikileaks, President Kikwete’s wife fondly known in Tanzania as Mama Salma Kikwete is a cousin of former Rwandan Leader Habyarimana.”

Tafsiri yake ni kwamba “Taarifa mpya zilizoifikia News of Rwanda (gazeti) zinaweza kutoa mwangaza wa kwanini raisi wa Tanzania amekuwa mtu pekee kuwahi kuwatetea waasi wa Kinyarwanda, FDLR walioko nchini Congo tangu 1994. Kwa mujibu wa taarifa za siri kutoka wizara za marekani zilizovujishwa na mtandao wa wikileaks zimeeleza kuwa mke wa raisi wa Tanzania maarufu kama Mama Salma ni binamu yake kiongozi wa zamani wa Rwanda.”

Juvenal Habyarimana alikuwa ni Raisi wa Rwanda mwenye asili ya ki Hutu aliyeuawa mwaka 1994 kwa ndege aliyokuwa akisafiria kulipuliwa, jambo lililochochea vita vya kimbali baina ya wa Tutsi na wa Hutu.

Kuna mambo kadha wa kadha ya kushangaza juu ya aya hizo kutoka kwa mwandishi huyo aitwaye Gahiji. Mosi, kuna tatizo gani la Mama Kikwete kuwa binamu yake Habyarimana. Kama kweli Wanyarwanda ni watu waliosameheana (reconciled kama wasemyavyo) kutokana na tofauti zao za kikabila zilipopelekea takriban watu 800,000 zaidi zaidi wa asili ya kitusi kuuawa na wahutu, iweje kuwa ndugu wa mhutu marehemu Habyarimana liwe jambo la kushitua sana?

Pili, kulikuwa kuna utetezi gani wa wahutu (FDLR) kutokana na tamko la Raisi kikwete la kuwataka wakae faragha na kurejesha amani ya mashariki ya kati?

Tatu, je? Kulikuwa na uhitaji gani wa kuanza kufukua historia ya mke wa Raisi ambaye kwa mujibu wa Wanyarwanda, amewaghafirisha sana? Huu sio uchochezi? Kwenye matatizo baina ya pande mbili, ni busara kuzidi fukua matatizo au kutafuta suluhu ili kuleta hali ya amani?

Nikihitimisha uandishi wa andiko hili, ningependa kuweka bayana kwamba baadhi ya vyombo vya habari vya nchi hizi mbili (Rwanda na Tanzania) havijatenda kwa kutumia busara na weledi ili kuzuia hali mbaya kuwa mbaya zaidi. Ni vyombo hivi ndivyo vimekuwa na mchango mkubwa katika kuwaaminisha Wanyarwanda na Watanzania kwamba kuna tatizo kubwa ilhali hakuna tatizo au kama lipo basi ni dogo na kwamba taarifa za kusawazisha hali ya taharuki na sintofahamu ndizo zingepewa kipaumbele. Badala yake, sijui ni kwa uchu wa kufanya biashara, au kuchochea uhasama, vyombo hivyo vimekuwa vikichochea moto kwenye tofauti iliyojitokeza.

Wakati suala hili linatarajiwa kumalizika kidiplomasia siku za usoni, nitoe rai kwamba vyombo vya habari vina nguvu kubwa sana ya kujenga na kuharibu/kubomoa kwa maana ya kuweza kuuaminisha umma kuwa nyeupe ni nyeusi na nyeusi ni nyeupe wakati sivyo na matokeo yake kupelekea kuwepo kwa jamii iliyogubikwa na uvunjifu wa amani na manung’uniko. Hivyo basi, penye fursa ya kurejesha amani kwenye mgogoro, media zitumike kufanya hivyo na siyo kuchochea tofauti kupitia machapisho.
 
:doh:Hivi kama Marekani wangekuwa wanaongozwa na pressure ya vyombo vya habari si wangepigana na kila nchi?
 
Taarifa iliyopo ni kwamba mnamo tarehe 21 Mei 2013 wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Umoja wa Afrika (AU) Addis Ababa nchini Ethiopia, ulipofika wasaa wa Mh. Rais Jakaya M. Kikwete kusema aliyokuwa nayo, alitumia fursa hiyo kuishauri serikali ya Rwanda ikiongozwa na Raisi Paul Kagame juu ya hali ya amani nchini Congo. Alimsihi ya kwamba ili hali ya amani irejee, hana budi kufanya mazungumzo na kundi la FDLR, waasi wa Kinyarwanda walioko Congo.

Ushauri huu ulikuwa kama cheche kwenye kichaka maana kilichofuata hapo ni kama ambavyo tumeshuhudia serikali ya Rwanda ikionyesha kugadhabishwa kwa hali ya juu kutokana na ushauri huo.

Kabla sijarejea kwenye mada kuu iliyonifanya niandike, ningependa kuchambua ushauri huu kimtizamo binafsi na kwa kutuma utashi (common sense) ambao kila mwanadamu amejaliwa. Mtu anapokushauri jambo, na zaidi zaidi awe ni mshirika wako (katika hali hii wahusika ni maraisi wa nchi jirani), unaweza kuuchukua ushauri huo na kumshukuru, pengine hata kumdadisi juu ya namna ya kuufanyia kazi kwa maono na maoni yake. Pili, kama ni ushauri usioshabihiana na mtizamo wako au utashi wako juu ya mambo, utaukataa. Ni jambo la nadra sana kukuta mtu anakataa ushauri kwa ukali na lugha ngumu kama aliyotumia Mh. Kagame labda awe na ukosefu wa staha (kitu ambacho siamini raisi wa Rwanda kapungukiwa kwacho). Hivyo basi inanifanya niamini kukaripiana huku ni hatua ya mwisho kabisa ya tatizo ikiashiria kuwa kumekuwa na misuguano ya chini kwa chini ambayo kwa namna moja au nyingine haikufika kwenye vyombo vya habari. Hata hivyo, naepuka kujihusisha na utabiri (speculations).

Nini basi alichokisema Raisi Paul Kagame? Alipokuwa akihutubia wahitimu wa mafunzo ya kijeshi katika chuo kilichopo Musanze, mnamo tarehe 10, Juni 2013, (nitanukuu na kutafsiri yale muhimu kwa mujibu wa video ipatikanayo mtandaoni (youtube) iitwayo (President Kagame on Kikwete's statement) alisema

"…nilisikia kuna baadhi ya watu walikuwa na mambo ya kusema kuhusu Rwanda kufanya mazungumzo, kujadiliana na wauaji wa watu wetu…watu wanaizungumzia FDLR kirahisi rahisi hivyo…na wanajua wanazungumzia makaburi haya ya watu wetu, na kwamba wale waliofanya hivi (waliofanya kitendo cha mauaji)…tuna deni kwao. Hata hivyo, awali sikusema kitu juu ya hili, kutokana na mosi, kuchukizwa nalo, pili nilifikiri ni upuuzi mtupu, tatu, labda ilitokana na umbumbumbu, nne…kama ni tatizo la kimlengo, (na nadhani ndio tatizo kuu) basi tatizo hilo ni bora likabaki na wenye nalo…lakini tutapata siku nyingine ya kulikabili hilo (tatizo)…"

Ikafuata hotuba ya Mh. Raisi Kikwete mwishoni mwa mwezi Julai ambayo ilisheheni mambo kadha wa kadha likiwemo la uhusiano baina ya Rwanda na Tanzania. Nitanukuu yale machache nyenye manufaa katika andiko langu hili;

"…napenda kuwahakikishia watanzania wenzangu na ndugu zangu wa Rwanda kuwa mimi na serikali ninayoiongoza tunapenda kuwa na ushirikiano mzuri…mimi na serikali ninayoiongoza tutakuwa wa mwisho kufanya vitendo vibaya dhidi ya serikali ya Rwanda au nchi yoyote jirani au nchi yoyote duniani…napenda kuwahakikishia ndugu zetu wa Rwanda kuwa kwa upande wetu hakuna kilicho badilika wala kilicho pungua katika uhusiano na ushirikiano..

…kwa upande wangu binafsi, sijasema lolote kuhusu Rwanda, pamoja na maneno mengi kutoka Rwanda na viongozi wake, pamoja na maneno mengi ya matusi na kejeli kutoka kwenye vinywa vya viongozi wa Rwanda dhidi yangu…sio kwamba sisikii, wala si kwamba siambiwi yanayosemwa au sijui kusema, au sina la kusema, la hasha! Sijafanya hivyo kwasababu sioni faida yake…"

Kwa mtizamo wa karibu wa hotuba hizi mbili; yaani ile ya Mh. Kagame na ile ya Mh. Kikwete zina ujumbe (tone) tofauti. Wakati ile ya awali ikionekana kutoka kwa mtu mwenye gadhabu, ya mwisho inaonekana ikitaka kusawazisha hali (atmosphere) ilo tengenezwa na ile hotuba ya mwanzo.

Shida inakuja pale vyombo vya habari vinapozinasa hotuba hizi mbili na kuamua kuleta muktadha viutakavyo vyenyewe sijui kwa manufaa ya nani.

Gazeti la Mwananchi, Agosti 3 lilibeba kichwa cha habari kisemacho "Kikwete amvaa Kagame, amshangaa kwa lugha za matusi na kejeli." Jambo la kujiuliza hapa ni je? kulikuwa na "kuvaana" kupi katika hotuba ya Mh. Raisi, kama sio kutia chumvi kwenye kidonda? Muandishi wa makala husika alimnukuu raisi Kagame kwa kusema,

"…nilinyamaza kimya kwasababu sikupenda kusikiliza ushauri kuhusu FDLR, kwa sababu nafikiri ni upuuzi ulioambatana na ujinga. Hatuwezi kuacha maisha yetu kama Wanyarwanda tunavyoishi sasa. Ushauri wa kikwete ni sawa na kucheza na makaburi ya watu wengi ambao ni ndugu zetu"

Kwa mtu makini ni rahisi kugundua kuwa nukuu hii imeongezwa chumvi hasa ikizingatiwa kwamba Rais Kagame hakumtaja Raisi Kikwete katika hotuba ile.

Hata yale magazeti ambayo huitwa ya "udaku" (sijui kwanini) kama vile Uwazi yakajitosa. Katika toleo lake la tarehe 6 agosti, lilibeba kichwa cha habari "choko choko za Rwanda, Kagame kukiona". Pia liliambatana na picha za vifaa mbali mbali vya kijeshi (bila shaka kuashiria nguvu ya kivita ya Tanzania). Je? Katika hotuba ya Mh. Raisi, alilenga ujumbe ufikishwe kwa mantiki hii? Ni kweli kwamba raisi alilenga kutoa onyo kwamba tuko tayari kwa vita na jirani zetu?

Makala nyingine iliyoandikwa katika gazeti la Mwananchi la tarehe 21 Agosti ilibeba kichwa kisemacho "Kagame kujenga nchi miaka, kuibomoa dakika". Kwa juu juu, kichwa hiki cha habari hakina madhara yoyote, ila mpaka pale utapo ingia na kusoma undani wake. Moja ya aya ilisema;

"Chuki za Kagame dhidi ya kikwete zimeibuka pale Tanzania ilipoamua kupeleka majeshi yake DRC kwa mapendekezo ya UN kwa ajili ya kulinda amani katika kifungu cha saba, kinacho ruhusu kujibu mashambulizi pale askari wa kulinda amani wanapo shambuliwa."

Sijui na sidhani kama muandishi wa makala husika hapo anao ushahidi wa kutosha juu ya hilo alilopenda kutuaminisha ya kwamba kisa cha uhusiano wa nchi hizi mbili kuharibika ni kutokana na sababu hiyo ya askari wa Tanzania kuingia nchini Congo .

Mwandishi wa makala hiyo pia anajitahidi kuihusisha serikali ya Rwanda na uwepo wa kikundi cha M23 kule Congo pale anaposema;

"…lakini uhusiano huu umeanza kuingia dosari pale Tanzania ilipoamua kuingilia mgogoro wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) pale ilipokitaka kikundi cha M23 kiondoke katika nchi hiyo ya Afrika ya kati."

Huu ni uandishi unaotia doa taaluma ya uandishi wa habari maana hakuna vyanzo vyovyote vya habari vinavyo nukuliwa ili kuthibitisha madai haya. Na hata kama vyanzo vingenukuliwa, hadithi ilipaswa kufunika pande zote mbili (yaani ile ya wanaodai Rwanda inahusika na M23, na ile inayopinga).

Kwa upande mwingine, vyombo vya habari vya nchini Rwanda navyo havikuwa nyuma.

Mara baada ya kutoka kwa makala tajwa hapo juu ya gazeti la Mwananchi, gazeti la The New times la Rwanda la Tarehe 27 Agosti, liliandika hivi; "war mongers in Tanzania media: Rwanda supports peace, not war" na kwa tafsiri isiyo rasmi ni "wachochezi wa vita katika vyombo vya habari Tanzania: Rwanda inapenda amani na sio vita." Andiko hili lilikuwa jibu la andiko la gazeti la Mwananchi nililojadili awali. Tofauti ni kwamba wakati mwandishi wetu akichochea mtafaruku, mwandishi wa Kinyarwanda ambaye ni Stephen Ruhanamilindi alitofautiana na hali hiyo.

Hata hivyo, gazeti hilo hilo la Tarehe 9 Agosti lilichapisha toleo lenye kichwa cha habari kisemacho "Govt reassures Tanzanians as Kikwete kicks out Rwandans", likiwa na maana "serikali yawapa uhakika watanzania (waishio Rwanda) huku Kikwete akiwafukuza Wanyarwanda." Tatizo la kichwa hiki cha habari, kinamfanya mtu aamini kwamba Raisi Kikwete kawafukuza Wanyarwanda kibaguzi ilhali si kweli. Katika hotuba yake niliyonukuu hapo awali, alipata kutoa agizo kwamba wale wote waliohamia nchini Tanzania isivyo halali, basi wahalalishe ukaazi wao au la warudi makwao. Kama wanyarwanda ambao tumewasikia wakilalamika baadae kuwa wamefukuzwa baada ya kuishi nchini miaka yote walikuwa na uhalali wa kuendelea kuishi, hapakuwa na ugumu wowote wa kuhalalisha ukaazi huo.

Gazeti la The News of Rwanda la tarehe 19 Agosti, nalo lilibebelea kichwa cha habari kilichosema Tanzania president Kikwete "married to Habyarimana Cousin", kikimaanisha Raisi wa Tanzania Kikwete kamuoa binamu yake Habyarimana. Ndani yake kuna aya isemayo;

"New details obtained by News of Rwanda may give insight into why Tanzania's president Jakaya Kikwete came out as the sole global leader symphatheic to Rwandan FDLR rebels based in DR Congo jungles since 1994.

According to secret US State Departement cables published by whistle blowing site Wikileaks, President Kikwete's wife fondly known in Tanzania as Mama Salma Kikwete is a cousin of former Rwandan Leader Habyarimana."

Tafsiri yake ni kwamba "Taarifa mpya zilizoifikia News of Rwanda (gazeti) zinaweza kutoa mwangaza wa kwanini raisi wa Tanzania amekuwa mtu pekee kuwahi kuwatetea waasi wa Kinyarwanda, FDLR walioko nchini Congo tangu 1994. Kwa mujibu wa taarifa za siri kutoka wizara za marekani zilizovujishwa na mtandao wa wikileaks zimeeleza kuwa mke wa raisi wa Tanzania maarufu kama Mama Salma ni binamu yake kiongozi wa zamani wa Rwanda."

Juvenal Habyarimana alikuwa ni Raisi wa Rwanda mwenye asili ya ki Hutu aliyeuawa mwaka 1994 kwa ndege aliyokuwa akisafiria kulipuliwa, jambo lililochochea vita vya kimbali baina ya wa Tutsi na wa Hutu.

Kuna mambo kadha wa kadha ya kushangaza juu ya aya hizo kutoka kwa mwandishi huyo aitwaye Gahiji. Mosi, kuna tatizo gani la Mama Kikwete kuwa binamu yake Habyarimana. Kama kweli Wanyarwanda ni watu waliosameheana (reconciled kama wasemyavyo) kutokana na tofauti zao za kikabila zilipopelekea takriban watu 800,000 zaidi zaidi wa asili ya kitusi kuuawa na wahutu, iweje kuwa ndugu wa mhutu marehemu Habyarimana liwe jambo la kushitua sana?

Pili, kulikuwa kuna utetezi gani wa wahutu (FDLR) kutokana na tamko la Raisi kikwete la kuwataka wakae faragha na kurejesha amani ya mashariki ya kati?

Tatu, je? Kulikuwa na uhitaji gani wa kuanza kufukua historia ya mke wa Raisi ambaye kwa mujibu wa Wanyarwanda, amewaghafirisha sana? Huu sio uchochezi? Kwenye matatizo baina ya pande mbili, ni busara kuzidi fukua matatizo au kutafuta suluhu ili kuleta hali ya amani?

Nikihitimisha uandishi wa andiko hili, ningependa kuweka bayana kwamba baadhi ya vyombo vya habari vya nchi hizi mbili (Rwanda na Tanzania) havijatenda kwa kutumia busara na weledi ili kuzuia hali mbaya kuwa mbaya zaidi. Ni vyombo hivi ndivyo vimekuwa na mchango mkubwa katika kuwaaminisha Wanyarwanda na Watanzania kwamba kuna tatizo kubwa ilhali hakuna tatizo au kama lipo basi ni dogo na kwamba taarifa za kusawazisha hali ya taharuki na sintofahamu ndizo zingepewa kipaumbele. Badala yake, sijui ni kwa uchu wa kufanya biashara, au kuchochea uhasama, vyombo hivyo vimekuwa vikichochea moto kwenye tofauti iliyojitokeza.

Wakati suala hili linatarajiwa kumalizika kidiplomasia siku za usoni, nitoe rai kwamba vyombo vya habari vina nguvu kubwa sana ya kujenga na kuharibu/kubomoa kwa maana ya kuweza kuuaminisha umma kuwa nyeupe ni nyeusi na nyeusi ni nyeupe wakati sivyo na matokeo yake kupelekea kuwepo kwa jamii iliyogubikwa na uvunjifu wa amani na manung'uniko. Hivyo basi, penye fursa ya kurejesha amani kwenye mgogoro, media zitumike kufanya hivyo na siyo kuchochea tofauti kupitia machapisho.

Binafsi nimekuja kugundua kumbe JK na Kagame siyo maadui, bali maadui wa hawa MA-rais hasa wanasiasa ndiyo wamekuwa mstari wa mbele kutaka kuiaminisha dunia kuwa Tanzania na RWANDA ni maadui. sijui huko Rwannda, hapa Tanzania MAgazeti kama Tanzania Daima, MAWIO , mitandao ya kijamii kama Jf ambayo humilikiwa na wanasiasa walitaka kuwaaminisha watanzania kuwa JK alikosea kumshauri KAGAME. hata kauli ya Dr. SLAA na maswali ya Kiongozi wa Kambi ya UPinzani aliyomuuliza WAZIRI MKUU ni ushahidi tosha kuwa walikuwa nyuma ya vyombo vya habari ambavyo vilkuwa msatari wa mbele kutaka kuwaaminisha WAtanzania kuwa kuna mgogoro. JK na KAGAME wamezima kabisa ndogo za wapinzani wao za kutaka kujizolea umaarufu wa kisiasa pale waliposhikana mikono mapema wiki iliyopita huko KAMPLA UGANDA.

hakika hii ni aibu kwao.
 
Huu uzi umeshafika hapa na watu wasiopungua mia moja nawewe bado unauleta ulikuwepo kwenye cave au ulikuwa unamaliza kifungo chako pale keko
 
:doh:Hivi kama Marekani wangekuwa wanaongozwa na pressure ya vyombo vya habari si wangepigana na kila nchi?
Ni kweli kabisa, hata Jakaya KIKWETE angekuwa anawasikiliza wanasiasa na media zao hakika watu wengine wangeshakimbia nchi. RAis atakumbukwa kwa uvumilivu na Staha zake , hakika ana sifa zote za kuwa kiongozi.
 
Kweli kabisa!! Alifurahishwa na kifo cha Mwagosi na kumpandisha cheo Kamuhanda bila kujali kelele za vyombo vya habari!!!
 
Back
Top Bottom