Nafasi ya Polepole yajazwa, Luteni Jenerali Mathew Edward Mkingule apangiwa kuwa Balozi nchini Cuba

Nafasi ya Polepole yajazwa, Luteni Jenerali Mathew Edward Mkingule apangiwa kuwa Balozi nchini Cuba

Precious Diamond

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2023
Posts
710
Reaction score
1,610
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya uhamisho na kuwapangia vituo mabalozi. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, mabalozi waliopangiwa vituo ni kama ifuatavyo:-

(i) Balozi Togolani Edriss Mavura amepangiwa kuwa Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, New York;

(ii) Balozi Mhandisi Cyprian John Luhemeja amepangiwa kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Zambia;

(iii) Balozi Salim Othman Hamad amepangiwa kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Comoro;

(iv) Balozi Maulidah Bwanakheri Hassan amepangiwa kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Oman;

(v) Balozi Dkt. Suleiman Haji Suleiman amepangiwa kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini China;

(vi) Balozi Luteni Jenerali Mathew Edward Mkingule amepangiwa kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Cuba;

Screenshot_20260302_194926_Samsung Notes.jpg
Screenshot_20260302_195246_Samsung Notes.jpg
 
Wameogopa nini kusema Marehemu Polepole??

Siku yao inakuja watasema tu.
 
Kwa slowslow nadhani serikali ilishafunga mjadala nae toka rais alipomvua hadhi ya ubalozi
Hakuna mjadala uliofungwa , wamesogeza muda wa kufungua pandora box , hiyo siku inakuja kuna kuna watu watatafutana.
 
Baada ya kumteka na kumtesa kijana wa watu wameamua kureplace nafasi yake leo hii?, alipojiondoa mwenyewe walikuwa wapi kujaza ile nafasi haraka?.

Anyway huu utawala ujifunze matumizi sahihi ya vyombo vya ulinzi, wenzetu huko duniani wanavitumia kupambana na maadui wa nje, huku shithole countries viongozi wahuni wanavitumia kuwakandamiza raia wao, kuwatishia, kuwateka na kuwaumiza, inabidi tupate adui sirias kutoka nje aje atufundishe matumizi sahihi ya vyombo ya kiulinzi, tubondekee akili ikae sawa.
 
Back
Top Bottom