Ave Ave Maria
JF-Expert Member
- Apr 22, 2011
- 10,707
- 5,682
Hiyo ya kugeuza watoto vijakazi haijakaa sawa. Sema ndio hivyo kukaa kwa mtu kazi, inabidi ufanye tu.
kweli aisee, maisha yanataka ukishaoa uachane na utaratibu wako wa zamani hasa usiompendeza mkeo, kama marafiki, ndugu, jamaa wote hawatakiwi kukufata fata wala wewe kuwafata fata. Unatakiwa kuchukulia ulimwenguni kama mmebaki nyie wawili tu. Eti eeh?
Huyo sasa kazidi, au alidhani kukaa kwa wakwe ni sawa na kukaa hotelini?Inaweza kuwa ni kazi ndogo......fine, lakini it is not a guarantee kuwa yeye asifanye kwa sababu kuna watoto! Ebu fikiria, umeamka saa 5 umekuta mama mkwe kapika chai unakunywa! Badala ujifulie basi na wewe vijiguo vyako, ila unaloweka then huyoo unakula misele unasubiria flani aje akufulie.......kumbuka hapo hujihusishi na kazi nyingine ile!! Ukikuta nguo hazijafuliwa unaanza kulalamika na kusingizia kuwa ni flani alimkataza kumbe walaa ukute hata dogo hakuwepo au alichelewa kurudi!! Basi we unachukulia hasira tu, ukimsingizia kakondoo wala hana shida kabisa nakuelewesha tu lawama zikizidi sana nakuacha tu au namwambia mumeo atajua mwenyewe lakufanya!!
Mara nyingi huwa ni hulka tu maana unakuta wengine pamoja na kuwa na kazi zao nzuri na kuwa na maisha yao binafsi bado tu ataanza kumuandama mke wa kaka yake mara hivi mara vile mimi nafikiri hakuna sababu ya msingi sana zaidi ya kuwa ni hulka waliyonayo baadhi ya wanawake kuona kuwa kaka zao hawawezi kutunzwa vizuri na mwanamke mwingine ili hali uamuzi wa kuoa aliyeuchukua ni mwanaume na mwanaume akiendekeza hiki kitu ndio hapo mfarakano kwenye ndoa unaanza na mwanamke naye akiwa legelege ndio kabisa atapelekeshwa puta mpaka basi.
Maana hawa mawifi wakigundua weakness ya kaka yao ni wapi ndio hapo hapo wanapo hit na kumfanya mwanamke aliyeolewa kuonekana anashindwa kumudu ndoa yake kitu ambacho kinawapa nafasi mawifi kuonekana wao ndio wao binafsi kwangu mimi ndoa ni baina ya mwanamke na mwanaume ukiishaanza kuwa-entertain mawifi it will cost you big time..
Kuachana na utaratibu sio ishu, kubadili ndio ishu..
Hapo nimekusoma kakondoo, inabidi kaka yako sasa ndio amwambie mke wake asimfanye mtoto mfanyakazi wake.
ukitaka kujua wanawake ni viumbe vya ajabu ni hapo kwenye ugomvi wa mke na mawifi....
kila ambacho watapinga unachomfanyia mkeo ndio wao wataenda kukidai kwa waume zao....
hivi viumbe hivi lol
kubadili aje hapo? Kama ulikuwa unaenda club kila siku (refer mfano wako) kwahiyo kubadili utaratibu awe anaenda mara moja moja au? Kama mkewe hapendi hata hiyo mara moja afanyeje? Kama mwanaume alikuwa anawashirikisha ndugu kwenye maamuzi, kwenye kubadilika unamaanisha asiwashirikishe tena akishao au awashirikishe nusu nusu. Kama asipowashirikisha hapo utasema amebadili utaratibu au ameacha?
Huyo sasa kazidi, au alidhani kukaa kwa wakwe ni sawa na kukaa hotelini?
Uko sawa BAK. Lakini uki-entertain maneno yanaendelea kuja. Kuna wake pia nao wana tabia ya kuwafuatilia wifi zao, kama kakako kakupa sh ngapi etc. Mi nadhani ni malezi na life style, usipoendekeza hayakupati. 'usilete ufundi kwa mwenzio, ngoja upate nafasi uwe na kwako tuje tukuone', period! Usi-comment any observation ya kwa ndugu,kaka wala rafiki!
huu uzi uko poa sana, ngoja nikalale ntarudi tena kesho.. G9t peoples
"....damu nzito kuliko,....!" uchungu wa mwana...
..acheni madada waendelee kuwatetea kaka zao bana,
wake wengine ni wanyanyasaji banaa...hahaha..
...Mkuu Mbu uyasemayo ni kweli lakini madada wengine hata wakilambwa miguu na wake za kaka zao hawaridhiki hata kidogo!!! lazima tu wahakikishe wanaanzisha sokomoko ili kuondoa furaha ndani ya nyumba. Kaka yao ni mtu mzima ana uwezo wa kuchanganua baya na zuri kama haoni shida kwa mkewe kuamka saa tano, nguo zao kufuliwa na HG, vyakula vyao vyote kuanzia asubuhi hadi jioni kupikwa na HG kuna tatizo gani la kumfanya dada wa kaka akose raha na kutaka kuingilia maisha ambayo hayamuhusu!!!!?
Yaani BAK,I wish ungekuwa tu karibu....lol... sina hata la kuongeza kwenye hii mada,umezungumza yote!! Midada mingine inawafanya kaka zao kama wenyewe hawana uwezo wa kupima wanayotendewa,kila kitu wao lazima waweke pua zao na hata umtunzeje ndugu yao wao wanafikiri wangeweza kufanya zaidi ya mke...inatesa sana!
...Mkuu Mbu uyasemayo ni kweli lakini madada wengine hata wakilambwa miguu na wake za kaka zao hawaridhiki hata kidogo!!! lazima tu wahakikishe wanaanzisha sokomoko ili kuondoa furaha ndani ya nyumba. Kaka yao ni mtu mzima ana uwezo wa kuchanganua baya na zuri kama haoni shida kwa mkewe kuamka saa tano, nguo zao kufuliwa na HG, vyakula vyao vyote kuanzia asubuhi hadi jioni kupikwa na HG kuna tatizo gani la kumfanya dada wa kaka akose raha na kutaka kuingilia maisha ambayo hayamuhusu!!!!?
Eti anachekelea. . ..
Ngoja nimsaidie dearest kumalizia. . . angekufinya ili ahakikishe haoti kwamba kuna wanaume wenye mawazo kama yako.Lolz
mimi kama kaka yako Husninyo nakujibu
mke wangu lazima 'ajimwage mwage nyumbani' kwake kama wewe unaona dharau tafuta nyumba yako...
na kama unaishi nyumbani kwangu ambako mke wangu ndie malkia wa nyumba
lazima habari zako zote azijue,usije kupewa mimba ukashindwa kusoma nikapoteza pesa nazotumia kukusomesha...
misiba na wagonjwa hawezi kwenda bila mimi kumruhusu....so sio kosa lake
na sio kila msiba unakwenda.....utaenda misiba mingapi mjini hapa....?.
ni lazima ajioneshe ili awaoneshe wale waliosema 'ningeshindwa kumtunza na kumpa furaha' how wrong walikosea
so muache aringe na kujionesha ni haki yake
na kuhusu nyinyi dada zangu kuja nyumbani..
hiyo ndo chanzo cha umbea na majungu....mimi mwenyewe sitaki...
mkiwa na shida mnifuate oficin....mke wangu ana haki ya kulala mmchana na kutazama tamthilia bila bughudha
na nyinyi mna haki hizo majumbani mwenu sawa????
so now umenisikia.......i hope utanielewa...