Nafanya kama sijali ila moyoni naumia!

Nafanya kama sijali ila moyoni naumia!

vunja ukimya, sema nae.

Imeletwa kwenu kwa hisani ya watu wa obama
 
Jamani naombeni msaada, hivi mtu kama huyu nyie mnamchukuliaje? tulikuwa ndo tumeanza tu kuongea kwa njia ya simu mimi na mpenzi wangu ambae nkonae mbali, hata dakika tano hazikuisha akanambia "kata simu kuna mtu anapiga" hapo akatumia zaidi ya lisaa kuongea anadai ni kaka yake,mi nkaamua kumpotezea, kiukweli ameniboa na nimeamua kuzima simu kabisa au nimekosea?

Anaongea na kaka usiku wa manane tena lisaa? Mkuu, ukiona hivyo ujue kishakimbizwa, kakamatwa, anaenda kuliwa.....
 
Jamani naombeni msaada, hivi mtu kama huyu nyie mnamchukuliaje? tulikuwa ndo tumeanza tu kuongea kwa njia ya simu mimi na mpenzi wangu ambae nkonae mbali, hata dakika tano hazikuisha akanambia "kata simu kuna mtu anapiga" hapo akatumia zaidi ya lisaa kuongea anadai ni kaka yake,mi nkaamua kumpotezea, kiukweli ameniboa na nimeamua kuzima simu kabisa au nimekosea?

khaa! Dalili ya mvua mawingu eti...! No! no! no! Mawingu mengine hayaleti mvua bali huleta dhoruba ya upepo, mmmn!!!! Sometimes huleta radi!!!
Ah! Ah! Ah! Nimekumbuka hilo wingu liwe kubwa ndio maradi, upepo wa dhoruba na mafuriko hutokea! Inasikitisha mawingu hayo sometimes hututisha, tukaacha kwenda safari zetu za msingi, lol kumbe hata iyo mvua hainyeshi! NAJUTA! Bora ningelikwenda, hata ingenikuta njiani si ningeloa tu! Kuloa kwani kufa? Nimekumbuka tena 'eti kosa si kosa bali kosa kurudia kosa' khaa! Sijui wazee wanakusudia nini wakisema 'kosa la mwanzo haliachi mke!'
mh! Mi simo...
 
Pole sana kwa hilo, ila ni lazima uelewe kuwa yapo mengi tuu ambayo binaadamu tumeumbiwa na mwenyezi mungu ila sometime tunapotezea siku zisonge tuu ingawa moyoni inaumiza sana.
 
Kaka kuwa na amani tu, usiweke mtazamo hasi mbele, huenda ni kaka yake kweli na labda walikuwa na ishu ya kifamilia na km tujuavyo, usiku ni muda mzuri kuongea kirefu, ukizingatia gharama ni ndogo na pia unakuwa free kwa maana ya kwamba huna shughuli ukilinganisha na mchana. Pia hukufanya vizuri kuzima simu na kwa kias flani ulimkwaza. Ungezungumza nae kwa upendo na ungemwambia awe anakuambia mapema vitu km hivyo. Mi sijaona km kuna harufu ya usaliti hapo ndugu
 
Ndugu yangu mimi na wewe ni sare sare maua! mimi mwenywe yamenikuta sana hayo, ila mimi za mbayuwayu nimechanganya na zangu!!!!!!!!
 
Jamani naombeni msaada, hivi mtu kama huyu nyie mnamchukuliaje? tulikuwa ndo tumeanza tu kuongea kwa njia ya simu mimi na mpenzi wangu ambae nkonae mbali, hata dakika tano hazikuisha akanambia "kata simu kuna mtu anapiga" hapo akatumia zaidi ya lisaa kuongea anadai ni kaka yake,mi nkaamua kumpotezea, kiukweli ameniboa na nimeamua kuzima simu kabisa au nimekosea?

wakati wa mahusiano kabla ya ndoa(uchumba.....whatsoever)huwa sio wakati wa kusomana tabia bali HUWA NI WAKATI MAALUM WA KUJIFUNZA NAMNA YA KUYAVUMILIA MAPUNGUFU YA MWENZAKO(mtarajiwa wako).so nilazima uwe na uvumilivu wa kutosha pia kile ambacho hukipendi ni lazima umweleze mwenzako kuwa hukipendi na yeye lazima atambue kwa kukifanya hicho ambacho hukipendi anakuudhi.kuzima cm siyo solution
 
Mwenzenu nilikua nalia usiku mzima kisa mwanamke....usiombe hayo makitu yakukute bhana
 
dah! ukiona manyoya ,ujue.............. kitafute kijiji cha songambele tu...............
 
Umekimbia tatizo na haujatenda haki kufanya hvy inawezekana ni kaka yake kweli ila wewe ukawa unakichukia kivuli chako mwenyewe. Muulize kisha chunguza kwa makini na kama huyo mtu anampigia mara kwa mara hapo kutakua na jambo na si kaka yake.
 
mwizi huyo achana nae!!!!!!!!!!!!!!!!
Jamani naombeni msaada, hivi mtu kama huyu nyie mnamchukuliaje? tulikuwa ndo tumeanza tu kuongea kwa njia ya simu mimi na mpenzi wangu ambae nkonae mbali, hata dakika tano hazikuisha akanambia "kata simu kuna mtu anapiga" hapo akatumia zaidi ya lisaa kuongea anadai ni kaka yake,mi nkaamua kumpotezea, kiukweli ameniboa na nimeamua kuzima simu kabisa au nimekosea?
 
Hamna Kitu Hapo??haiitaj Elimu Ya UDSM,kubain kuwa penz limechuja,!! piga chini tafta wa kutuliza maumiv na www!! ila km umependa sana,utakufa na presha,maaana mapenz ya mbali balaa,mwenzio nlikuwaga nakesha kuongea nae na cm mpk saa saba ucku,
 
msg yako?? ilikuwa na rangi gani? hiyo nimeandika mwenyewe,and I don want those stresses any more!! Km ni yako au c yako to hell?? utajua mwenyewe.
 
Asanteni sana brothers and sisters kwa ushauri, kitu nlichogundua ni kwamba the guy ni pasua kichwa! So nimeamua ku move-on na maisha yangu....love u all and be blessed.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom