Nafaka zimepanda mara dufu

Nafaka zimepanda mara dufu

amanindoyella

Senior Member
Joined
Oct 13, 2009
Posts
104
Reaction score
9
Jamani juzi nilikwenda mwananyamala sokoni ili nijipatie mahitaji kidogo kwa ajili ya nyumbani. Amini usiamini nilishindwa kununua kwani mchele kilo moja ni 2,400/= mpaka 3,000/= kwa kweli ilinichukua dakika 15 kufikiria ninunue au la mwisho niliondoka mikono mitupu!
Hapa kinachonishangaza ni kwanini nafaka ipande kwa kiasi kikubwa wakati ni kipindi cha mavuno? Nini kinaendelea nchini kwetu?
Unga nao bei juu! Sasa sisi wanyonge tukimbilie wapi? Nimesikia soko la kisutu mchele mzuri kilo ni 3,500/=
Kinachonikera zaidi ni kuwa Tanzania tunalima chakula cha kila aina hadi tunatoa misaada nchi za nje.
Kwanini chakula kinapanda bei?
 
Back
Top Bottom