Dr Akili
JF-Expert Member
- Aug 21, 2011
- 4,953
- 4,326
Tunaambiwa kuwa mfumuko wa bei (inflation rate) nchini kwetu bado ni mdogo sana, ni chini ya asilimia 5%! Wao wanauita single digit inflation.
Lakini kwa miezi ya hivi karibuni, bei za vyakula muhimu sokoni vimepanda kwa zaidi ya maradufu. Yaani mfumuko wa bei wa vyakula ni zaidi ya asilimia 50%, yaani ni double digit inflation! Vyakula hivi ni pamoja na vile wanavyotumia watu wa kawaida, walala hoi na waamka hoi. Kwa mfano Unga wa mahindi ni sasa hivi ni Sh 2,000 kwa kilo moja kutoka Sh 1,000 kwa kilo mwezi Julai 2022. Mchele (grade A) umepanda kutoka Sh 1,200 kwa kilo hadi Sh 3,500 - 4,000. Maharage kutoka Sh 1,800 hadi Sh 3,000. Karanga kutoka Sh 2,000 hadi Sh 5,000 na kadhalika.
Hili ni janga la kitaifa kwani hadi kufika msimu ujao wa mavuno, hatujui hali itakuwa vipi. Sasa hivi mwananchi wa uchumi wa kawaida, ni vigumu kula zaidi ya mlo mmoja kwa siku. Hizo kampeni za lishe bora ili kuepusha vijana wetu wa kiume kutegemea nguvu za supu ya pweza, hazitaweza kufanikiwa kwa mazingira kama haya.
Ili kupata ufumbuzi wake tunapaswa kujua chanzo chake hasa ni nini:
1. Je, ni vita ya Ukraine?
2. Je, ni ukame wa msimu uliopita ambao tulishuhudia mafuriko maeneo mbali mbali ya nchi na kusababisha uharibifu wa miundombinu hususani barabara zetu?
3. Je, ni akiba yetu ya taifa ya chakula (Strategic National Grain Reserves) imeshindwa kufidia upungufu uliopo wa chakula nchini kama ilivyo jukumu lake?
4. Je, ni hayo mamisafara ya malori ya urefu wa kilomita 7 kila siku yanayofanywa na wafanyabiashara (middle men, not our peasants) kupeleka chakula chetu kwa nchi jirani waliokuwa na uhaba wa chakula uliosababishwa na lockdowns walizojiwekea wakati wa mlipuko wa covid? Kwa nini sisi ambao hatukuji lockdown ndiyo tupate shida?
5. Je, ni kwa sababu ya kupanda kwa bei ya mafuta ya petroli na dizeli iliyosababishwa na sisi kususia kununua mafuta hayo toka Urusi, ili kuwaunga mkono West Europe ambao wao hata hivyo wanaendelea kununua gesi kutoka Urusi? West Europe wanalalama na kuishutumu sana Urusi kwa kuwabania gesi yao hasa kwenye kipindi hiki cha kuelekea winter. Kwa nini na sisi au kama East Africa Union tusiwe na msimamo kama wa Uchina na India wa kununua mafuta haya kutoka Urusi ili kuepukana na balaa hili la kupanda kwa bei ya vyakula. Mseveni na Ruto wameonesha dhamira hii.
6. Je, mfumuko huu wa bei unauhusiano na upandishaji wa mishahara ya watumishi wa umma? Jee itakuwaje pale serikali itakapopandisha mishahara ya taasisi binafsi hivi punde? Awamu iliyopita iliogopa sana kupandisha mishahara hii kwa kuogopa kuleta mfumuko wa bei kama zilivyo kanuni za kiuchumi.
Nini kifanyike kinategemea na majibu ya maswali hayo na mengine mtakayopendekeza.