Naepuka lawama

Naepuka lawama

Upiversity

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2015
Posts
3,487
Reaction score
2,634
Ugomvi wa baba na mama,siwezi kuingilia kwa sababu ningali mdogo,wapo wazee,majirani na ndugu watakaosuluhisha!
Ingawa rafiki zangu wananilaumu,eti siwajali wazazi wangu tena siwajali kwa shida na mambo yao,sio kweli mimi nasema,ukweli ninao mwenyewe.

NITAWAELEZA;

Hata kama baba ndie mwenye kosa nifanye nini, hata kama mama ndie mwenye kosa niamueje mie! Nisije kosa radhi ya baba nisije kosa radhi ya mama!

#Naepuka Lawama,naepuka lawama,miimi sio mtoto wa upande mmoja, nisimame upande gani mwenzenu?Nisije nikaharibikiwa!
 
Upiversity

Binafsi sijawahi kuona my parents wakigombana . Ila kama ingetokea at first I wouldn't know what I would do honestly . May be I would probably talk to them in different times privately and hear their complains . After that nitaongea nao wote kwa pamoja . Thanks..
 
Last edited by a moderator:
Mtetee mama, tena umpiganie haswa awe salama. Mama anatakiwa kulindwa kwa nguvu zote; UTAOMBA RADHI BAADAE KWA BABA HASIRA ZIKIPOA, ila mama yupo salama kuliko umwache mama akiaibishwa na kuvuliwa nguo mbele ya halaiki. Mpiganie mama kwani yeye ndo anajua uchungu wako, ulikuwa ukirusha vipi miguu tumboni, ulikuwa unakula vipi ulipo kuwa tumboni. Acha masikhara ndugu, MAMA YANGU NITAMLINDA KWA GHALAMA YOYOTE, nampenda sana MAMA YANGU.
 
sometimes kama mama anajielewa dingi hata ukimpotezea haina shida.
ngoma inakuja kama mama naye ni kama kina wema sepetu au faiza.!!
utaona bora usepe na dingi tu.
 
Mama yangu mimi niache aonewe adhalilishwe
Nampenda sana mama
Namlinda mama yangu
Namtetea kadri niwezavyo
Sijali ni nini wala na nani nahata iwe wapi
 
sometimes kama mama anajielewa dingi hata ukimpotezea haina shida.
ngoma inakuja kama mama naye ni kama kina wema sepetu au faiza.!!
utaona bora usepe na dingi tu.

hahahahahaha....umenikumbusha kitu aisee
 
Nakumbuka miaka ya nyuma
Nilipopokea barua kutoka kwa mama,akinipa malalamiko yake
Kwamba Yupo mbali na Baba!
Kwa uchungu niijibu barua ya Mama,
Ya kwamba nitajaribu kuwasuluhisha
Lakini hilo lilinishinda
Leo,nawaeleza muelewe jamani
Sitaki mnilaumu mie mwenzenu,
MATATIZO YAMENIZIDI UMRI!!
 
Wazazi wote muhimu,na unapo taka kusuluhisha basi akikisha unawaita wote,kwanini aibu ya nyumbani kwenu uitoe nje?
ongea nao na pia watakuona mtoto wao umeshakua mkubwa na huenda ikawa ndio sababu ya wao kutokugombana tena..
 
Nilikuwa darasa latano kipindi hicho, nilikuwa mimi na wadogo zangu wawili. Kawaida yetu ilikuwa kila tukimaliza kula chakula cha usiku tunapumzika kidogo, halafu tunasali, na kama kuna mwenye homework anafanya na anaingia kitandani na kulala. Sikuhiyo baba alikuwa hajarudi kipindi nafanya homework baada ya kuwa tumemaliza kusali na mama pamoja na wadogo zangu walikuwa tayari wamesha lala.

Takribani saa sita usiku baba akarudi akiwa chakali amelewa, alibisha hodi mama akaamka na kumfungulia, alikuwa mkali sijawahi kumwona baba yangu akiwa mkali vile, akamnasa mama makofi mbele yangu, mama aligumia kwa maumivu, hali ile iliniuma sana mpaka nikalia. Hakuishia hapo bali alimrushia mateke kana kwamba anapigana na mwanaume mwenzake.

Mama aliumia sana, nami sikuweza kuvumilia haliile, kipindi hicho tulikuwa tumeagizwa fimbo za kupeleka shuleni aina ya mikamilwa, nilichukua fimbo mkamilwa mmoja nikamfuata baba aliyekuwa amemwangusha mama chini nakuendelea kumpa makonde yasiyonaidadi. Kwahasira na nguvu nilimtiririshia baba mvua za fimbo mgongoni mpaka nayeye akapiga mayowe.

Akamwacha mama na kuanza kunikimbiza, kwakuwa mlango ulikuwa haujafungwa nilitoka mbio nayeye yupo nyuma yangu anakuja mbio anikamate, nikakimbilia sehemu moja iliyokuwa imezibwa njia kwa miiba ya michongoma. Kwakuwa sehemu ile nilikuwa naijua nikairuka miba ile nayeye hakuwa akijua kama kuna miba, aliingia mzimamzima.

Alikipata hakika. Nikahamia kwa rafiki yangu wiki nzima na mama akawaomba wazee watusuluhishe mimi na baba. Nilimwomba radhi baba na akanisamehe. Je nisingechukua maamuzi magumu kama hayo mamaangu siangeuwawa mbele yangu namwona?
 
Weeeeeeeeeeeeeee mama kitu kingine aisee,! Miezi 9 tumboni kwake, kashika sana mikojo yangu afu leo eti apigwe mbele yangu, DINGI usirogwe ukajaribu kumrushia ngumi bi mkubwa aisee.
 
Ulifanya la maana
Nilikuwa darasa latano kipindi hicho, nilikuwa mimi na wadogo zangu wawili. Kawaida yetu ilikuwa kila tukimaliza kula chakula cha usiku tunapumzika kidogo, halafu tunasali, na kama kuna mwenye homework anafanya na anaingia kitandani na kulala. Sikuhiyo baba alikuwa hajarudi kipindi nafanya homework baada ya kuwa tumemaliza kusali na mama pamoja na wadogo zangu walikuwa tayari wamesha lala.

Takribani saa sita usiku baba akarudi akiwa chakali amelewa, alibisha hodi mama akaamka na kumfungulia, alikuwa mkali sijawahi kumwona baba yangu akiwa mkali vile, akamnasa mama makofi mbele yangu, mama aligumia kwa maumivu, hali ile iliniuma sana mpaka nikalia. Hakuishia hapo bali alimrushia mateke kana kwamba anapigana na mwanaume mwenzake.

Mama aliumia sana, nami sikuweza kuvumilia haliile, kipindi hicho tulikuwa tumeagizwa fimbo za kupeleka shuleni aina ya mikamilwa, nilichukua fimbo mkamilwa mmoja nikamfuata baba aliyekuwa amemwangusha mama chini nakuendelea kumpa makonde yasiyonaidadi. Kwahasira na nguvu nilimtiririshia baba mvua za fimbo mgongoni mpaka nayeye akapiga mayowe.

Akamwacha mama na kuanza kunikimbiza, kwakuwa mlango ulikuwa haujafungwa nilitoka mbio nayeye yupo nyuma yangu anakuja mbio anikamate, nikakimbilia sehemu moja iliyokuwa imezibwa njia kwa miiba ya michongoma. Kwakuwa sehemu ile nilikuwa naijua nikairuka miba ile nayeye hakuwa akijua kama kuna miba, aliingia mzimamzima.

Alikipata hakika. Nikahamia kwa rafiki yangu wiki nzima na mama akawaomba wazee watusuluhishe mimi na baba. Nilimwomba radhi baba na akanisamehe. Je nisingechukua maamuzi magumu kama hayo mamaangu siangeuwawa mbele yangu namwona?
 
Mama ni mama lazm umtete na ukikaidi akikuachia radhi haki yako.
 
Pole ndugu, issues za wazazi wenye migogoro ni ngumu sana. Mungu akupe busara na hekima katika kutatua matatizo ya wazazi wako.
Tunasubiri full story.
 
Kweli umenifanya nimecheka na umenikumbusha mbali mnoooo."eti ukamtiririshia mvua ya fimbo"najaribu kuimagine ulivyokuwa unamcharaza baba ako.kweli nimecheka mno
 
Mkuu OLD KOROGWE unaona mwisho wa siku WAZEE ndio waliokuja leta SULUHU?na ni mama mwenyewe uliekuwa unamtetea ndie aliewaita?..na ulimuomba baba radhi kwa sababu ulimkosea!
Ugumu bado upo kuingilia ugomvi wa wazee!
 
Last edited by a moderator:
Pole ndugu, issues za wazazi wenye migogoro ni ngumu sana. Mungu akupe busara na hekima katika kutatua matatizo ya wazazi wako.
Tunasubiri full story.

kweli kabisa mkuu!...na ndo mana naepuka lawama,mimi sio mtoto wa upande wa mmoja!,hata kama baba ndie mwenye kosa nifanye nini?
 
Mkuu OLD KOROGWE unaona mwisho wa siku WAZEE ndio waliokuja leta SULUHU?na ni mama mwenyewe uliekuwa unamtetea ndie aliewaita?..na ulimuomba baba radhi kwa sababu ulimkosea!
Ugumu bado upo kuingilia ugomvi wa wazee!

Nikweli ningumu kuingilia ugomvi wawazee, lakini pale inapobidi hakunabudi kufanya hivyo na mengine baadae. Kuokoa uhai wa mtu ni bora kuliko lawama.
 
Back
Top Bottom