bampami
JF-Expert Member
- Nov 5, 2011
- 5,700
- 4,126
Watanzania bwana! Kila unapoenda hawakosi cha kukuagizia Ukienda mwanza utasikia utuletee samaki! Ukienda Mbeya tuletee mchele na maparachichi! Ukienda Tanga tuletee machungwa! Ukienda Moshi tuletee kahawa! Ukienda Tabora tuletee asali! Ukienda Morogoro tuletee magimbi! Ukienda Kigoma utasikia tuletee mawese! Ukienda Mtwara tuletee korosho! Ukienda Bukoba tuletee ndizi! Ukienda Zanzbar tuletee tv au deki! Ukienda Singida tuletee mafuta ya alizeti! mbaya zaidi sasa ukienda Iringa utasikia tuletee msichana wa kazi. Dah! Mi naenda Ujerumani sijui nikuletee nini.