Naenda kwa mama..............

Naenda kwa mama..............

tindikalikali

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2011
Posts
4,854
Reaction score
1,139
Mtu na mkewe wanagombana chumbani, ghafla ugomvi unakuwa mkubwa mke anaamua kukusanya vitu vyake kwa lengo la kuondoka. Mume anashangaa anamuulizaa: Unakusanya vitu unaenda wapi? Mke kwa nyodo anajibu: Nakwenda kwa mama yangu. Mume naye akaanza kukusanya nguo zake na kuweka kwenye mabegi yake, mke kwa jeuri akamuuliza mume wake: Unapaki unakwenda wapi? Mume akajibu kwa tabasamu: na mimi nakwenda kwa mama yangu. Mke akauliza tena "Hawa watoto wako watabaki na nani:Mume kwa kujiamini akajibu Nao waende kwa mama yao kama sisi tunavyokwenda
kwa mama zetu.
 
Hapo bi mkubwa inabidi abaki,teh teh teh teh...
 
Umetisha kaka\
 
Safi sana,tuone sasa,watoto nao waende kwa mama yao!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom