Naenda kuishitaki Jamhuri.... Kesho

Padri Mcharo

JF-Expert Member
Feb 28, 2015
1,899
3,683
Wakuu....

Achaneni na kichwa cha habari kwanza, nataka nijue haya kabla cjafanya lolote.

Madaraka ya Raisi wa Jamhuri ya Muungano:

1. Raisi anaweza kufuta uraia wa mtu (hata kama ni mzawa)
2. Raisi anaweza kumfukuza mtu nchini (hata kama ni raia mzawa)
3. Raisi anaweza kumpiga mtu mafuruku aliyeenda nje ya nchi kurudi nchini
4. Raisi anaweza kufuta leseni ya elimu ya mtu (mfano akaifuta degree yako) mnakumbuka yule daktari mtwara alifutiwa leseni na Mh Majaliwa. Lowassa nae nakumbuka alfutaga leseni ya Engineer wa ujenzi Dar.
5. Raisi anaweza kuchukua ardhi yoyote ya mtu kwa amri
6. Raisi anaweza kumfunga mtu jela kwa muda usiojulikana (mpaka atakapoamua yeye)
7. Raisi anaweza kufungia account za mtu za bank (zilizo ndani na nje ya nchi)
8. Raisi anaweza kufuta validity ya passport ya mtu na kuzuia usipewe passport milele
9. Raisi anaweza kukupiga marufuku kutoka mji mmoja kwenda mwingine (mfano marufuku kutoka nje ya dar maisha yako yote)

Je kuna lolote ambalo niko opposite hapo wadau wa sheria??????

Hivi vitu napenda kuvijua ili kuwa na confidence kwenye masuala fulani fulani.
Karibuni.
 
Back
Top Bottom