"Nadharia ya Ugwekaji" Athari za Ugwekaji katika maisha yetu.

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,460
52,101
UGWEKAJI JINSI UNAVYOATHIRI MAISHA YETU.

Mwandishi, Robert Heriel
0693322300
Kazi: "Natharia ya UGWEKAJI"
Maandiko ya Robert Heriel katika Lugha ya Kiswahili.
© 2021 Haki zote ZIMEHIFADHIWA.

DONDOO
I. Maana ya Ugwekaji (Utangulizi)
II Aina za Ugwekaji
III. Sababu za Ugwekaji.
IV. Athari za Ugwekaji katika maisha yetu ya kila siku.
IV. Hitimisho.

Muhtasari wa Nadharia ya UGWEKAJI

UTANGULIZI

Ulishawahi kufikiri mtu Fulani ni mwema lakini baadaye ukagundua ni mbaya, au ulidhani ni mbaya lakini baadaye ni Mwema. Pengine ulishawahi kupewa hadithi za mtu Fulani ukamfikiria Kwa namna ambayo siku uliyokutana naye ukaona ni tofauti kabisa na ulivyomdhania.

Nafikiri wengi wetu tumeshawahi kuongea na watu Kwa njia ya simu au mitandao ya kijamii tukawaona na kufikiri wapo hivi lakini siku tulipokutana nao live tukashangaa kuona wako vile(tofauti na mawazo yetu).

Kwa tulioenda shule, mtakubaliana nami kuwa, kuna wakati nyakati za mitihani ya shule au Chuo kabla hatujaingia kwenye chumba cha kufanyia mtihani akili zetu zinafikiri mtihani utakuwa MGUMU Lakini ukiingia kwenye paper unakuta mtihani kumbe ni rahisi. Au kinyume chake kuwa ulifikiri mtihani utakuwa mrahisi lakini kuingia kwenye paper unakuta Ngoma ngumu.

Au paper ni ngumu hivyo unaona utafeli lakini unashangaa umefaulu, na zile paper ulizoziona rahisi ukashangaa ukafeli.
Je uliwahi pata uzoefu huo?

Je ulishawahi kudhani maisha ni rahisi baada ya kumaliza shule au Chuo lakini ulipomaliza ukakuta magumu tofauti na ulivyoyaona awali. Au kinyume chake?

Katika mahusiano, nafikiri wengi wetu tumewahi kupitia Ile Hali ya kufikiri Fulani(Mpenzi umtakaye) hawezi kukukataa lakini ukashangaa ulipoenda kumtongoza ukapigwa cha mbavu. Au Yule uliyedhani atakukataa ukashangaa anakukubalia kirahisi. Ulishawahi kupata uzoefu huo?

Ikiwa ni hivyo nadharia ya UGWEKAJI ndio inazungumzia mambo/vitu mfano wa hivyo.

UGWEKAJI ni moja ya nadharia niliyoiandika mwenyewe(Mimi Taikon) ambayo ipo katika kitabu cha nadharia za Taikon; nadharia hii nimeiandika Kwa manufaa ya kizazi hiki na kile kijacho.

UGWEKAJI ni Ile Hali/kitendo cha kitu au Jambo kuonekana tofauti na lilivyo. Ni kitendo cha kitu au Jambo kuchukuliwa tofauti na jinsi lenyewe lilivyo.
UGWEKAJI ni kitendo cha kitu au Jambo kugeuka kutoka vile watu walionavyo, walichukuliavyo na kubadilika na kuwa tofauti na Mitazamo au muono wao.
UGWEKAJI ni Ile Hali ya Jambo au kitu kubadilika kutoka kwenye uzuri kwenda kwenye ubaya, au kutoka kwenye ubaya kwenda kwenye uzuri.

Hata hivyo Jambo linaweza lisiwe zuri lakini likafanywa kuwa Baya, au Jambo linaweza kuwa Baya lakini likafanywa kuwa zuri, hii huitwa UGWEKAJI-HILA.

UGWEKAJI unaweza kufanywa kwenye kitu au jambo.
Mathalani, unaweza kuta kitu kimepambwa vizuri lakini kikawa kibaya, au Kwa nje kitamu lakini Kwa ndani kichungu, huo ni Ugwekaji.

Pia kwenye mambo Kama Elimu, dini, Siasa, Afya n.k Ugwekaji upo.

Mtu anayefanya Ugwekaji huitwa MGWEKA. Hakuna Ugwekaji pasipo MGWEKA.
UGWEKAJI hufanyika Kwa sababu kadhaa WA kadhaa. Hii ni kusema WAGWEKA Hufanya Ugwekaji Kwa sababu mbalimbali, miongoni mwa sababu hizo ni pamoja na;

1. Kisasi au chuki.
UGWEKAJI hutumika zaidi kulipa kisasi. Mtu huweza kufanya mzuri ili umuamini alafu akabadilika ghafla na kukuangusha au kukuangamiza.

2. Biashara na kujipatia Faida.
WAGWEKA hutumia Ugwekaji kukuza majina Yao, bidhaa zao, kujipatia faida na mahitaji Yao.

Nitatoa mifano miwili au mitatu ya Ugwekaji katika Mambo halisi.

Mfano 01.
UGWEKAJI katika IMANI.
Katika Vitabu vya dini Ugwekaji umetokea katika Maeneo mengi, Ila eneo maarufu ni lile lililotokea Bustani ya Eden.
Kisa cha Tunda la Kati. Adam na Hawa walikatazwa wasilile kwani watakufa(kumaanisha ni sumu) lakini Nyoka anafanya Ugwekaji kuligeuza Tunda lile kuwa zuri na wala halima ubaya wowote Kama vile Mungu alivyo waagiza Adamu wasilile.

Hawa anakuona Tunda lafaa Kwa Kula na linatamanika, kumbuka Mwanzoni hakuliona hivyo Bali maneno ya Nyoka ndio yanamfanya aone hivyo. Hii ni kawaida kwenye Ugwekaji kwani huanzia Fikarani, ndipo huenda machoni. Wanakula Tunda kisha wote wajiona wapo uchi(Ugwekaji mwingine kwani Mwanzoni hawakujiona hivyo, walijiona wapo Sawa). Baadaye wanapata athari Kama walivyo ahidiwa na Mungu.

Sijui kama ninaeleweka.

Mfano wa 02
UGWEKAJI katika Elimu.
Elimu ni Jambo zuri lakini WAGWEKA huweza kuingiza hila zao na kuifanya elimu kuwa mbaya Kwa lengo la kujipatia kipato.

WAGWEKA katika Elimu waliikuza na kuitangaza elimu kuwa ni ufunguo wa maisha (Jambo ambalo ni kweli) lakini wakagweka baadhi ya Mitazamo ndani ya elimu kuwa ukiipata elimu watakayokupa utakuwa na maisha mazuri Kwa kufanya kazi nzuri, yenye mishahara mizuri. Katika hila Yao hapo Wagwekaji ambao ni waathirika wakajikuta kadiri wanavyosoma ndivyo wanavyodharau kazi zenye vipato vidogo na zile zakutoa jasho,
Wakasoma makundi Kwa makundi na Kuhitimu wakiwa wengi wakiwa na mtazamo kuwa baada ya elimu maisha yatakuwa bwerere kumbe walifanyiwa Ugwekaji pasipo ya wao kujua.

Walipohitimu hawakuamini kwani hawakupata vile walivyodhani watapata.


Mfano wa 03
UGWEKAJI katika Mahusiano.
Wengi hupenda wenza wenye mvuto, tabia njema na wenye vipato. Kwa watu kujua hayo hujigweka ili wapendwe. Vijana hujifanya maridadi watanashati na wenye tabia thabiti za kiume za utafutaji, wanawake nao hujiweka Safi, urembo na wenye tabia za kutamanika kuwa mke.
Ndoa ikishafungwa Mambo hubadilika, tabia halisi hufichuka na mambo huwa mabaya zaidi.

Pia wapo wenye tabia mbaya, wenye mivuto ya kukasirisha, na wasio na pesa lakini hayo yote sio Kwa mapenzi Yao isipokuwa mazingira ndio yaliwafanya hivyo. Baadhi Yao waingiapo kwenye mahusiano ya kindoa hubadilika na kuwa watu tofauti na vile wenza wao walivyokuwa wakiwachukulia. Huwa watu Bora na wenye manufaa ndani ya jamii.

Tuishie hapa Kwa leo. Itaendelea.

Wakati ujao tutaona namna Ugwekaji unavyoweza athiri maisha yako, nini ufanye uepukane na WAGWEKA ili wasiharibu maisha yako.

Ni Yule Mtibeli

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Back
Top Bottom