Nadharia hii itawashangaza hata wanawake wenyewe…..!

Hiyo ndio formular ya maisha yangu...simshauri mtu kuhusu ndoa yake unless huyo mtu awe ndugu yangu kwani ndugu atakasirika lakini undugu haufi.

Kuna jirani yangu mmoja, mkewe(sijui ni sahihi kusema hivyo maana wana miaka 5 bila ndoa) ni mtu wa kutembeza kitumbua chake hovyo, sasa hapa mtaani watu wanamsema ile mbaya, mumewe ni mtu wa kusafiri sana, hivyo anaonekana kwa mara moja au mara mbili kwa mwezi. sasa wambea wakamwenleza yote bila kuficha hata moja, jamaa kwa ghadhabu kamfukuza mkewe...

Siku moja akaniomba tuzungumze kidogo, tukaenda zetu Mtambuzi Pub, tukaagiza maji baridi hatukutaka kupata kilevi ili tuongee tukiwa na kili timamu. Yule bwana ndo akaniambia kwmaba kamtimua mkewe kwa kuwa ni malaya na hadithi kibaoo, hata hivyo alitaka kujua maoni yangu maana tunaishi nyumba moja.

Kwa bahati alishaongea na mke wangu na mke wangu alikanusha kujua lolote kwa sababu yuko bize na shughuli zake na hasindi nyumbani. na mimi kama mama Ngina nikasema hivyo hiyo. Ila nikamsaidia kitu kimoja. kwa sababu hata hivyo niliona majirani walizidisha uwongo mwingi sana na kutia chumvi ili mwenzao aachike.

Nilimshauri achunguze. nilimwambia kwamba akisikia jambio lolote kuhusu mkewe ni vyema achunguze ili kujiridhisha kuliko kuchukua maamuzi ya kukurupuka. nilimshauri amrudishe mkewe ajipe muda wa kuchunguza tuhuma hizo. ni kweli alifanya hivyo,. alimweleleza mkewe kwamba mimi na mama Ngina tumemtetea sana. aliporudi nyumbani alikwenda kwa mke wangu na kushukuru kwa wema wetu lakini pia aliapa kwa miungu yake yote kwamba hata kaa arudia kufanya umalaya tena katika maisha yake.
 
Katika dunia hii hakuna kiumbe tata kama mwanadamu...! Wakilia hutoa machozi, wakicheka hutoa machozi...! Wengine wakikasirika hung'ata meno, wakitabasamu hung'ata meno...! The only organism which can say YES, meaning NO, and vice versa.....!
 
sababu wanaume wenye fujo mara nyingi uwa na akili nyingi sana, na wanajua jinsi ya kuiteka akili ya mwanamke. Ndio maana ipo ivo
 
kuna nadharia kuwa wanawake wanawapenda wanaume wakorofi na wenye tabia za ajabu (bad guys in general) nikiiangalia hii na ya kwako naona hawa ni viumbe wa ajabu sana. Sijui nijifunze ka ukorofi kidogo?
 
nyumba kubwa asante kwa kushare stories hizi, na dingi asante kwa kutukumbushia hizi issues. Kuna dada nafanya nae kazi, mumewe ni controlling na haoni kwamba it is wrong. Na haamini wenzie wakisema hawapitii manyanyaso anayopata yeye.
Ila nilijifunza kwa ndugu yangu mmoja.kitambo. Alikuwa anapigwa na mumewe. Mama wa haja ana wowowo la kufunga mtaa, mume mwembamba kama cartoon. Siku moja dada karudi kwao. Tukaenda na kakake, kaka akamuambia huwa sielewi ukisema ile cartoon imekupiga. Si umpige na wewe? Yaani the next time yule dada kapigwa alishusha kipondo kwa mumewe cha mwaka! Na akatimua akakaa kwao kama mwaka. Mumewe alikuwa mlevi sana, ule usingle ulimsaidia kuacha na pombe, kaokoka anahubiri injili na mkewe alirudi anyways. Sasa hivi raha mustarehe!

Mie husema siku mume aseme ananipiga nitamuua na nitaenda kutoa taarifa polisi wakienda kukamata wanakuta mzoga. Atasema na tv, stuli, sufuria na majagi. Na baada ya kubondana polisi waje wamchukue ili mie nikalale nyumbani kwangu. Na hakuna negotiation hapo wala kurudisha kesi nyumbani. Kwa kweli i hate all abusive men, nawadharau na akili na moyo wangu wote na nadhani they are cowards!!!
 
Last edited by a moderator:

Ahsante mama Ngina kwa kunizalia chema........
Itakuwa ajabu eti napiga tilalila hapa kumbe hata wanangu wanapondwa na mijanadume isiyopitia jando la porini...LOL
 
Main_African_American.jpg

Mnamo Agost 23, 1973, majambazi wawili wenye silaha aina ya machine gun, walivamia benki moja jijini Stockholm, Sweden. Mmoja kati yao ambaye Alikuwa ametoroka jela siku chache nyuma, Jan-Erik Olsson alitangaza kwamba, “Shughuli imeanza.”

Majambazi hao waliwashikilia mateka watu wanne, wanawake watatu na mwanaume mmoja. Mateka hao walifungwa mabomu miilini na kushikiliwa ndani ya benki hiyo kwa muda wa saa 131, ikiwa na maana kwamba, walishikiliwa kwa siku tano. Mateka hao waliokolewa Agosti 28 na majambazi hao kukamatwa.

Baada ya kuokolewa, mateka wawili walionyesha jambo la kuchangaza na pengine kutisha, kama siyo kuudhi kwa baadhi. Walifanyaje?

Pamoja na kufungiwa mabomu na watekaji wale, kutishwa, kudhalilishwa na kuishi kwa hofu kuu mikononi mwao, lakini walipookolewa wanawake wawili kati ya hao watatu waliwakumbatia na kuwabusu wale majambazi kwa bashasha. Lakini pia waliamua kuwapenda na kuwasaidia majambazi wale.

Walipohojiwa na vyombo vya habari vya nchi hiyo, walisema, hata watu wa usalama walipofika kuwaokoa, walishajenga upendo kwa watekaji, wakiamini kwamba, ni kweli watekaji walikuwa wakiwalinda kutoka kwa polisi.

Baadaye mwanamke mmoja kati yao alifunga uchumba na jambazi mmoja. Mwanamke wa pili alianzisha mfuko kuwachangia wale majambazi fedha za kuwawezesha kupata huduma bora za kisheria ili wasifungwe au kupata adhabu nafuu. Kumbuka hawa wanawake ndiyo waliokuwa wamefungiwa mabomu wakati wa utekeji…!

Hali hii ambayo baadaye ilikuja kupewa jina la Stockholm syndrome, imekuwa ikitambuliwa katika Saikolojia kwa miaka mingi kabla ya tukio lile la Stockholm. Kilichotokea kwenye tukio hili, ni wale waliotekwa kujifunga kihisia na watekaji.

Hali hii imewahi kujitokeza huko nyuma kwa watekwaji wengine, wafungwa na kwenye ufujaji wa aina mbalimbali ukiwemo ule wa watoto, wanawake, na wafungwa wa kivita. Imebainika na inafahamika vizuri sana kwamba, uamuzi wa mateka kujibainisha na kujifunga kihisia na watekaji huwa ni mkakati wa mateka kujiwezesha kuendelea kuishi. Kwenye uhusiano wa kifujaji, mwanamke anayefujwa anaweza kuamua kumtetea na kumpenda zaidi mumewe ikiwa ni mkakati wake wa kujiweka katika mazingira ya kumudu kuendelea kuishi.

Kwa hiyo, mwanamke kufujwa na mumewe na bado mwanamke huyo akamtetea mumewe, akawa tayari kufa kwa ajili yake akimlinda asichukuliwe hatua za kisheria kwa kumpiga kwa mfano, ni jambo ambalo kwa wanasaikolojia halishangazi tena. Lakini halishangazi kwa polisi ambao wamekutana sana na kesi za wanawake wanaofujwa.

Kuna wanawake wengi ambao hufujwa na waume zao, lakini wao ndiyo wako mstari wa mbele kuwatetea waume hao wasiadhibiwe. Kuna wakati wanawake wanaofujwa huenda kuwawekea dhamana waume zao ambao wamekamatwa kwa kuwapiga wao (wake) kuna wakati wanawake hao wako tayari kuwatukana au hata kuwageuka na kuwashambulia watu wanaokuja kuwasaidia wakati wakipigwa na waume zao……………!
Cynthia Masasi ndio aombewe
 
kuna nadharia kuwa wanawake wanawapenda wanaume wakorofi na wenye tabia za ajabu (bad guys in general) nikiiangalia hii na ya kwako naona hawa ni viumbe wa ajabu sana. Sijui nijifunze ka ukorofi kidogo?

Naomi Campbell na billionaire boyfriend .yaani Naomi ni drama Tupu ila huyu mrusi wake ambae Ana mke Amefika kwa drama queen .
 
Back
Top Bottom