G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,555
- 35,880
Naamini hata kama ni mimi ningekuwa ndiye Katibu mkuu wa Chadema kwa sasa, basi ningeuona uzembe wa dhahiri nilio nao. Uzembe ambao mimi kuwa nao unaendelea kukigharimu chama changu ninachokiongoza. Ningeamua kujitafakari ili nitoe nusura.
Tuwe wa kweli. Haiwezekani katibu mkuu yupo miaka mingi tu sasa bado hajajua kujisimamia kama katibu mkuu. Kweli huyu ni katibu mkuu wa chama kikubwa kama Chadema?
Intelijensia ya Chadema inaundwa chini ya ofisi ya katibu mkuu. Baada ya katibu mkuu "kufa" kisiasa na kiushawishi hiki chombo muhimu cha chama nacho kimekufa. Haiwezekani mfano Tundu Lissu pamoja na madhila aliyonayo bado anaonyesha kujituma kwa Chadema kuliko katibu mkuu ambaye yupo ofisini kila siku na mzima wa afya.
Kupooza kwa ofisi ya katibu mkuu chini ya Mashinji kumewafanya hata wasaidizi wake wawili ambao hapo kabla ya ujio wake walikuwa machachari sana lakini ghafla nao wamepooza! Hii kusema kweli ni kutokana na kukosa morali kutoka kwa boss wao. Mtu kama Mbowe huwezi kutegemea akafanya kila kitu ndiyo maana Chadema ilipokuwa chini ya Dr. Slaa ilikuwa kweli chini yake na alionyesha kulimudu vyema jukwaa la kisiasa Tanzania.
Hatuwezi kutoa kisingizio endelevu cha kuzuiwa kwa mikutano ya kisiasa. Hilo lipo kila sehemu, sasa ni wajibu wa kiongozi kujitoa kweli kweli. Kama ni kesi hata kina Slaa waliwahi kuzushiwa mpaka za kujaribu kumuua Zitto na bado walikomaa. Najikuta nikishangaa kesi moja aliyo nayo Mashinji pale Kisutu imemfanya aone kama ndiyo mwisho wa maisha! Lazima kugangamala.
Naamini Chadema kwa mara ya kwanza imempata katibu mkuu asiye sahihi kisiasa. Hata hivi leo tungekuwa na Benson Singo nadhani ingekuwa tofauti sana.Siasa za upinzani kwa Afrika nzima ni kupigana tena kweli kweli. Mtendaji mkuu wa chama ni lazima aonyeshe uhai kweli kweli.
Kwakweli Chadema ni lazima ione haja ya hali ya dharura.
Hata Lissu leo anasema kuwa Chadema yapo pia matatizo ya kujitakia na kwa uhakika kabisa pamoja na mengine pia anaigusia ofisi ya katibu mkuu ambayo imedhoofu isivyo kawaida!