Nadhani nimesahau kukasirika

Nadhani nimesahau kukasirika

Ngoja nimalizie stori

Shule ya msingi niliyosoma alikuja mwalim mpya, huyu alijaribu kuongea na mimi akitumia njia tofauti. Nadhani aligundua kipengele cha upweke wangu neio akakaza hapo. Aisee alikuwa akinipa muongozo ambao umenikenga mpaka leo. Yule jamaa mpaka leo namkumbuka sana.

Nikaanza kujiweka mbali na vitu vinavyonikasirisha, mwanzo ilikuwa ngumu. Alinielekeza kunyamaza kimya na kuhesabu kimya kimya mpaka 20 kabla ya kumjibu mtu yeyote. Nikaanza kuwa 'neo zezeta' wakati mwingine nikipata ghadhabu wakati nikihesabu kimoyomoyo najikuta napiga mguu chini kwa nguvu, au na-crush nilichokishika, wakati mwingine napiga ngumi ukuta yaani ilimradi tu hasira zipungue bila kumdhuru mtu.

Miaka hiyo kulikuwa na zile kalam za wino za kuandikia zinaitwa BIC, basi hizo zimeshanichanachana sana mikono zile glass zake nikizivunjia mkononi au mfukoni. Sema Mungu mkubwa makovu madogo kwenye viganja vya mikono huwa yanafutika na kupokea kabisa.

Kucontrol hasira kulianza kuniweka karibu na baadhi ya watu ambao wamepelekea mpaka leo nimemaliza chuo kikuu, namshukuru Mungu kwani sijui kama primary yenyewe ningeimaliza.

Nachoshukuru kingine ni kuwa, pamoja na kiburi na hasira zile ila nilikuwa siibi cha mtu. Watu walikuwa wananitegea nikiiba wanipige waniue (nilikuwa naboa) lakini haikutokea, hiyo ikawa ndio pona yangu.

Kati ya mwezi August na September mwaka jana nilienda kijijini nilipokulia, niliwaona watu baadhi wanaotembea kwa kuchechemea kwa ajili ya kilema nilichowatia, niliona mtu mwenye kovu kubwa kichani, nikakumbuka it was all my doing, kuna mtu mwingine nilikutana nae mkono wa kulia umepinda nikamkumbuka, nilimvuja mkono sehem mbili, wazazi wake hawakumpeleka hosp, wakamtibu kienyeji. Sipendi kuielezea hii.

Napapenda kijijini kule na watu hunichukulia kama mfano unaoishi, uthibitieho wa muujiza ila ile guilty inaninyonga mno.

Sasa hivi nina theory naiita 'tinting' yaani kumpuuza mtu anayenitafuta ugomvi. Sasa hii inanifanya nazidi kudharaulika. Nashindwa kujitetea, nahesabu kila neno nalozungumza nikianzisha mazungumzo na watu. Siku za karibuni nimeanzisha ucheshi na utani kwa watu wachache niliobahatika kuwazoea, ila naona I am not good at it. Najiona kama naigiza maisha. Wakati mwingine najishtukia mwenyewe.

Pamoja na kuwa nina uwezo mkubwa wa kusoma saikolojia ya mtu, lakini nashindwa yani kuendana na energy ya kila mtu. Mtu akiniona negative, nafunga 'tinted' sasa inanipa shida. Kwa sababu ya kutozoea kuishi kijamii sana, kauli zangu huwa zimekaa kimaamizi sana. Watu hawapendi hiyo, wanaamini katika majadiliano. Sasa mpaka nakosa niganyaje.

Kipengere muhimu sasa, hata kwenye mahusiano hali hii inaniathiri. Ni afadhali ningekuwa nakasirika nafoka yanaisha. Ila siwezi. Yaani nikiudhiwa, nafunga vioo 'kufunga ubalozi' nabaki natafakari suala kimoyomoyo mpaka nafikia maamuzi bila kujadiliana. Huwa nawaepuka wapenz naokuwa nao, nakata mawasiliano kuepuka ugomvi, nakaa kimya, na wakati mwingine hata kuziacha kabisa namba zangu za simu.

Nilishawahi kumkimbia mpenzi wangu geto nilikopanga baada ya kunizingua, nilikaa kitaa muda mrefu bila kumrudia, akanitafuta sana tusuluhishe, akaharibu akanitafuta kupitia mtu pekee anayenifahamu, na akatumia approach mbaya akazidi kuharibu. Na hadithi yetu iliishia happ.

Suala linaloniharibu zaidi ni lawama. Aisee lawama huwa zinanitafuna mno. Na zimenikosanisha na watu wengi mno. Nimefunga ubalozi na watu lukuki kisa nimelaumiwa. Kipengere ni kuwa mimi siwez kujitetea kukanusha madai. Siwezi kumshawishi mtu aamini kinyume na alivyodhania.

Mimi huishi nikijua, siibi, siui, sio mnafiki niko 'fea' na 'ofkoz' sina shida na mtu. Ila ikitokea ukanichukulia tofauti na nilivo basi nakukata lisehem chako kwenye maisha yangu.

Najitahidi nirudishe hasira kidogo ili nipate reaction ya kawaida niishi na watu vizuri nashindwa.

Ndugu zangu, natamani sana kukasirika tena. Nina madonda ya tumbo sugu kwa ajili ya kunyamaza mambo yangu kwa muda mrefu, nakaa na maudhi siku zote bila kumlaum mtu wala kujadiliana nae. Nateseka mno.

Sijui kama mnanielewa, ila napitia wakati mgumu sana.

Anyway. Niwatakoe majukumu mema.
Bana weee kaa ivoivo!! kwani watu wa nini???? sanasana watakuja kukuibia mkeo tu!! watu hawana maana ila unacho niudhi hayo mawazo yanayokuletea madonda....watu wengine mizigo tu!! wachawi, watakuletea ukimwi maksudi! mpaka utamani hali yako ya ukimya!

wote piga chini kama huwajui vile!! anza moja!
 
Bana weee kaa ivoivo!! kwani watu wa nini???? sanasana watakuja kukuibia mkeo tu!! watu hawana maana ila unacho niudhi hayo mawazo yanayokuletea madonda....watu wengine mizigo tu!! wachawi, watakuletea ukimwi maksudi! mpaka utamani hali yako ya ukimya!

wote piga chini kama huwajui vile!! anza moja!
Asante
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom