mtoto mdogo sana
JF-Expert Member
- Apr 16, 2020
- 476
- 1,446
Habari wana jamvi.
Bila shaka hamjambo, mimi pia sijambo.
Bila longolongo nyingi, naenda kwenye mada.
Nadhani mimi ni kati ya watu waliowahi kupata maswaibu makubwa kwenye maisha na hii nadhani imepelekea kujenga usugu wa hali ya juu. Na wakati fulani hata mimi nilikuwa sijiamini, yaani najitilia mashaka mwenyewe.
Kuna muda nilikuwa nikifikiri hivi je nafaa kuaminiwa?
Au je ni salama mimi kupewq dhamana ya jambo? Ila mwisho wa siku nikaanza kujifunza kuishi na watu mwisho nikaweza.
Anyway nisitoke nje ya mada. Zamani utotoni nilikuwa ni mtoto mtukutu mwenye hasira za kuua, hali iliyonipelekea kutopata hata marafiki wa kucheza nao. Nilikuwa siwezi kabisa kuvumilia kuudhiwa. Nilikuwa napigana mpaka ninayepigana nae ashindwe kurudisha.
Ilikuwa nikishiriki mchezo wa mpira wa miguu, basi akijichanganya mtu akanichezea vibaya 'rafu' basi keaho lazima atatembelea magongo na POP nyingi.
Nadhani kwa sababu sikuwa na uangalizi wowote na nilikuwa sina ninayemuogopa. Ilikuwa hata mwalimu akinizingua, basi namlia 'timing' anakula virungu na kesho yake atatembelea magongo
Ilifika wakati nikawa naogopwa hata na watu wazima. Nishapigwa lockup mara nyingi sana utotoni. Sema sio lockup ile
nilikuwa nafungiwa kwenye ofisi ya mtendaji wa kata. Mpaka siku tatu. Kwa kuwa sikuwa na mtu wa kuniletea chakula basi wananichimba mkwara wananiachilia.
Shule nilikuwa na akili kupita kiasi, yaani nilikuwa mpaka naboa, kuna darasa moja nilirushwa (hii sio stori ya leo) basi nilikuwa nashauriwa sana, ila nikikasirika, basi ushauri woote nausahau. Ni vita tu.
Ilikuwa sio inshu kubwa mimi kumpiga mtu tofali, wala nilikuwa sina ile hali ya kusita. Sijui kama mnanielewa ila nilikuwa mnyama hasa.
Nikawa sipati wa kucheza nae mpira wa miguu, sipati watoto wa kwenda nao kucheza michezo ya kitoto n.k.
Basi nachokumbuka nilijikuta mimi ni jasiri kupita maelezo, naenda mapori makubwa narudi na sungura, kware, mayai mbalimbali, na sometime niliwahi kurudi na nungunungu peke yangu.
Akinizingua tu mtu, nakiwasha.. basi nikatengwa mazima na watu wa rika langu. Nilioweza kuongea nao ni wazee sana kwnye vijiwe vya kucheza bao, pamoja na askari polisi. Hao ndio nilikuwa siingii nao vita. Anywai nikatokea kuwa mtoto mdogo mwenye uwezo mkubwa sana wa kucheza bao (mpaka leo)
Basi tu cut the story short, niliqnza kujifunza kucontrol hasira zangu, kwa kipindi kirefu zaidi nikajimudu kuzuia hasira mpaka nikaweza kuendelea na masomo, nikahitimu masomo, mpaka nikawa zezeta kabisa
nikawa siwezi kuhoji hata napokashfiwa, ninapptukanwa sijibu chochote. Unaambiwa mpaka leo kuna wakati nadhulumiwa haki ila natabasamu tu na maisha yanaendelea.
Nimeanza kushtuka siku hizi naona sasa watu wananipanda sanankichwani kwa kuwa wanajua sina madhara kabisa, wananidhulumu, wanatukana, wanasingizia, wanafanya chochote ilimradi wanaamini mimi ni 'zombitype'.
Kimsingi, hata nikisingiziwa jambo huwa siwezi kujitetea kabisa. Najikuta tu nanyamaza namsikiliza mtu na madai yake na hatimaye hukumu yake. Najikuta jibu la haraka nilonalo ni OKAY, au wakati mwingine kufuata maelekezo bila kuhoji zaidi.
Hali hii ya kuzuia hasira kwa muda mrefu, imenipelekea kupata mdonda ya tumbo kwa kuwa pamoja na kutolitoa fukuto la hasira
Anyway, nitaimalizia stori baadae. Ngoja kwanza nile

Bila shaka hamjambo, mimi pia sijambo.
Bila longolongo nyingi, naenda kwenye mada.
Nadhani mimi ni kati ya watu waliowahi kupata maswaibu makubwa kwenye maisha na hii nadhani imepelekea kujenga usugu wa hali ya juu. Na wakati fulani hata mimi nilikuwa sijiamini, yaani najitilia mashaka mwenyewe.
Kuna muda nilikuwa nikifikiri hivi je nafaa kuaminiwa?

Au je ni salama mimi kupewq dhamana ya jambo? Ila mwisho wa siku nikaanza kujifunza kuishi na watu mwisho nikaweza.Anyway nisitoke nje ya mada. Zamani utotoni nilikuwa ni mtoto mtukutu mwenye hasira za kuua, hali iliyonipelekea kutopata hata marafiki wa kucheza nao. Nilikuwa siwezi kabisa kuvumilia kuudhiwa. Nilikuwa napigana mpaka ninayepigana nae ashindwe kurudisha.
Ilikuwa nikishiriki mchezo wa mpira wa miguu, basi akijichanganya mtu akanichezea vibaya 'rafu' basi keaho lazima atatembelea magongo na POP nyingi.
Nadhani kwa sababu sikuwa na uangalizi wowote na nilikuwa sina ninayemuogopa. Ilikuwa hata mwalimu akinizingua, basi namlia 'timing' anakula virungu na kesho yake atatembelea magongo
Ilifika wakati nikawa naogopwa hata na watu wazima. Nishapigwa lockup mara nyingi sana utotoni. Sema sio lockup ile

nilikuwa nafungiwa kwenye ofisi ya mtendaji wa kata. Mpaka siku tatu. Kwa kuwa sikuwa na mtu wa kuniletea chakula basi wananichimba mkwara wananiachilia.Shule nilikuwa na akili kupita kiasi, yaani nilikuwa mpaka naboa, kuna darasa moja nilirushwa (hii sio stori ya leo) basi nilikuwa nashauriwa sana, ila nikikasirika, basi ushauri woote nausahau. Ni vita tu.
Ilikuwa sio inshu kubwa mimi kumpiga mtu tofali, wala nilikuwa sina ile hali ya kusita. Sijui kama mnanielewa ila nilikuwa mnyama hasa.
Nikawa sipati wa kucheza nae mpira wa miguu, sipati watoto wa kwenda nao kucheza michezo ya kitoto n.k.
Basi nachokumbuka nilijikuta mimi ni jasiri kupita maelezo, naenda mapori makubwa narudi na sungura, kware, mayai mbalimbali, na sometime niliwahi kurudi na nungunungu peke yangu.
Akinizingua tu mtu, nakiwasha.. basi nikatengwa mazima na watu wa rika langu. Nilioweza kuongea nao ni wazee sana kwnye vijiwe vya kucheza bao, pamoja na askari polisi. Hao ndio nilikuwa siingii nao vita. Anywai nikatokea kuwa mtoto mdogo mwenye uwezo mkubwa sana wa kucheza bao (mpaka leo)
Basi tu cut the story short, niliqnza kujifunza kucontrol hasira zangu, kwa kipindi kirefu zaidi nikajimudu kuzuia hasira mpaka nikaweza kuendelea na masomo, nikahitimu masomo, mpaka nikawa zezeta kabisa
nikawa siwezi kuhoji hata napokashfiwa, ninapptukanwa sijibu chochote. Unaambiwa mpaka leo kuna wakati nadhulumiwa haki ila natabasamu tu na maisha yanaendelea.Nimeanza kushtuka siku hizi naona sasa watu wananipanda sanankichwani kwa kuwa wanajua sina madhara kabisa, wananidhulumu, wanatukana, wanasingizia, wanafanya chochote ilimradi wanaamini mimi ni 'zombitype'.