kindikwili
JF-Expert Member
- Oct 5, 2016
- 1,862
- 2,876
Sitaki kueleza mambo mengi hapa ila kwa nia njema kabisa, kwa moyo mkunjufu wa kizalendo naomba niwaombe NACTE watoke ofisini watembelee hivi vyuo vya kati na ikibidi waongee na wanachuo bila uwepo wa uongozi wa vyuo hivyo. Pili wafanye utafiti wa siri kujua kiundani mambo yanayofanyika ndani ya hivyo vyuo vyetu vya kati huku TCU ikifanya kwa vyuo vikuu.
Nina mifano michache na nitaitoa hapa , mfano mwanafunzi anajisajiliwa (anadahiliwa) chuo kusoma ngazi ya cheti (certificate)tena chuo hupeleka vyeti vyao NACTE kukaguliwa kama kweli wanasthili kudahiliwa lakini baada ya muhula wa kwanza na wa pili anafaulu baadaye anapotaka kujiunga diploma anaambiwa NACTE hawamtambui kwasababu hana vigezo wakati kipindi chote alikuwa anatoa ada na kumbuka wakati wa usajili kuna pesa kwa ajili ya NACTE.
Mwanafunzi anafanya mitihani anafaulu vizuri baada ya muda anaambiwa aje afanye supplementary kwa madai kwamba NACTE wamebadili mfumo wa alama , hii ni kwamba NACTE wanatoa maagizo lakini vyuo huchelewa kuyafanyia kazi matokeao yake ni hayo. Hebu piga picha kwa mwanafunzi anayekaa mbali garama hizo za kuja kufanya supplementary nani atazilipa na je ikitokea mwanafunzi akashindwa kusapua atadisco au ndiyo sasa mtihani hutungwa usio na tija ili wanafunzi wafaulu wote kuua soo.
Vyuo vya NACTE wanafunzi wanajiunga muda wowote kabla ya mtihani wa semister as long as atalipa ada, vyuo vingine wazazi huadaiwa kwamba watoto wao watapigwa brush ili waendane na wenzao ambao ni utapeli mkubwa . Hivi vyuo vinajali pesa kuliko elimu na hii ipo hadi kwa vyuo vya umma
Vyuo vingine hutoza wanafunzi shilling elfu hamsini kwa ajili ya bima ya afya na hii ni non refundable lakini mwanafunzi akienda hospitalini anaambiwa kiwango hicho hakitoshi mtu kutibiwa bure, sasa kama hiyo hela haitoshi kwa bima kwanini itozwe kwa wanafunzi?
Waalimu wengi wa vyuo hivi wanafundisha kwa kiswahili masomo yote, wachache huelezea kwa kingeereza lakini wengine husoma sentensi kwa kiingereza huku maelezo menginine yakiwa kwa kiswahili, situkuzi kiingereza lakini kwasasa nchi imekubaliana kuwa English ndiyo lugha ya kufundishia. Hii hali ipo secondary hadi vyuoni
Ili kuwapata wananfunzi wa kike kirahisi , waalimu wengi wa vyuo hivi huwataka wanafunzi kufanya presentation ofisini, humo ndani anapata muda kutongoza na kuweka mambo sawa. Hivi kwanini mwalimu awapangishe watoto foleni nje ya ofisi yake ili wafanye presentation ilihali madarasa yapo?
Upangaji wa ratiba katika vyuo hivi unaweza kuchua wiki mbili au tatu na kwa wakati wote huo masomo yanasuasua kwa vipindi kugongana lakini muda huo huhesabika kama muda wa kusoma matokeo yake wanafunzi wanapelekeshwa bila kuelewa vitu kwa undani ili kufidia muda.
Watu wa idara ya mitihani wanapaswa kuangaliwa kwa macho yote maana mwanafunzi anaweza kupata kwa mfano A,C,C,C C, kwa masomo matano kwa mafuatano huo lakini wakati wa matokeo yanapelekwa NACTE kwa ajili ya ku print cheti kwa vile mwalimu hahusishwi wala booklet zake haziko pale watu wasio waaminifu wa idara ya mitihani wanaweza kupewa pesa na kubadili matokeo maana wana access ya system. (Hii inaweza fanyika popote ikiwa control mechanism siyo kubwa nimeiona ndiyo maana nimeisema hapa)
Sijataka kutaja vyuo kwa majina yao bali nimeandika general sana ili NACTE ifanye kazi yake. Ili kuboresha elimu ya nchi hii wasimamizi wa taaluma hawatakiwi kufanya kazi maofisini kila wakati watoke nje wakutane na wanafunzi na wadau kupata uhalisia wa mambo. Wakati ujao nitataja vyuo kadhaa na madudu yake ila kwa leo itoshe kusema haya .
Wadau si vyuo vyote vilivyo chini ya NACTE vina madudu haya ila vingi
Wapendwa wadau wa elimu hebu tusaidie taifa hili kwa kueleza madudu ya elimu yetu ,mimi leo nimeanza na hivi ila kadri siku zinavyokwenda nitakuja na mengine mengi zaidi.
Mzalendo wa nchi yake
kindi (a.ka. Kangomba) -Masasi Mtwara