NACTE Mmebadilisha viwango kwa Wanaoomba Elimu ya Juu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

NACTE Mmebadilisha viwango kwa Wanaoomba Elimu ya Juu?

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by mmaroroi, Aug 6, 2009.

 1. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #1
  Aug 6, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Wadau tufafanulie kuhusu hili.Sifa inayojulikana kwa wanaoomba Elimu ya juu ni Kidato cha Sita,Kidato cha Nne na Stashahada ya B grade.Lakini kuna Watu niliosoma nao wamepitishwa na NACTE kwa Elimu ya juu wakiwa na Kidato cha Nne na Stashahada ya C PASS.Tueleni kama viwango vimebadilika tuchukue fomu kwa kuwa mwanzo tulisita kwa kufuata matangazo ya Vyuo husika.Wana JF wenye ufahamu wa hili na NACTE mtuelimishe.
   
 2. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #2
  Aug 6, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Tuelezeni kama viwango vimebadilika tuchukue fomu kwa kuwa mwanzo tulisita kwa kufuata matangazo ya Vyuo husika.Wana JF wenye ufahamu wa hili na NACTE mtuelimishe.
   
 3. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #3
  Aug 6, 2009
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Kabla sijakusaidia ufafanuzi, naomba kujua wewe una sifa gani kati ya hizo ulizotutajia.

  Vinginevyo itakuwa vigumu kukupatia msaada utakaokufaa.

  Kwasababu mtu wa kidato cha sita, mwenye mchundo (FTC) na mwenye diploma wanatofautiana alama za kujiunga na elimu ya juu,

  wewe uko kundi gani?
   
 4. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #4
  Aug 10, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mimi ni Kidato cha Nne na Stashahada ya daraja C (PASS)
   
 5. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #5
  Aug 10, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,868
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Aibu!

  Bosi wa NACTE nani??

  Hebu weka majina walipendelewa hapa!!

  Are we for quality or quantity or both??
   
 6. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #6
  Aug 10, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Ngoja niorodheshe majina maana ndio sababu nawaamini TCU kuliko NACTE kwa umakini wa Selection.Wengine pia waorodheshe wanaowafahamu ili tukomeshe udanganyifu kitaaluma.
   
Loading...