NACTE: IFM, CBE na Arusha Tech siyo Vyuo Vikuu bali ni Taasisi za Elimu

Lakini ipo 10 bora ya vyuo vikuu duniani. Na kupata nafasi lazima uwe kipanga kweli kweli
Tazama rankings ya vyuo vikuu bora duniani.

Utakutana na MIT, California institute of technology, Georgia institute of technology.

Hapo huwa sielewi kwa nini wanaingiza taasisi ziwemo katika 10 bora ya vyuo vikuu duniani
MIT = Mbeya Institute of Technology; zamani Mbeya Tech.
 
Tuekezeni sifa ya chuo kuitwa chuokikuu na sionkushindana kama hamjaenda shule ya kutosha kufanya mijadala.
Vyuo vikuu vyote ni sehemu ya taasisi za elimu ya juu.
Si taasisi zote za elimu ya juu ni vyuo vikuu
 
Hata Mimi nilikuwa nashangaa sana. Taasisi nyigi hata qualifications za lecturers ni questionable! Mwenye Bachelor anamfundisha anayechukua Bachelor! Ghafla bin vuu mara mtu huyohuyo ana Masters!
Hii ipo sana kwa wanaojiendeleza wakiwa kazini. Na consequences zake ni utendaji hafifu sana.
 
Ilitakiwa atuelezee sifa na tofauti kati ya chuo kikuu na Taasisi ya elimu

Sidhani kama Kuna tofauti ya kiubora maana ametoa mfano wa Taasisi inayotoa cheti mpaka masters so naona bado hajaeleweka naona ameeleza kiushabiki zaidi kuliko uhalisia
Utofauti ni majina tu kaka.
College,Institute VS University.
 
Mwenye Bachelor anakuwa Tutorial Assistant,Mwenye Masters anakuwa Assistant Lecturer,Mwenye Phd ni Lecturer mbona hakuna tatizo hapo.
 
Huyu kaka sioni neno baya kutoka kwake, maneno yake yanatokana na maswali aliyoulizwa na host wake, ni kweli kabisa Hivo sio universities, DIT, TIA, IFM ni institutions moja inahusika na technology and engineering nyingine inahusika na uhasibu na nyingine ina deal na finance. CBE ni collage inayohusiana na elimu ya biashara. University inaweza kuwa na colleges,schools and institutions ndani ake but vice versa is not true na haiwezekani mfano udsm ni university ndani yake kuna Coet na Conas hizi ni college, na pia kuna IKS(institute of kiswahili studies) mfano mwingne ni muhimbili university yenyew ndani yake kuna schools e.g school of medicine ila huwez kuta IFM au CBE ina colleges au institutions ndani yake, zenyewe zina department tuu,ila degree vinatoa na masters pia. Brethren, nnachoshangaa kwa Tanzania institute kama IFM inayohusiana na finance inatoa degree ya computer science au kama CBE inatoa degree za kisayansi kama metrology and standardization
 
Ukienda kwenye Interview HRs hawaangalii umesoma University au Institute. Wanaangalia Capability yako.. sasa wewe kaa hapo chuoni uvimbe kichwa kuwa upo University na sio Institute. Utaishia kujisifia kwenye vilabu vya pombe kijijini kwenu
 
Halaf mim kuna siku nilijiulizaga hili swali
Ifm na comp sci wapi na wapiπŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„
Itakua bodi imekaa ikaona itafute vyanzo vingine vya mapato πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„
 
Ngoma Nzito Yaani Wataandamana Muda Huu
Vipo Vingi Sana Vyuo Vya Utumishi Magogoni Mtwara Tanga Mbeya Singida Na Tabora

Huyu Mwamba Anachafua Hali
Kaamua kueleza ukweli na hali halisi. Kuna nyakati ukweli huwa mchungu kukubalika.
 
Lower second, Pass!!!? Ridiculous!!
Uwezo na marks ni vitu viwili tofauti.
Kuna watu mimi nilisoma nao walikuwa wanapiga GPA za 4.5 kila semister,lakini baada ya kuingia mtaani wanashindwa kujieleza kwenye interview hata kazi za wahindi zinawapiga chenga na sisi wenye lower second tunabadilisha makampuni kila mwaka.
 
Ukienda kwenye Interview HRs hawaangalii umesoma University au Institute. Wanaangalia Capability yako.. sasa wewe kaa hapo chuoni uvimbe kichwa kuwa upo University na sio Institute. Utaishia kujisifia kwenye vilabu vya pombe kijijini kwenu
wanasemaga ukishamaliza chuo bango la chuo unaliacha getini unarudi mtaani na kichwa chako kupambana.
Hili wengi hawalijui wanashabikia majina ya chuo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…