Nacheka - kicheko cha uchungu!

Nacheka - kicheko cha uchungu!

Setfree

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2024
Posts
5,527
Reaction score
7,121
Mfalme ameandaa sherehe kubwa ya arusi. Amewaalika watu wote bila upendeleo. Lakini ajabu, wote walioalikwa wamekataa mwaliko!

Huyu anasema: "Samahani, naenda kuzika." Yule anasema: "Lazima niende shambani, nimeanza kupanda mbegu." Mwingine amejibu: "Naomba unielewe, nimeoa hivi majuzi!" Wote wana visingizio!

Wahubiri ni wengi mitaani, masokoni, kwenye redio na TV, na kwenye mitandao. Wanapaza sauti kwamba Yesu yuaja kuwachukua watakaokubali mwaliko wake. Atawachukua waende kula vinono kwenye sherehe hiyo ya arusi!

Nacheka kwa uchungu kwa sababu sauti za wahubiri hao zinajibiwa kwa kejeli:
"Ah, hao wahubiri wamechanganyikiwa kabisa! Wafungwe kamba wapelekwe Mirembe!" "Wamekosa kazi ndiyo maana wanatisha watu na moto wa milele!" "Wanapiga makelele tu, dunia haiishi!"

Magari ya abiria yanasafiri kutoka mkoa mmoja hadi mwingine huku yakipiga nyimbo za mwaliko wa arusi. Nacheka kwa uchungu kwa sababu abiria waliomo ndani ya magari hayo hawazitaki nyimbo hizo. Wanamshauri konda aweke movie za mapenzi. Na wengine wameweka headphones masikioni wanasikiliza bongofleva kwenye simu zao, huku wakirushiana picha za aibu TikTok na kugombania mademu Facebook!

Nacheka – si kwa dhihaka, bali kwa uchungu, nikiwaangalia watu wengi wanavyoenda motoni. Wanapita njia pana huku wameinua glasi za pombe wakimnyanyapaa Bwana wa uzima. Nawasikia wakishangilia, lakini punde sauti zao zitageuka kuwa za kilio na kusaga meno.

Nacheka kwa uchungu kwa sababu siku ya hukumu inakuja. Waliozoea kukata rufaa, siku hiyo hakuna nafasi ya kukata rufaa.

Watu watakumbuka zile video walizo-skip YouTube kwa sababu zilikuwa za mahubiri badala ya comedy. Watakumbuka nyuzi alizoandika Setfree waka-comment "ana tatizo la afya ya akili."

Ndugu yangu, usifanye mzaha na wokovu. Furaha yako ya leo isije kuwa kilio cha milele. Tubu leo kwa kuwa ufalme wa Mungu umekaribia. Tubu leo uwe miongoni mwao watakaoshiriki karamu(sherehe) kubwa, isiyo na mfano, aliyoiandaa Bwana Yesu. Ukikubali kuokoka leo, nitacheka kicheko cha furaha. Mungu akubariki.
 
Mada hii imetokana na vifungu vifuatavyo:

Karamu ya Arusi na Mwaliko wa Yesu
Mathayo 22:2-5
"Ufalme wa mbinguni umefanana na mfalme aliyemfanyia mwanawe arusi. Akawatuma watumishi wake kuwaita waliokuwa wamealikwa arusini, lakini hawakutaka kuja... Lakini wale walioalikwa hawakujali, wakaenda zao, huyu shambani kwake, huyu katika biashara yake..."

Ufunuo 19:7-9
"Na tufurahi, tushangilie, na kumpa utukufu wake; kwa kuwa arusi ya Mwana-Kondoo imekuja, na mkewe amejiweka tayari... Heri wale walioalikwa kwenye karamu ya arusi ya Mwana-Kondoo."

Visingizio vya walioalikwa karamuni
Luka 14:16-20
"Mtu mmoja alifanya karamu kuu, akawaalika wengi. Wakaanza kuomba radhi wote kwa kauli moja... mmoja alisema, ‘Nimenunua shamba’; mwingine, ‘Nimenunua ng’ombe’; mwingine, ‘Nimeoa, siwezi kuja.’”

Kejeli dhidi ya wahubiri wa kweli
2 Petro 3:3-4
"Katika siku za mwisho watakuja watu wenye kudhihaki, waendao kwa tamaa zao wenyewe, wakisema: ‘Iko wapi ahadi ya kuja kwake?’”

1 Wakorintho 1:18
"Kwa maana neno la msalaba kwao wanaopotea ni upuzi, bali kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu."

Njia pana na giza nene
Mathayo 7:13-14
"Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana, na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo. Bali mlango ni mwembamba, na njia imebana iendayo uzimani, nao waionao ni wachache."

Yuda 1:18-19
"Waliwaambieni: Siku za mwisho, watatokea watu watakaowadhihaki nyinyi, watu wafuatao tamaa zao mbaya."

Furaha ya sasa katika anasa za dhambi itakuwa kilio cha baadaye
Luka 6:25
"Ole wenu ninyi mnaocheka sasa, kwa kuwa mtahuzunika na kulia."

Yakobo 4:8-9
"Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu, enyi wenye nia mbili."

Siku ya hukumu haina rufaa
Waebrania 9:27
"Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya hapo hukumu."

Mwaliko wa kutubu sasa
Marko 1:15
"...Wakati umetimia, na ufalme wa Mungu umekaribia; tubuni, na kuiamini Injili.."

2 Wakorintho 6:2
"Tazama, sasa ni wakati unaokubalika; tazama, sasa ndiyo siku ya wokovu."

Ukikubali kuokoka leo, nitacheka kicheko cha furaha.
Luka 15:10
"Nawaambia, vivyo hivyo, kuna furaha mbele za malaika wa Mungu kwa mwenye dhambi mmoja atubuye."
 
Nilishangaa ulipo tuaga humu nikajua umeshinda addiction ya JF, kumbe bado uko nasi.
 
Mfalme ameandaa sherehe kubwa ya arusi. Amewaalika watu wote bila upendeleo. Lakini ajabu, wote walioalikwa wamekataa mwaliko!

Huyu anasema: "Samahani, naenda kuzika." Yule anasema: "Lazima niende shambani, nimeanza kupanda mbegu." Mwingine amejibu: "Naomba unielewe, nimeoa hivi majuzi!" Wote wana visingizio!

Wahubiri ni wengi mitaani, masokoni, kwenye redio na TV, na kwenye mitandao. Wanapaza sauti kwamba Yesu yuaja kuwachukua watakaokubali mwaliko wake. Atawachukua waende kula vinono kwenye sherehe hiyo ya arusi!

Nacheka kwa uchungu kwa sababu sauti za wahubiri hao zinajibiwa kwa kejeli:
"Ah, hao wahubiri wamechanganyikiwa kabisa! Wafungwe kamba wapelekwe Mirembe!" "Wamekosa kazi ndiyo maana wanatisha watu na moto wa milele!" "Wanapiga makelele tu, dunia haiishi!"

Magari ya abiria yanasafiri kutoka mkoa mmoja hadi mwingine huku yakipiga nyimbo za mwaliko wa arusi. Nacheka kwa uchungu kwa sababu abiria waliomo ndani ya magari hayo hawazitaki nyimbo hizo. Wanamshauri konda aweke movie za mapenzi. Na wengine wameweka headphones masikioni wanasikiliza bongofleva kwenye simu zao, huku wakirushiana picha za aibu TikTok na kugombania mademu Facebook!

Nacheka – si kwa dhihaka, bali kwa uchungu, nikiwaangalia watu wengi wanavyoenda motoni. Wanapita njia pana huku wameinua glasi za pombe wakimnyanyapaa Bwana wa uzima. Nawasikia wakishangilia, lakini punde sauti zao zitageuka kuwa za kilio na kusaga meno.

Nacheka kwa uchungu kwa sababu siku ya hukumu inakuja. Waliozoea kukata rufaa, siku hiyo hakuna nafasi ya kukata rufaa.

Watu watakumbuka zile video walizo-skip YouTube kwa sababu zilikuwa za mahubiri badala ya comedy. Watakumbuka nyuzi alizoandika Setfree waka-comment "ana tatizo la afya ya akili."

Ndugu yangu, usifanye mzaha na wokovu. Furaha yako ya leo isije kuwa kilio cha milele. Tubu leo kwa kuwa ufalme wa Mungu umekaribia. Tubu leo uwe miongoni mwao watakaoshiriki karamu(sherehe) kubwa, isiyo na mfano, aliyoiandaa Bwana Yesu. Ukikubali kuokoka leo, nitacheka kicheko cha furaha. Mungu akubariki.
Inafikirisha
 
Hatuzingatii tu lakini jehanamu na Mbingu vipo MUNGU Aturehemu sisi vijana
 
Hell and Heaven it's all in your brain..
The world is M.I.N.D
Kataa uongo wa shetani. Shetani alikuwa mbinguni na anajua uzuri wa huko. Yeye ameishahukumiwa kwenda motoni. Anatuonea wivu sisi kwakuwa Yesu anatuandalia makao mbinguni. Shetani anataka tuangamie pamoja naye ndo sababu anawashawishi watu wasiamini. Mkatae shetani kwa Jina la Yesu.
 
Nilisema "kwaherini" sikusema "buriani"
Hahaha JF ina urahibu wake, usiage kwa vyovyote maana unaweza kurudi ndani ya dakika chache baada ya kuaga.

Wachache wameweza kuondoka JF jumla.

Binafsi huwa nafikiria sana kuondoka jumla nashindwa, nimeweza kwingine.
 
Back
Top Bottom