Nachanganyikiwa nikisikia tutapata 3% ya faida ya madini

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
21,316
50,523
Wataalam Wa mambo ya siasa za uchumi hivi nini kilisababisha serikali zilizopita kushindwa kusimamia angalau asilimia 50 kama murahabu.

Na je rais wetu magufuli akiamua kubadilisha na kuvunja Ile mikataba ya awamu zilizopita.

MFANO tanzanite inauzwa ya billion nane AFU serikali inajisifia kuingia million 300.

Mimi naamini upinzani ungeingia ungeweza kubadilisha kabisa hizi sera za kinyonyaji.

Na kwanini Kuna hii serikali kitu na je upinzani wakiingia ndio kwamba hizi sera watazibadilisha?

Mitambo ya kuchimba madini ni bei Gani kiasi kwamba serikali is ifanye biashara na yenyewe IKEA na ma kampuni yake.

Uchumi WA nchi utakuwa mkubwa zaidi. Kwanini tusiuze madini direct.
 
Wapinzani sini kila siku wanawakumbatia imperialists wanaenda ulaya kufanya nao mikutano?kama wapinzani wanaomba misaada kwa imperialists na kufuatisha Sera zao sasa ndio unataka kuamini wakichukua nchi watabadilisha?? Ondoa fikra hiyo kichwani

Ukishawapa ardhi yako imperialists sahau kabisa unawatajirisha wao

The late Hugo Chavez pekee mpaka anakufa hakuwapa ardhi yake imperialists ,mafuta yaliyopo Venezuela alikataa USA aguse
Akiamini atakuwa anamtajirisha USA kwa Mali asili yake, nadhani tumeona namna USA walivyomuwekea vikwazo,kusponsor mapinduzi ya kumuondoa nk

Gaddafi alipinga sana unyonyaji huo nadhani tumeona alivyofanywa

Ukishakubali Sera za imperialists za kinyonyaji basi ardhi siyo yako ,migodi yote ni Mali ya world bank na IMF ,ukivunja hutokuwa salama kwanza utawekewa vikwazo,figisu figisu na utaondolewa madarakani nk

Afrika ni wahanga wakubwa sana ardhi yao lakini wana watajirisha imperialists ndio madhara yakutoa ardhi hovyo na Fidel aliwahi sema wanasema ujamaa umefeli ni yapi faida za capitalism Africa ,je unaweza kuanzisha bifu na IMF ,world bank?

Kama unafuata Sera zao basi wasikilize wao wanaamua nini na wanataka nii...madini,ardhi yapo kwenu lakini siyo zenu hebu tender zote wape urusi,China halafu uone kitatokea nini?

Usilalamikie mkataba ,lalamikia capitalism


Pongezi zimuendee Chavez alikataa ardhi yake iwatajirishe imperialists ,kafa kishujaa alifunga milango kwa imperialists ..socialist wa ukweli
 
Kuna mifupa mingine hata kama una majeshi yote duniani huwezi kuitafuna.

Yeye saizi yake ni kina hawa James Delicious.
 
Back
Top Bottom