Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 2,436
- 5,234
Nabii Mkuu wa Makanisa ya Ngurumo ya Upako (N.Y.U), Dkt. Moses Kasambale Geordavie, ametoa wito kwa Watanzania kuhakikisha wanatumia haki yao ya kikatiba kwa kushiriki kikamilifu katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 kwa kuwachagua viongozi wa nafasi za Udiwani, Ubunge na Urais.
Dkt. Geordavie ametoa wito huo leo, Jumamosi Julai 5, 2025, jijini Dodoma, wakati wa hafla ya kutunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari katika masuala ya Uongozi na Huduma za Jamii pamoja na tuzo maalum kutoka Umoja wa Madaktari wa Falsafa na Maprofesa Tanzania (APDPT).
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Nabii Dkt. Geordavie amesisitiza kuwa kila Mtanzania ana haki ya kikatiba ya kuchagua au kuchaguliwa, hivyo ni muhimu kuitumia fursa hiyo kwa ajili ya maendeleo ya taifa.
Aidha, ametoa pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kazi kubwa anayoifanya kuongoza nchi, na kuwataka viongozi wa dini kuendelea kumuombea pamoja na Serikali anayoiongoza.