Naangamia nahisi kukata tamaa

Naangamia nahisi kukata tamaa

Nilipata kazi 2020 kwenye kampuni X maarufu sana hapa Tz nashukuru Mola mambo yangu yalinyooka saaana vijisent vidogo vidogo havikuwa vikwazo tena kwangu

Ghafla mwaka jana 2022 mwezi wa 12 nikasimamishwa kazi kwa kosa ambalo mpaka na leo sielewi bado nikatapeliwa milion 1.4 na kampuni yangu huku mikosi inaniandama nikipata pesa hazikai kila lolote nifanyalo halifanikiwi.

Kuna siku nilishawahi kukuta mbegu 3 juu ya mlango sebuleni kibaya zaidi nina ndugu zangu ambao nimeshare nao baba hawapendi kuniona ninafanikiwa hasa huyu mmoja ndio nilikuwa nakaa nae jirani ni kaka angu yeye ni askari polisi lkn kajawa na chuki na wivu siku zote hawa ndugu zangu wanapenda mimi niwe wakuteseka tu.

Ila kila mtu alikuwa na familia yake na mji wake ila sasa hivi kahamia kota za Barracks toka mwaka jana mwezi wa 4 lkn jamaa huyu haachi kunisemea ubaya kwa watu na kudai mm mzee wetu ananipendelea sana kuliko wao ila kiuhalisia haipo hivyo ni chuki tu zimemtawala na tumekua wote toka wadogo nafahamu tabia zao za chuki na alivyohama hakuwahi kuniaga yeye hata mkewe ilifika kipindi hata mtoto wao alishawahi kusema "mama amenikataza nisije kwa baba mdogo" tena akiwa na mama yake mm na mke wangu tukaishia kucheka tu na kupotezea

Mara nyingi ndugu yangu nishawahi kumchana tabia yake ya chuki na roho mbaya anaeza kumpigia simu mama yake jamaa akaongea uongo uongo juu yangu hata mama yake pia hanipendi japo kanilea lkn ni mtu aliyekuwa na chuki na mimi za kimya kimya na mm hilo nalifahamu sana.

NIFANYAJE HAPO KUJIKWAMUA KWA MAANA NAHISI KAMA KUNA MCHEZO NINAOFANYIWA AMBAPO SIELEWI MAMBO YANGU YANAFELI GHAFLA PESA SIZIONI NA NIKIPATA HAZIKAI NIKIENDA KUFANYA INTERVIEW ZA KAZI NAONA MATUMAINI KABISA LKN SIITWI WALA MREJESHO WOWOTE

SIJUI NIFANYE NINI HAPO AKILI YANGU IMEKOSA KUFIKIRI ZAIDI BADO FAMILIA INANIANGALIA MAMBO YAMEYUMBA SANA MPAKA SASA NAANZA KUUZA VITU VYA NDANI ILI NIPATE KULISHA MKE NA MTOTO WANGU
Hata kama ni ndugu zako. Jitenganishe nao ili kuepusha gharama za kujitibia tibia na kusaka muujiza kila siku
 
Amka kila.sku saa Tisa soma zaburi ya 27 afu piga maombia ya Toba na shida zako.

Saa Tisa mchana hvo hvo. Haijalishi we ni muislam shika Biblia soma..kwa Mwaposa wamejaa akina halima ,Salim ,Abdul sembuse ww

Mambo yakianza kunyooka tuma sadaka yako niendelee kupata ka whisky
 
Amka kila.sku saa Tisa soma zaburi ya 27 afu piga maombia ya Toba na shida zako.

Saa Tisa mchana hvo hvo. Haijalishi we ni muislam shika Biblia soma..kwa Mwaposa wamejaa akina halima ,Salim ,Abdul sembuse ww

Mambo yakianza kunyooka tuma sadaka yako niendelee kupata ka whisky

shukran mzee shirimaa
 
Back
Top Bottom