Naangamia nahisi kukata tamaa

Mm siku izi nachukia kazi za kuajiriwa..... Sizipendi Kaz za laki 2 na nusu mpk 1m labda kama ni kwame kabisa...

Nakushaur Kwa Imani yako NENDA KWA MWAMPOSA
Napenda sana kuajiriwa aise tuko tofauti sana japo ninabiashara yangu inaniingizia kipato cha uhakika lkn natamani tu kuajiriwaa cjui ninapepo gani linanisumbua
 
KATAA NDOA
NDOA NI UTAPELI
NDOA NI WIZI
NDOA NI NDOANO
NDOA INALETA YOTE HAYA.
 
Hakuna mtu anaweza kukufanya chochote mkuu usije ingiza waganga ndio utaisha kabisa...kwenye Maisha acha kuamini uchawi utasonga mbele hata dini usiegemee sana nenda Sali lala mbele mambo ya maombi yatakumalizia zaidi hela.
Jutathmini wapi unapeleka hela haziwezi isha tu...halafu hizo hela unasema unapata na hazikai ni shillingi ngapi?
 
Kuna mtu alipata kuniambia kwenye haya maisha hakuna mtu anayependa kukuona ukiwa unafanikiwa zaidi ya mama yako mzazi tu.Inafikirisha kwa kweli.
Marioo nae kaimba "kwani nikifanikiwaa nini unapungukiwa"
 

sawa mkuu
 

asante kwa ushauri
 
Huwezi kufanikiwa hadi uache kuhisi kila mtu anakuchukia, na uache kulazimisha ukaribu na watu wasio hitaji ukaribu na wewe ikiwezekana hata habari zao usiulizie waache wao ndo waulizie habari zako
 
Napenda sana kuajiriwa aise tuko tofauti sana japo ninabiashara yangu inaniingizia kipato cha uhakika lkn natamani tu kuajiriwaa cjui ninapepo gani linanisumbua
Ukiajiriawa uajiriwe sehemu nzuri sio unakua mtumwa au kijakazi...
Hata ukiwa kijakazi fanya Kwa akili Mingi ukijipanga...
 
Come on my Nigga .
Ifike mahali ujue kuwa ndugu na watu wa kujali na kuwaza juu yao ni mkeo na wanao .

Ila ukumbuke hizi imani ukiziamini basi ndiyo inakuwa shida pia so pambana ujuavyo usiwaze uwepo wa mkono wa mtu maishani mwako .
 
Pole sana kamanda hao ndio walimwengu baab. Ushapigwa nuksi yani na nyota wamezifyeka. Utahangaika kinoma bila kujipiga dodoki la kiimani. Pambana kujisafisha kiroho aidha kwa mitishamba au kwa upako sababu bila hivyo wewe ni sawa na crate tupu kwa sasa.
 
Wewe hujaROGWA ni ka msimu tu ka upepo flani hivi unakapitia sema tu hujaamua kukubaliana nako na kuamini kua utavuka na huenda hujazoea kupitia shida maisha yako mengi ila hii hali huwa ya kawaida sana inamkuta kila mwanaume katika maisha... ACHA KUAMINI MIZIMU, UGANGA, MAJINI NANI SIJUI NA UJINGA UJINGA MWINGINE WA MAMBO YA GIZA (Uchawi upo ila usiuamini sana, Imani yako ndiyo itakuokoa au kukuangamiza ni wewe kuamua kujiset sehemu sahihi sasa)....
 

1. Acha kukata Tamaa
2. Jiamini na Jikubali sana
3. Acha Kuamini Umerogwa
4. Kuwa Mbunifu wa Fursa
5. Jichanganye na Watu
6. Tathmini Mapungufu yako
7. Mtumainie Mwenyezi Mungu
 

shukran mkuu
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…