Naamini kuwa Mke anaweza patikana popote

Igembe28

Member
Dec 19, 2014
16
5
Habari zenu brothers and sisters. Wakubwa zangu, heshima kwenu pia. Mimi ni mgeni kwenye site hii. Baada ya rafiki yangu mmoja kufanikiwa kupata mke umu JF, nami nimeamua kuja katika jukwaa hili linaloheshimika ili nijaribu bahati yangu.
Wapendwa, mimi nahitaji MKE, not a mere girlfriend. Nahitaji mwanamke wa kupendana kwa dhati, kuelewana, kufurahi pamoja, kufanya maisha na kujenga familia.

Briefly kuhusu mimi:

a) Sex: MALE
b) Umri: 28 years
c) Asili & Kabila: Geita/Mwanza – msukuma
d) Makazi: Dar
e) Elimu: Diploma. (If God awards me a green-light in my endeavors, naplan kujiendeleza kielimu hapo baadae
possibly in one year to come)
f) Occupation: Employed, though kipato changu bado ni kiduchu mno. Kusema ukweli, kipato changu ni kidogo mno, and I am
extremely struggling for extra earning.
g) Dini: mkristo, nasali Lutheran church. Nina hofu ya Mungu.
h) Muonekano: Good looking and smart, mweusi kidogo, mrefu wa kati, moderate body (si mnene wala si mwembamba)
i) Marital status: Single and never married before, na sina mtoto.
j) Ni mcheshi. Ni mkweli.
k) I am always open and straight forward. I NEVER pretend life, I live my reality!

Sifa kuhusu yeye / ninayemhitaji:


1. Sex: FEMALE
2. Umri: 21 – 26
3. Dini: mkristo
4. Kabila: lolote
5. Elimu: kuanzia Form 4 or/and above
6. Occupation: Awe anafanya kazi au kujishughulisha na chochote halali kinachomuingizia kipato. (i.e. asiwe tegemezi fully)
7. Marital status: Awe single, hajawahi kuolewa, na hana mtoto.
8. Muonekano: Awe mrefu wa wastani (not short), mzuri wa sura, msafi, rangi maji ya kunde au mweupe (weupe wa asili, sio
kujichubua), umbo la kati (sio mnene na wala asiwe mwembamba saaaaana), awe na ‘shape' ya kuvutia
(flat-screens are not preferable to me kwakweli, I listen to my heart).
9. Awe mcheshi, anajua kupenda, mpole, mkarimu, mkweli, na mwenye hofu ya Mungu.
10. Awe na akili ya maisha, and serious kuanzisha familia.

N.B:
Please no jokers and pretenders. No time-wasters as well. Sipendi kumchezea mwanamke na kumpotezea muda wake coz I know the way it hurts, likewise sipendi mwanamke wa kunipotezea muda na kupeana stress. LIFE is short! So tuwe wakweli, wawazi, and we see how further we can step-up together.

As such, a lady who fits the above criteria and interested, please feel free to hit my inbox. Just shoot me a PM for more info na kufahamiana zaidi.

Otherwise, sincerely nawashukuru sana wanaJF wote kwa kusoma ukurasa huu. Pia mnisamehe sana kwa kuwachosha na gazeti, but hopefully my advert ipo self-explanatory na imejaribu kujibu maswali mengi ya kuanzia.
Mwenyezi Mungu awabariki sana, na awatangulie vyema katika sherehe hizi za mwisho wa mwaka. Merry Xmass & Happier New Year!!

JF idumu!
 
Mmmhhhhh...mchumba kwenye social networks... Puuuuuu uzushi mtipu

inamaana wote waliomo kwenye social nets ni hawafai? nina rafiki angu mmoja amepata mke umu umu JF, true story!!! tunapata best friends wa kudumu from hizi hizi social nets, why not kupata mchumba? Hakunaga formula juu ya wapi pa kumpata mwenza. popote pale watu humeet, hufahamiana na kuanzisha mahusiano.
 
Ebana kwa sifa ulizonazo mtaan kwenu ungeshapata mchumba ...maana hata hapo kuna mabinti wanahitaj ndoa..bahati ya mwenzio
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom