D Metakelfin
JF-Expert Member
- Mar 23, 2017
- 3,193
- 3,325
Naamini...........
Unahitaji kufanikiwa kwa kuwa na elimu nzuri, nyumba nzuri, gari zuri, uwe na miradi inayofanya vizuri na kukupa kipato kizuri.....
KWA UFUPI UNAHITAJI KUWA NA MAISHA BORA
SASA naomba utambue kuwa kufanikiwa sio bahati bali ni process.
Kila anayefanya jambo vizuri sio kwamba ana kipaji kuzidi wengine, ama ana elimu kubwa kupita wengine, wala sio amebarikiwa kuwapita wengine.
Bali ni kwa sababu ana shauku kubwa na anajitihada inayomfanya awe kama alivyo.
Kufanikiwa si shughuli ya siku moja bali ni zoezi la muda mrefu.
Chukulia mfano wa jinsi ulivyojifunza KUSOMA NA KUANDIKA halikuwa zoezi la wiki moja. Kumbuka ulivyosoma kwa kutamka neno au silabi moja moja na ulivyokuwa unaandika A E I O U ambazo hazielezeki hata umbo lakini leo upo vizuri.
Ni kwa kuwa ulitumia muda kufanya mazoezi hayo mpaka ukawa mzuri wa kusoma na kuandika.
Mafanikio hayajileti ungekaa ukasubiri kusoma na kuandika kujilete mbaka leo ungekuwa unaona kitabu ama gazeti kama picha tu.
LEO NDIO HUANDAA KESHOOO
Ukianza leo kufanya kidogo kidogo kile unachohitaji maishani kwa hakika mwakani utakuwa mbali.
Mfano: kama shida yako ni mtaji, ukianza sasa kwa kujikana ukasema iwe isiwe unataka kuwa unaweka hata elfu tano kila wiki baada ya mwaka sita utakuwa na mtaji wa kuanzia biashara unayohtaji.
Kumbuka: Usingejikana kusoma kwa bidii kidato cha nne kamwe usingekanyaga kidato cha tano wala chuo.
Na usipojitoa kusoma kwa bidii kidato cha sita daima huwezi kufika chuo kikuu ama diploma. Hivyo unayoyafanya leo ndiyo yataamua kesho utakapokuwa. LET'S DOING THINGS TODAY IS ONLY YOUR RIGHT MOMENT.
USIPOLIMA LEO USITARAJIE KUVUNA KESHO.